Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,804
- 12,251
Katika kampeni za uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2010, Dr. Chami aliwahamasisha wananchi wa Moshi Vijijini na kuwezesha kukusanya kiasi cha Sh. 50,000,000/= ili zisaidie kampeni za urais wa JK. Matunda ya kazi hii nzuri Chami anaamini kuwa iliwezesha yeye kuteuliwa kuwa waziri wa viwanda na biashara na hivyo kujiaminisha kuwa atakuwa waziri kwa kipindi chote cha miaka mitano ya utawala wa JK.
Kitendo cha JK kumwondoa katika baraza ya mawaziri kutokana na kashfa zilizoibuliwa na CAG kumemletea machungu na mateso makubwa na kumfanya yeye na baadhi ya wapiga kura wake kuona ameonewa kutokana na mchango mkubwa alioutoa katika kufanikisha kampeni za urais wa JK.
Kwa kuwa Chami ameendelea kulalama na kuomba wapiga kura wake wamuombee ili asiadhirike, je Chami anataka kutuaminisha kuwa mchango alioutoa ili kufanikisha kampeni za JK ilikuwa ni rushwa au sehemu ya kumshawishi JK amfikirie katika moja ya nafasi za uwaziri?