Mwanamalundi
JF-Expert Member
- Aug 30, 2007
- 3,125
- 1,432
Mkuu,
Uwaziri siyo right ni privelage. Kama jinsi kupewa uwaziri kusivyo kupendelewa, kukosa uwaziri haiwezi kuwa kuonewa.
Mkuu naomba unisome vizuri. Wameonewa kwa sababu waliosababisha hayo madudu bado wamo wizarani wanaendelea kupeta na kupika madudu mengine. Mbona hatujasikia kwamba waliosababisha yale madudu wameshughulikiwa? Ndio maana tunasema huu ni uonezi. Na hao mawaziri waliopewa hizo wizara wanatakiwa kuwa makini sana. Vingenevyo, itakula kwao next time. Just wait, time will tell.
Ndio siasa ilivyo..........hakuna uonevu kwa kazi ya kupewa......utaonewa kama uliihangaikia kazi
Tatizo ni kwamba wengi walikuwa fixed baada ya kuonekana mitandao yao ya 2015 haisomi ramani mmoja na mkulu. Kama huamini kwa nini G. Mkuchika pamoja na kashfa kubwa kugusa wizara yake hajaondolewa? Je, Jumanne Maghembe ameondoka? Selina Kombani alipinga uwepo wa katiba mpya lakini anapeta. Tatizo ni mitandao mkuu kuelekea 2015. Sijasema hawajala rushwa kwa hiyo wameonewa - hapana. Nimesoma hoja ya kubaki au kuondolewa siyo Rushwa ni mtandao. Unaweza ukala rushwa wazi wazi na ukapeta vile vile. Je, tutafika 2015 salama? Kwa neema ya Mungu, YES, and thati is my prayer.
Mimi Msimamo wangu bado uko palepale. Haiwezekani waziri peke yake tu ndio awajibike wakati waliosababisha hayo madudu bado wanapeta. Basi serikali itamke wazi kuwa Mabadiliko ya baraza la mawaziri yalikuwa ni mabadiliko ya kawaida ambayo hayana uhusiano na "fiasco" iliyotokea bungeni mwezi April. Hapo nitaelewa. Vinginevyo, mimi bado nasema akina Maige na Ngeleja walionewa.
Kawaida hatuendi hivyo.........ni rahisi kumuwajibisha mwanasiasa(waziri- hana mkataba wa ajira) kuliko mtendaji (ana mkataba huyu)......kwa utuuzima wangu hii ni mara yangu ya kwanza kusikia Mawaziri wakilalamika kuondolewa.......miaka yote haya hufanyika na kuisha kimyakimya tu.....hata Lowassa aliwekwa benchi na Mkapa kwa muda tu (1995-1997)
Mkuu naomba unisome vizuri. Wameonewa kwa sababu waliosababisha hayo madudu bado wamo wizarani wanaendelea kupeta na kupika madudu mengine. Mbona hatujasikia kwamba waliosababisha yale madudu wameshughulikiwa? Ndio maana tunasema huu ni uonezi. Na hao mawaziri waliopewa hizo wizara wanatakiwa kuwa makini sana. Vingenevyo, itakula kwao next time. Just wait, time will tell.
Kwani kunyimwa uwaziri ni adhabu? Wale wabunge wengine ambao hawajapewa uwaziri wako kwenye adhabu? Wewe umeshawahi kuteuliwa na Rais kushika nafasi yoyote? if not, je uko kwenye adhabu?
Ndio maana nakwambia walipopewa uwaziri walipewa privelage, sasa uwaziri amepewa mwingine, huyo ni zamu yake kupata privelage. Hakuna aliyeonewa, wangekuwa wameonewa iwapo wangevuliwa Ubunge walioupata kwa jasho lao baada ya kunadi sera kwa wananchi sio uwaziri...
watu washaeka vindumba vyao hawag'oki hata kwa dawa
Kaka, adhabu na kuonewa ni vitu viwili tofauti. Nisome vizuri. Sijasema kwamba hawa jamaa wamepewa adhabu. Nimesema wameonewa. Ndio maana serikali haijachukua hatua yoyote kwa watuhumiwa waliosababisha ile "fiasco" ya April,2012.
kama mlimsoma vizuri jk alipowa-
drop mawaziri yao alionesha wazi kuwa wao ha
hawakuwa watndaji wabaya ila wale wsliochini yao. hataivyo aliahaidi kuchukua hatua dhidi yao mpaka leo hajafanya hivyo.
Nadhani ingekuwa vizuri kama ungechambua tuhuma za kila waziri halafu ueleze ni kwann walisingiziwa. Hii si hoja bado.
Samahani Lakini