A
Anonymous
Guest
Jamii Forums naomba msaada kwenu.
Nipo kata ya Mlandizi, Kitongoji cha Msufini, Mtaa wa Kilimanjaro. Kuna changamoto ya Uhaba wa maji kutoka, huu ni mwezi wa pili sasa. Wakati wa Mchana huwa yanatoka kwa masaa si zaidi ya 8 na saa 12 jioni yanafungwa - kuna baadhi ya siku yanafunguliwa mchana na jioni yanaondoka. Zipo siku kama J'mosi hayatoki kabisa. USIKU NDIO HAYATOKI KABISA.
Nimewasilisha KERO yangu kupitia Huduma kwa wateja zaidi ya mara 20 sijapewa majibu yoyote yanayoridhisha zaidi "Changamoto yako tumeichukua na tutaifanyia kazi".
Leo nimepiga simu nikawa mkali sana Huduma kwa wateja, ndipo wakaniunganisha na Engineer (+255789583203). Juhudi za kumpata Meneja hazikufanikiwa.
Engineer kanieleza wanachokifanya ni kuzuia upotevu wa maji (Water Retention) wakati wa usiku kwani kuna watu wanaiba, na vile vilevile kuhusu changamoto ya kufungua maji na kufunga akadai ni changamoto ya mfungua na mfunga Bomba.
Soma Pia: Changamoto Sugu ya Ukatishaji Maji na Ucheleweshaji wa Matengenezo Mlandizi (Pwani): Tunaomba Majibu Kutoka DAWASA
Hii ni masika, wanzauia maji ya nini? Mbona miaka yote maji yalikuwa yanatoka? Hii miezi miwili tu ndo yanaibiwa? Kama yanaibiwa si washughulike na wezi? Je, HUDUMA ya Maji inapaswa kutolewaje? Naomba msaada.