Chami alinunua uwaziri?

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,796
12,239
Katika kampeni za uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2010, Dr. Chami aliwahamasisha wananchi wa Moshi Vijijini na kuwezesha kukusanya kiasi cha Sh. 50,000,000/= ili zisaidie kampeni za urais wa JK. Matunda ya kazi hii nzuri Chami anaamini kuwa iliwezesha yeye kuteuliwa kuwa waziri wa viwanda na biashara na hivyo kujiaminisha kuwa atakuwa waziri kwa kipindi chote cha miaka mitano ya utawala wa JK.

Kitendo cha JK kumwondoa katika baraza ya mawaziri kutokana na kashfa zilizoibuliwa na CAG kumemletea machungu na mateso makubwa na kumfanya yeye na baadhi ya wapiga kura wake kuona ameonewa kutokana na mchango mkubwa alioutoa katika kufanikisha kampeni za urais wa JK.

Kwa kuwa Chami ameendelea kulalama na kuomba wapiga kura wake wamuombee ili asiadhirike, je Chami anataka kutuaminisha kuwa mchango alioutoa ili kufanikisha kampeni za JK ilikuwa ni rushwa au sehemu ya kumshawishi JK amfikirie katika moja ya nafasi za uwaziri?
 
Anaposema aombewe ili asiathirike ina maana kubaki na cheo cha Mbunge halipwi? au kuna tofauti kubwa sana kati ya anacholipwa waziri na mbunge?

Viongozi wa kisiasa hapa Tanzania wakichukulia nafasi zao za kisiasa kama ajira nyingine Taifa litaendelea kubaki nyuma kimaendeleo. Nilitegemea kuachwa kuwa waziri ingekuwa fursa nzuri kwake kutetea wananchi wake ndani ya Bunge. Mfano wakati wa kampeni alileta "Bulldozer" na raisi Kikwete aliahidi kumalizia barabara zile lakini baada ya wao kuchaguliwa (yeye na Kikwete) hakuna kinachoendelea pengine huku ndiko kuathirika anakozungumzia.
 
Bora arudi jimboni kuja kutatua kero huku. Huyu bwana alibweteka sana na uwaziri. Mara tu baada ya kuteuliwa kuwa waziri alimtuma diwani mmoja kutoka kibosho azunguke jimboni kote kuwaeleza wananchi eti.... kutokana na mmbunge wetu kuteuliwa kuwa waziri, hatopata nafasi ya kutembelea tena wapiga kura wake. Badala yake huyo diwani ndo engekuwa anasikiliza matatizo yetu na kumpelekea chami! Sisi tukuchague wewe kuwa mbunge wetu... halafu wewe ukamchague mtu unayemtaka wewe kutuwakilisha???? Wapi na wapi. Sijawahi kusikia tokea nizaliwe!
 
Sasa amepewa nafasi ya kuzunguka jimboni kwake analialia tena kwanza Afya yake hamruhusu majukumu makubwa ya Uwaziri tena aje jimboni huku akutane na nyuso za mbuzi ndio atakoma
 
Story nyingine Bw ! source yake huwezi jua labda hii ya ugonjwa ndio inaweza isimrudishe lkn kachangisha 50m kampelekea Mkuu wapi na wapi maana meneja wa kampeni ni shemeji yake na kiasi hicho hakikufika hata nusu.
Uwaziri ulitegemea @ mkoa au wilaya CCM ilikoshinda
 
Uwaziri au cheo chochote cha kuteuliwa na mkweree inategemea jinsi unavyojikomba kwake au familia yake basi!! Chunguza teuzi zake zote utakuta ni hivyo; wakina Maneno sasa DC wa Kigoma elimu yake darasa na saba!!
 
Bora arudi jimboni kuja kutatua kero huku. Huyu bwana alibweteka sana na uwaziri. Mara tu baada ya kuteuliwa kuwa waziri alimtuma diwani mmoja kutoka kibosho azunguke jimboni kote kuwaeleza wananchi eti.... kutokana na mmbunge wetu kuteuliwa kuwa waziri, hatopata nafasi ya kutembelea tena wapiga kura wake. Badala yake huyo diwani ndo engekuwa anasikiliza matatizo yetu na kumpelekea chami! Sisi tukuchague wewe kuwa mbunge wetu... halafu wewe ukamchague mtu unayemtaka wewe kutuwakilisha???? Wapi na wapi. Sijawahi kusikia tokea nizaliwe!

Wabunge wengi hudhani kuwa kwa kuteuliwa kwao kuwa mawaziri kunawafanya kuwa mabosi wa wananchi hivyo badala ya kushirikiana nao kujadili changamoto za maendeleo hutoa maagizo kwa wapiga kura wao kwa kisingizio wana majukumu mengi nya kitaifa!
 
With all the brain he has, he might end up as a loser...he should know his destinations belongs to him. Kufanya kazi za kisanii sanii badala ya kulisaidia Taifa mwisho wake ndio huo
 
Story nyingine Bw ! source yake huwezi jua labda hii ya ugonjwa ndio inaweza isimrudishe lkn kachangisha 50m kampelekea Mkuu wapi na wapi maana meneja wa kampeni ni shemeji yake na kiasi hicho hakikufika hata nusu.
Uwaziri ulitegemea @ mkoa au wilaya CCM ilikoshinda

Wewe ni mmoja wa wapambe wake unajuaje kuwa hazikufika hata nusu!?
 
Natamani kuonana sana na huyu ndugu nimkumbushe aliyotuahidi wakibosho naye angalau atujuze alichotekeleza na kwa % ngapi!! Ikishindikana bac tutavumilia tu mpaka 2015.kwan kama ni makosa tulishafanya.WELCOME home munama!!! "GLORIA DEO PUX OMNIBUS!!
 
Aliwachangisha sana kina mangi wenye maduka Kariakoo. Ila baada ya kupewa uwaziri wa viwanda mikopo kwa hao kina mangi ilikuwa nje nje bila dhamana ya chochote. Sasa baada ya kuondolewa ni wazi kina mangi hao hali zao kwa kweli sijui zitakuwa je. Hata hivyo mangi kwa kawaida hana njia moja ya kutokea kimaisha, hubadilika kulingana na mazingira.
.
 
Huyu jamaa anapenda sn uwaziri. Hata kipind kile cha lowasa kujiuzuru na jk kuteua baraza jipya la mawazir alikua roho juu akakusanya ndugu zake wote kwenda kibosho wamwombee ili achaguliwe tena.
 
Huyu jamaa anapenda sn uwaziri. Hata kipind kile cha lowasa kujiuzuru na jk kuteua baraza jipya la mawazir alikua roho juu akakusanya ndugu zake wote kwenda kibosho wamwombee ili achaguliwe tena.

Inaelekea ana allergy ya uwaziri!
 
Back
Top Bottom