Changamoto upatikanaji wa NaPA Reference number

Mimi niseme hiyo kazi niliifanya mwenyewe na mtendaji akawa muungwana kujifunza kwani nikamwelekeza nini afanye, niliwasiliana na wadau TCRA wakafungua hiyo akaunti ya mtendaji wa mtaa baada ya kutuma taarifa zake kama email, majina matatu, mtaa, namba za simu.
Hahaha kwamba wewe siyo govt official ila ukawaambia TCRA wamfungulie akaunti WEO?

Katika ishu sensitive kama ya mtu kuomba mkopo? Hahaha sawa bwana
 
Ndvy ilivyo mzee, mana bila mtendaji huchomoki...ukishindwa kabisa chukua namba ya mtendaji wako ichome kwa watu wa napa, wanampigia simu
 
Naelewa kinachohitajika.

Naelewa pia kwa kawaida akaunti za mifumo za watumishi wa LGAs hufunguliwa na IT wa Halmashauri.

Ila kusema kwamba mtu siyo IT wa Halmashauri au Afisa yeyote serikalini awapigie TCRA ili wamfungulie akaunti WEO hii haiingii akilini.
 
Ni kweli haiingii akilini ila inawezekana, nahisi wanacheki kwny mfumo kama Mtaa fulani Mtendaji kasajiliwa, kama hajasajiliwa wanafanya follow up wanamsajili...though ni kazi ya halmashauri, hata kusajili mtegemezi wa anwani ni kazi ya mtendaji wa mtaa ila kama ukiwapigia cm na ukaweza kuthibitisha kuwa unakaa nyumba fulani labda kwa kutoa namba ya simu ya mmiliki ambayo inalingana na surname yako basi wanakusajili vizuri tu.....mi nilipiga kwny namba zao
 
Hahaha kwamba wewe siyo govt official ila ukawaambia TCRA wamfungulie akaunti WEO?

Katika ishu sensitive kama ya mtu kuomba mkopo? Hahaha sawa bwana
Mimi pia ni gvt official vilevile na huyo VEO ananitambua.
 
Mbona mfumo ni mzuri na rahisi kutumia.
Ishu ya msingi ni watendaji wapewe maelekezo ya masaa 2 tu kazi inafanyika.
Nimefanya kazi hii kwa kijana wangu na akamaliza ndani ya siku 3 aka submit maombi ya mkopo bila shida yoyote.
Nilisoma kupitia youtube akaunti ya NaPa.
Nikaenda kwa mtendaji nikampa maelekezo, akasajiliwa. Nikarekebisha taarifa zoezi likaisha.
Huyo mtendaji kwa mfano huku zanzibar masheha hawafahamu chochote mimi Nimeingia NaPa nimefanya mpaka nimefikia kupata zile reference number kwa mfano 3630OK221 lakini hatua ya kupata ile barua ndio shida, reference ambazo nimepata kwa applicant ukirudi kwenye mfumo wa bodi kuiweka unakuja ujumbe bado hazijakuwa approved.

Lakii pia nataka kujua hivi ni kila mmoja inabidi apate reference namba yake? kwa mfano baba mama na mdhamini?

Kama una link inayoelekeza zaidi tunaomba mkuu
 
Halmashauri wanajivuta sana.
Piga simu, wacheki wasap kwa kujitambulisha kama mtendaji wa eneo husika utasikilizwa kwa mfumo huu
Jina:
Mkoa:
Wilaya:
Kata:
Mtaa:
Email:
Phone:
0738938757
0658098809
Mimi nishasajiliwa tayari kwenye mfumo wa makazi lakini mbona nikiweka ile Reference No kwa ajili ya barua barua haiji? Kwanini barua siipati na nikijaza ile reference number kwenye mfumo wa bodi inasema bado haijakuwa approved?
 
Huyo mtendaji kwa mfano huku zanzibar masheha hawafahamu chochote mimi Nimeingia NaPa nimefanya mpaka nimefikia kupata zile reference number kwa mfano 3630OK221 lakini hatua ya kupata ile barua ndio shida, reference ambazo nimepata kwa applicant ukirudi kwenye mfumo wa bodi kuiweka unakuja ujumbe bado hazijakuwa approved.

Lakii pia nataka kujua hivi ni kila mmoja inabidi apate reference namba yake? kwa mfano baba mama na mdhamini?

Kama una link inayoelekeza zaidi tunaomba mkuu
Kila mmoja inabidi apate reference namba yake.
Mama wa muomba mkopo.
Baba wa muombaji mkopo.
Muombaji mwenyewe.

Barua utaipata endapo mtendaji ataidhinisha ombi lako kwenye app ya Napa DC live
 
Mimi nishasajiliwa tayari kwenye mfumo wa makazi lakini mbona nikiweka ile Reference No kwa ajili ya barua barua haiji? Kwanini barua siipati na nikijaza ile reference number kwenye mfumo wa bodi inasema bado haijakuwa approved?
Mtendaji wako ndiye mwenye mamlaka ya kuidhinisha ombi lako kwenye mfumo wa NaPa.
Bila hivyo ombi linakua ni batili.
Iwapo hataidhinisha ndani ya masaa 24 maombi yako yataenda kwa mratibu wa makazi ngazi ya wilaya.
 
Kila mmoja inabidi apate reference namba yake.
Mama wa muomba mkopo.
Baba wa muombaji mkopo.
Muombaji mwenyewe.

Barua utaipata endapo mtendaji ataidhinisha ombi lako kwenye app ya Napa DC live
Naomba hiyo app ya Napa DC Live ili nimpelekee mtendaji wangu afanye approval
 
App wanapewa mkuu na watehama wao wa wilayani ama wale walioko mawasiliano..
Hakikisha amesajiliwa ndipo atakua na uwezo wa ku access hiyo app.
 
Sasa kama App wanapewa mkuu wa tehama wa wilayani huku kwetu hao watu bado hawajawezeshwa na dirisha la maombi limeanza wanafunzi wanahangaika, ukienda kwenye huyo mjumbe/sheha kumueleza jambo hili ata hakuelewi hafahamu kabisa
 
Ndvy ilivyo mzee, mana bila mtendaji huchomoki...ukishindwa kabisa chukua namba ya mtendaji wako ichome kwa watu wa napa, wanampigia simu
Sasa mtendaji akipigiwa simu na napa, Labda mtendaji 1 atakuwa na watu 100 kwenye shehia yake ambao wataomba mkopo hawa wote atawaidhinisha kwenye simu atakayopigiwa? au Mtendaji akiingia jina lake tu inatosha watu wake kutambuliwa kwa wale washaojisajili na kupata ref number??
 
Back
Top Bottom