Changamoto ya kazi katika mashirika ya kujitolea ya jamii

Idrissou02

JF-Expert Member
Jul 31, 2018
354
643
Miaka kadhaa iliyopita nilipata kazi kwenye shirika moja la maendeleo ya jamii.
Katika shirika ilo nilipelekwa kijijini sana uko mkoani Tabora ambapo niliyekua nalipwa mshahara ni mimi pekeangu huku wanachama wengine wa shirika wakifanya kazi ya kujitolea na kupokea tu posho ndogondogo.

Asee nilipata changamoto sana kwenye iyo kazi, wanachama wanajua kabisa kazi yao ni ya kujitolea na wakakubali kufanya shughuli za shirika lakini ikawa mimi naonekana kana kwamba ndie ninafaidi pesa za shirika na figisu nyingi sana zilianza kunikumba.

Nani mwenye uzoefu wa kufanya kazi kwenye mashirika ya aina hii atoe experience yake hapa
 
Nshawahi kufanya World Vision baada ya kumaliza form6 nlifanya mwaka1 tu nikaenda zangu chuo nikiwa nina kila kitu ndani ya gheto si unajua miradi ya UKIMWI ni seminars na mafunzo pesa ambazo ku-Audi ni ngumu kuliko ADP ambapo wanataka vitu tangible.

Ada ya mwaka wa kwanza nlilipa full baadae nikawa refunded, maana mwaka 2005 tulipata 100% ya mkopo.
 
Back
Top Bottom