CHANGAMOTO WaTZ -Kuinua Uchumi Wetu: Sasa Na Siku Za Usoni, NUNUA "MADE IN TANZANIA!"

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,403
1,241
Watanzania wenzangu, katika kipindi hiki kilichojaa shamra shamra za kufunga mwaka, naomba tusherehekee kwa mavazi yenye asili ya Kitanzania, yanayotokana na malighafi kutoka Tanzania na yaliyobuniwa na Watanzania.

Bidhaa 'feki' nchini mwetu kutoka pande mbalimbali za dunia zimezidi na zinazidi kuongezeka. Kuanzia bidhaa za umeme, madawa, nguo na hata vyakula zisizo kidhi hadhi ya kibinadamu zinazidi kutuingilia.

Hasara yake kiuchumi ni kubwa, na kikubwa zaidi ni ile hasara yake kiafya. Pamoja na kuwa kuna jambo la kutia matumaini limeanza kujitokeza hivi karibuni, maana kampeni kadhaa zimeanza kujitokeza na kushika hatamu katika kukabiliana na JANGA hili la bidhaa zisizofaa. Kwenye vyombo vya habari na pahala penginepo pengi, swala la bidhaa feki linazidi kuongelewa na tumeshuhudia bidhaa mbalimbali zikiteketezwa baada ya kugundulika kuwa hazitufai. Hivyo katika kuendeleza mapambano haya, bidii zaidi katika kuhamasisha na kuelimisha wananchi zinahitajika.

Ndiyo nakubali kuwa nchini mwetu hatutengenezi 'microchips', hatutengenezi 'energy serving bulbs', hatutengenezi 'mobile phone handsets' na vingine vingi. Lakini ninafurahi na kujisifia kwani tuna uwezo wa kulima zao la pamba na tunaweza kutengeneza nguo. Sasa kwanini basi tusitumie fursa kama hii kwenye sherehe za Idd, Noel na Mwaka Mpya kununua kilicho chetu 'ndani na nje'?!

Basi Wana JF na Watanzania wote, tuhamasike na kuchochea nguvu ya kuinua uchumi wetu. Tumelalamika na tumekosoa vya kutosha, sasa tutende angalau moja tu - TUNUNUE MADE IN TANZANIA. Hata hivyo naomba tu kuweka jambo moja bayana, ombi na changamoto hii siyo surutisho la mapambano yetu katika kukosoa, kukemea, kurekebisha, kufichua, kuelimishana n.k. katika mambo ya mustakabali wa Taifa letu. HII NI CHANGAMOTO KWA WATANZANIA KUFANYA KILE TUNACHOWEZA, TENA TUNAKIWEZA KIURAHISI NA KITU HIKI NI NGUO/MAVAZI!!

Miezi michache iliyopita tulishuhudia Spika wa Bunge letu Tukufu akijisifia na vazi lake la kikazi kwa vile lilibuniwa na kutengenezwa kule Uingereza. Sasa tukiacha siasa pembeni, hili swala kinamna na kwa maoni yangu ni jambo la kutia aibu. Hilo joho hata kama lingetengenezwa na "fundi Hamisi pale kwa jirani" mimi ningeliona ni jambo la kujisifia zaidi kuliko jinsi ilivyotokea.

Na cha kuleta matumaini zaidi ni kuwa, njia za mawasiliano zinazidi kuongezeka (nyezo za kutaka kujua vazi hili linaweza kupatikana wapi zinajizatiti). Pia wabunifu hapa nchini (tena wengine wenye hadhi ya kimataifa) wanazidi kuongezeka, na kikubwa kuhusiana na mavazi ni kuwa, ufanisi nao unaongezeka na kutia faraja katika mioyo ya wengi. Matukio mengi kudhihirisha hili yanatokea, na kwa waliopo hapa Dar-es-salaam basi hawana kabisaa la kujitetea wanapogundulika kuwa ni baadhi ya wale wachache wenye uwezo wa kununua bidhaa wapendazo toka nje ya nchi.

Katika kuinua pato la Taifa, kusaidia ndugu zetu walio katika biashara ya nguo/mavazi: WANA JF, WATANZANIA WOTE, SIFIENI WALE WALIOVAA "MADE IN TANZANIA", SIFIENI WALIOVAA VITENGE NA KANGA KUTOKA TANZANIA... TUDUMISHE NA KUENDELEZA VILIVYO VYETU KWA KUVINUNUA NA KUVISIFIA, KWA KUVITUKUZA NA KUVIENZI.

Tutafika tu....

Nawatakia Sikukuu Njema!


SteveD.
 
Nashukuru Bw.SteveD kwa moyo huo wa uzalendo. Afrika Kusini wana utaratibu wa ku-promote bidhaa zinazotengezwa nchi mwao.
What is Proudly South African

Proudly South African is an exciting campaign to promote South African companies, products and services which are helping to create jobs and economic growth in our country.

Supported by organized labour, organized business, government and community organizations, Proudly South African is the way for every South African to do something concrete to support job creation, and help build our young nation.

At the heart of the campaign is the Proudly South African logo. Companies who meet the standards set by Proudly South African can use the logo to identify themselves, their products and services.
. Kwa maelezo zaidi: http://www.proudlysa.co.za/
 
Naungana na nyinyi katika hii issue ya kupromote made in Tanzania, lakini ninawasiwasi........

Hizi made in Tanzania nyingi ni made in India/South Africa etc kwa maana ya kwamba wamiliki wake ni hao wageni na sina uhakika kama wanalipa kodi kihalali na kama mapato yatokanayo na mauzo ya hizo 'made in Tanzania' zinabakia Tanzania,

Made in TANZANIa ya Mohamedi Enterprises na so likes 'nahisi' ni hatari zaidi kuliko hizo substandard kutoka china na india.

Je tukimbilie wapi? kwenye michicha ya kando kando ya mabarabara yenye 'lead' kwa wingi? Mafuta ya kula ambayo yako substandard na ni machafu?


Angalia hivi viwanda vya nguo vya urafiki na vile vya mbagala (jina nimesahau), wananchi wananunua sana nguo zao! ni kipi wanachosaidia taifa? na angalia maji yao machafu wanavyoyaachia ovyo, kwanza bado wako kwenye likizo ya kulipa kodi,na kingine wamejaza wahindi/wachina hadi mlangoni (walinzi).

Sina uhakika ni wapi pa kushika, wapi pa kuchangia. Viwanda vyetu vyenyewe vya madawa ya binadamu, ubora wake uko mashakani.
 
Nimi nimekuwa napiga kampeni kwa kuwaelewesha watu kuwa Made in Tz ndiyo itakayoongeza ajira Tz, hivyo tunatakiwa sote tujitahidi kununua hivyo vitu. Ile tabia ya baadhi yetu ya kununua ati machungwa, toilet tissues, colgate nk toka sauzi kisa vina kwalite nzuri zaid inabidi tuache.

Ajira itaongezeka tu tutakaponunua vitu vilivyotengenezewa, kulimwa au unganishiwa tanzania.
 
Nimi nimekuwa napiga kampeni kwa kuwaelewesha watu kuwa Made in Tz ndiyo itakayoongeza ajira Tz, hivyo tunatakiwa sote tujitahidi kununua hivyo vitu. Ile tabia ya baadhi yetu ya kununua ati machungwa, toilet tissues, colgate nk toka sauzi kisa vina kwalite nzuri zaid inabidi tuache.

Ajira itaongezeka tu tutakaponunua vitu vilivyotengenezewa, kulimwa au unganishiwa tanzania.

Choveki, haswaa unalolisema, na kwa hapa Dar hili swala la kununua mavyakula yaliyosindikwa nje ya nchi na kutunzwa kwenye makopo na mafridge linakera sana... na cha ajabu na kusikitisha, ni pale unapoona familia inayojiweza na yenye wazazi wenye upeo wa mambo inakimbilia kununua majuice, matunda, nyanya, na majidubwasha mengine ya kwenye makopo, ili mradi tu waonekane wanaishi maisha ya majuu... to me, this is absolutely revolting!

SteveD.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom