Changamoto ya kupata mke

Lavit

JF-Expert Member
May 16, 2011
14,541
31,712
Habari za weekend?

Mimi ni kijana mwenye miaka 30 sasa, nimeanza kujitegemea toka 2011 baada ya kumaliza chuo, si haba sasa nina ahueni ya maisha katika shughuli zangu za kila siku!!

Changamoto kubwa niliyonayo ni jinsi ya kupata mke, huko nyuma nafikiri niliwekeza mahali pasipo sahihi(wakati bado nasoma), mwisho wa siku nikaishia kuumizwa tu hali ambayo ilinifanya niwepowepo tu na mapenzi nishindwe kuyapa uzito unaostahili!

Huku mtaani kila nikijaribu kufurukuta nakutana na vikwazo, either nakutana na mabinti wa 20's ambao habari ya kuolewa si kipaumbele kwao, nikigeuka upande wa pili nakutana na single moms na vituko vyao, sasa huwa nikichanganya na yanayosemwa humu MMU navunjika moyo kabisa!!

Ninachouliza, ni mbinu gani zapaswa kufuatwa ili kupata mtu mwenye utayari na ndoa, najua wapo wanawake wengi wanaotamani kupata wanaume wenye utayari wa kuoa!! Lakini je nakutana nao wapi?
 
Basi ndugu, nawasihi, kwamba nyote mnene mamoja; wala pasiwe kwenu faraka, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja.

Bado endeleee ukiona ivyo ata we bado ujafika kwenye ndoa
 
ili sasa lishakuwa tatizo sugu inabidi selikari iingilie kati mana hali ishakuwa mbayaa wanaume tumekata tamaa kabisa ya kupata majiko

ila najiuliza kwann vijana wa vipato vya kawaida tena wengine tumewaajili ktk vitega uchumi wanaWAKE na wanaishi maisha ya AMANI
why sisi wenye kiasi cha mboga kazi ya uhakika wengne gari za kutembelea nyumba nk
lkn tunalandalanda tu mitaani na kuzidi kulalamika nahisi kina sehemu tunakosea tujichunguzee sisi wenyewe kwanza udhaifu ni upi
 
Habari za weekend?

Mimi ni kijana mwenye miaka 30 sasa, nimeanza kujitegemea toka 2011 baada ya kumaliza chuo, si haba sasa nina ahueni ya maisha katika shughuli zangu za kila siku!!

Changamoto kubwa niliyonayo ni jinsi ya kupata mke, huko nyuma nafikiri niliwekeza mahali pasipo sahihi(wakati bado nasoma), mwisho wa siku nikaishia kuumizwa tu hali ambayo ilinifanya niwepowepo tu na mapenzi nishindwe kuyapa uzito unaostahili!

Huku mtaani kila nikijaribu kufurukuta nakutana na vikwazo, either nakutana na mabinti wa 20's ambao habari ya kuolewa si kipaumbele kwao, nikigeuka upande wa pili nakutana na single moms na vituko vyao, sasa huwa nikichanganya na yanayosemwa humu MMU navunjika moyo kabisa!!

Ninachouliza, ni mbinu gani zapaswa kufuatwa ili kupata mtu mwenye utayari na ndoa, najua wapo wanawake wengi wanaotamani kupata wanaume wenye utayari wa kuoa!! Lakini je nakutana nao wapi?
Pole kwa mkwamo huo ulio kupata mkuu, mtu yeyote anayetafuta kitu bora hata kama vipo vingi lazima utajiuliza njia sahihi ya kumsaidia kupata kitu chake, lakini pia yawezekana wakati hujafikia wazo la kuoa ulikuwa unawaona wengi, lakini sasa wanaweza kuwa hawaonekani kwa sababu ndani ya jicho lako unatafuta mke na sio wanawake. kwa hiyo uko sahihi kabisa kutoana kirahisi.

Lakini pia mafundisho mengine, namaarifa ulijipatia juu ya mke na utafutaji wake unaweza kuwa kikwazo kwako, pengine unaweza hisi utaota, utakuja na kukwambia nakupenda, au takuwa tofauti sana na hawa unaowaona, hii sio kweli utamuona mwenyewe na kumwambia mwenyewe nakupenda atakubali na maisha yataanza.

Wewe unakazi mbili tu, ni kuomba sana Mungu akusaidie kumpata Mke mwema, na pili kumtafuta umuone. Kuomba mi lazima lakini kujibidiisha ili umuone ni vyema pia. kwa maeneo ya mjini kama unatafuta mke wengi wanaanzi miaka 25, 26,27, 28, 29 na kuendelea, hawa mawazo ya kuolewa yanakuwa ya kweli na hisia zao zimekaa kindoa na wapo tiyari kuvumilia maisha, kadiri umri unavyakuwa mkubwa mawazo yao juu ya maisha ni bora zaidi kuliko wenye umri mdogo.

Nijichoandika hapo sio sheria ya upekee, kunaweza kuwepo tofauti za uelewa wa maisha chini ya umri huo. Jambo la msingi ni kujua tu kuwa umri nifactor ya maamuzi ya kuolewa kwa mwanamke.

Ukimweka Mungu akusimamie, usijiulize sana mtakutana wapi, paweza kuwa popote, jambo la msingi ukihisi unaona mahali kama ni penyewe endelea kumwomba Mungu akusaidie, wakati mwingine shetani hujipenyeza kuharibu mwenendo wa kimungu, hivyo kila hatua muulize Mungu.

Jihadhari na haya, Usidhani kwa kuwa umeomba atakuja geto, usifikiri Mungu atamleta kwenye daladala au rafiki atakwambia vipi huyu, au utaota mnakwenda shopping, yaweza kuwa ndiyo lakini ondoa kabisa akilini, kuomba ni nyenzo ya kurahisisha mambo lakini application lazima ifanyike ili upate kazi. lazima utumie utashi wako, lazima uangalie wapi unapata hisia.

Hivyo jiweke sokoni kila wakati saa na dakika, najua unanielewa nikesema jiweke sokoni.

Jioni Njema.
 
Dah hiyo ni changamoto sana siku izi, usishangae hauko peke yako...yeyote aliye makini na anataka mwanamke makini maishani atakiri ni changamoto japo inawezekana kabisa, endelea ivo ivo kutafuta usikate tamaa japo uvumilivu ni muhimu sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom