Changamoto kwa mabinti wengi

mrsfulani

Senior Member
Oct 19, 2015
113
69
Habari zenu wanajamvi..

Kuna changamoto ambayo mabinti wengi ikiwemo mimi pia inanihusu ni ile mtu unamaliza chuo vizuri ila unakuwa katika mahusiano linakuja suala la kutafuta kazi apo ndo inakuwa ngumu hasa katika mahusiano yale ambayo yapo serious kwa future sio michepuko tu.

Suala la kupata kazi au kutafuta kazi mbali na mume wako au mtarajiwa wako na mapenzi ya mbali yamekuwa ni chanzo cha magonjwa na hayadumu kabisa katika maisha ya siku hizi.

Jamani kina dada kina mama au wanaume pia waliopitia katika kufanya hayo maamuzi mlifanyanje kuchagua kazi mbali na mtarajiwa mkakubali litakalo kuwa na liwe manake kila kitu kina umuhimu wake kazi ina umuhimu mahusiano pia yana umuhimu,nipo njia panda kazi mkoa niliopo na mume nimejiataidi kutafuta nimekosa ila nikiulizia mikoani uko napata tu naambiwa ni wewe tu kazi zipo njo.

Naomba msaada kwa hili mliofanikiwa katika maamuzi.
 
nikiulizia mikoan uko napata tu naambiwa ni wew tu kazi zipo njo
Naomba msaada kwa hili mliofanikiwa ktk maamuzi.

Hapa inaonesha hujatuma maombi sehemu husika bali unauliza kwa mtu unayemfahamu sasa 'huyu' ama 'hao' unaowauliza huko mikoani niwa jinsi moja na wewe?
 
Erh ndio mtambue kuwa ndoa sio kugegedana na mabusu...mwanaume akitaka kuoa lazima atambue kuwa hatakiwi kuishi mbali na mke wake...pale ambapo mke wake hana kazi basi lazima yeye aweze kumtimizia mahitaji mke wake bila kutetereka....kuoa na kuolewa kunahitaji kujipanga. Ila pongezi kwako kwa kutambua kuwa long distance relationsships dnt work.
 
Umbali unaweza kuvunja penzi lakini kama penzi lina mizizi ya mbali basi umbali huwa kiungo na kipimo sahihi cha penzi
 
Omba Mungu and make a decision nenda ukafanye kazi, I met him nilipokuwa sehemu kikazi, when I least expected,rizq yako ya ndoa anapanga Mungu ukute ndo anakuitia huko akupe,
 
Back
Top Bottom