Changamoto kwa wahitimu vyuo vikuu

Damson88

JF-Expert Member
Jul 29, 2011
259
24
Ndugu zangu wana JF, mimi ni mhitimu wa chuo kimoja hapa nchini,nimesomea mambo ya ujasiriamali haswa hivyo inabidi nijiajiri mara baada ya kuhitimu na muda wenyewe ndiyo huu. Ubunifu ninao tena mkubwa sana bila kusahau kuwajari wateja au wanaohitaji huduma zangu. Mfano-na design website, fundi computer n.k. Sasa swali linakuja hivi:- nikiajiriwa(kama ajira zipo) ntafanya kitengo gani? maana mimi ni mtu anayepaswa kujiajiri. Je, mtaji wa kuanzisha biashara ntaupataje? Au niende jeshini TPDF? naomba mwongozo na mawazo yenu nayaheshimu sana. Ahsante!​
 
kwa maisha ya sasa ni bora ujiajiri kaka tumia ubunifu na elimu yako vizuri, suala la mtaji itakubidi uanze na kile kidogo ulicho nacho, wengi waliofanikiwa walianza na kidogo wakakiendeleza, kupata mikopo nowdays masharti magumu especially ukiwa ujaanza, cha muhimu mtangulize Mungu katika maisha yako!
 
kweli wew lito angel...nashukhuru sana kwa mchango wako wa kimawazo na uliyoandika ni ukweli kabisa kwa hali tuliyonayo
 
Back
Top Bottom