Chama pinzani ndilo jina la milele la chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chama pinzani ndilo jina la milele la chadema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by HAMY-D, Sep 19, 2012.

 1. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Kuna harakati nyingi sana zinafanywa na hichi "chama cha wavaa magwandwa" katika operesheni tofauti tofauti kwa lengo la kutwaa dola.

  Ingawa viongozi wa chama hiki wamekuwa wabunifu wa kutumia njia mbalimbali kama mikutano ya hadhara, maandamano yasiyo na vibali, fujo na shari, kutoheshimu mamlaka zilizopo na mbaya zaidi kutokuwa na nidhamu na ustaharabu wa wabunge wa chama hiki katika bunge letu tukufu la jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuathiri mara kwa mara shughuli za bunge kufanyika kama ilivyopangwa na kufanya heshima na thamani ya bunge kumomonyoka mbele ya jamii ndani ya nchi na hata nje ya nchi.

  Yote haya wanafanya kwa lengo la kujipatia umaarufu, taifa liwatambue kuwa wao ndio tumaini la ukombozi wa taifa, liwajengee imani kuwa wao ndio watabadili hali za watanzania wa chini kabisa na kuwapa unafuu wa maisha.

  Uongo wa waziwazi wa wavaa magwanda ndio huu, kujifanya wanajali kundi la walalahoi huku wao ndio vinara wa kula bata mjini, wanachukua pesa za wavuja jasho kwa kigezo cha kuchangia chama wakati wanapata ruzuku kutoka serikalini ambayo hatujui pesa hizo za walipa kodi wanafanyia nini.

  Ila tunaona wananunua helikopta mpya na magari ya hanasa, hapo wananchi tunajifanya kama hatuoni matumizi mabaya ya hawa watu. Safari zisizoisha za marekani na mataifa mengine yaliyoendelea ndio desturi na tamaduni ya wavaa magwanda. Haya yote mnayafumbia macho na kujifanya HAMUONI?

  Ila bado kuna kundi kubwa la watanzania wazalendo, wapenda amani, wapenda muungano na mshikamano, wameonyeshwa kuchukizwa na siasa za CHADEMA na kuomba kifutiliwe mbali ili kiepushe michafuko inayoweza kutokea kutokana na siasa yao chafu, ya uchonganishi na ya kibabe.

  Wananchi wengi wameonyesha kutokuwa na imani na hiki chama cha demokrasia na maendeleo kufuatia ukosefu wa maadili wa viongozi wake. Ninawachambua kama ifuatavyo (m/kiti na katibu wa chama)

  1. Mwenyekiti wa chama ni mmiliki wa kumbi za starehe kama nightclubs, bars na guest houses. Pia alikuwa DJ katika kumbi za starehe kadhaa hapa mjini.

  Kuhusu elimu naomba nisiliongelee kwani ndio mwenyekiti wa chama cha siasa mwenye kiwango cha chini kabisa cha elimu hapa nchini.

  Vilevile ni mfanyabiashara mkubwa wa kimataifa, kama ilivyo ada siku zote,hakuna mfanyabiashara asiyekuwa mnyonyaji. Sasa kazi kwetu watanzania kuendelea kumuwekea imani mtu kama huyu.

  2. Katibu wa chama hiki amekumbwa na misukosuko mingi hivi karibuni, kuna thread humu muitafute inaeleza ufisadi ndani ya chadema ili muweze kumjua huyu mtu vizuri.

  Kwa taarifa zilizonyooka kabisa ni kwamba ni mzoefu wa mechi za mchangani na mechi za kirafiki, halafu ikumbukwe alikuwa padre na tunafahamu wote, misimamo ya ma-padre wote ulimwenguni ni ipi, sasa mtu huyu anaonyesha wazi kutoweza kuvumilia na kutokuwa na msimamo thabiti wa anayoyaamini.

  Hafai kupewa taifa kwani ni rahisi kwa mtu huyu kushawishika na kubadili mwelekeo mzima wa maamuzi yake, ambayo yataathiri taifa. Hapa nawakumbusha ile kauli yake ya kutomtambua mheshimiwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, yeye na magwanda mengine ya chadema.

  Baada ya muda mfupi tukamsikia anataja jina la jembe letu, mkombozi wetu wa taifa, kipenzi cha walalahoi na adui wa mafisadi, his excellency the president of united republic of Tanzania dr. Jakaya.M.kikwete kwa upole, nidhamu na unyenyekevu wa hali ya juu.

  Mnaweza mkapima wenyewe kuona mtu kama huyu anafaa kusimama kama rais wetu. Kwa niaba ya wengi nachukua nafasi hii kuwajibia. Jibu ni HAPANA.

  Kwa hali hii ya vingozi wa chadema kutokuwa na sifa shindani na wale wa chama tawala nikimaanisha CCM, basi niitimishe kama ifuatavyo.
  "CHAMA PINZANI NDILO JINA LA MILELE LA CHADEMA".
   
 2. N

  Nonda JF-Expert Member

  #2
  Sep 19, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  HAMY-D
  Ikiwa mwalimu ameweza kuwa Rais,Mwandishi wa habari ameweza kuwa Rais, Mwanajeshi anaweza kuwa rais katika nchi hii sio vibaya pia kwa DJ au mwengine yeyote kuwa Raisi. Kubadili fani/ kazi inakatazwa siku hizi?

  Au nani katika CHADEMA unataka agombee Uraisi?

  Msikilize DJ hapa katika video.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #3
  Sep 19, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Hisia zenu ambazo zinakoshwa na huyu mvaa magwanda zitaliponza taifa. Wananchi hawana imani nae hilo unaliongeleaje?

  Chadema kibaki kuwa pinzani ili kiisimamie serikali vizuri, maana na magwanda yao hiyo kazi ya ulinzi ulinzi wanaiweza.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Sep 19, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Tanzania bila CCM inawezekana.
   
 5. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #5
  Sep 19, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,199
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Hizi ni thread za kipumbavu za kutafuta umaarufu hapa jamvin kupitia Chama kinachopendwa na rika lote. Kama ulikuwa hutafuti umaarufu kwanini hukuandika CUF? Nikwasababu thread yako isingechangiwa na mtu yeyote !!!!! Tafuta tena tittle nyingine ya kuiponda CDM Kama "Mbowe na Dr Ndalichako ni ndugu"
   
 6. LEGE

  LEGE JF-Expert Member

  #6
  Sep 19, 2012
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 4,914
  Likes Received: 5,351
  Trophy Points: 280
  mkuu mbona jana ilikuwa juma 4 ni vipi kwani ukaamka na pombe ??? Au ndoto za kuokota mashilingi usingizini zinakukumba sana na kukusumbua??? Inaonekana mwanzisha thread hii ni kikojozi. BISHA?????
   
 7. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #7
  Sep 19, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Utasubiri mkono wa binadamu udondoke kwa muda mrefu bila ya mafanikio kama fisi vile. Tanzania ya leo, ukiongelea siasa ni CDM, kama hujui kufa kachungulie kaburi.
   
 8. n

  nrashu Senior Member

  #8
  Sep 19, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wanabodi,
  Mtoa hoja inabidi afahamishwe tofauti ya elimu, kuelimika, na busara. inavyoonekana haelewi tofauti ya hayo maneno matatu. Je tunataka viongozi wenye elimu kubwa au walioelimika? tunahitaji viongozi wenye elimu kubwa au wenye busara? Kuitwa DKT au Profesa haina tija kama huwezi gundua tatizo linalokusibu. Tofauti kubwa ya Wanyama na binadamu ni kwamba mwanadamu anaweza kuforecast na kupangilia mambo ya mbele miaka hata 50 ijayo.
  ukiona kila kitu kinahudumiwa jinsi kinavyokuja (ADHOC), hamna tofauti kati yetu na wanyama.

  Hizo elimu (CV) tunazo nyingi sana huku kanda ya ziwa lakini maendeleo yetu ni aibu tupu. afadhali hata wahadzabe wanaojua kuweka mitego ya kitoweo cha kesho. Nini kimetokea lake victoria? je hao wenye elimu hawakuwepo? nini kinatokea kwenye raslimali za taifa letu? Je wenye elimu hawakuwepo? nini kinatokea kwenye mfumo wetu wa elimu? je wenye elimu hawakuwepo?
  Nipe CV ya wajasiriamali wakubwa Tanzania!!! na uangalie wameajiri hao unaowaita wana elimu wangapi? acha kupofushwa na Elimu, nenda mbele zaidi uangalie outcome.
  Tafakari vizuri na uchukue hatua.
   
 9. fugees

  fugees JF-Expert Member

  #9
  Sep 19, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 2,587
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  Umechomekwa vijiti masikioni harafu et udajidai unasikia kweli. Mleta mada inabidi utoe vijiti hivo ila kama poa viache.
   
 10. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #10
  Sep 19, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Aliyeko madarakani na Udaktari feki amefanya nini, mbona yeye ndio mnyonyaji namba moja, sitashangaa kama nae atakuwa na mapesa huko uswisi c/o Riz1
   
 11. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #11
  Sep 19, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  "Kuna harakati nyingi sana zinafanywa na hichi "chama cha wavaa magwandwa" katika operesheni tofauti tofauti kwa lengo la kutwaa dola".

  Acha kukurupuka ndugu yangu,hata hujui unaandika nini.Ila zingatia hili"ukisikia mbwa anabweka bweeeeeeee!Ujue jiwe limempata"kila la kheri!
   
 12. j

  jossy chuwa Member

  #12
  Sep 19, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM ni kama kifo cha nyani tu kila mti unatereza! masikini weee huruma!
   
 13. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #13
  Sep 19, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  HAMY-D, Salute,

  Nimependa uchambuzi wako wa kina na wenye ujenzi kwa taifa letu ni uchambuzi murua.

  Endelea kutoa elimu ya uraia.
   
 14. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #14
  Sep 19, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 10,636
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  CDM ni kama wapiga tarumbeta harusini kelele zao hazisumbui.
   
 15. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #15
  Sep 19, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,663
  Likes Received: 3,317
  Trophy Points: 280
  Mtoa thread amejiunga jana kwa kazi hii ya kuchafua hali ya hewa humu,na wapo wawili pamoja na mwenzie anaitwa zawadi ngoda,na anayewatuma huwa anawaandikia mada ya kuileta humu na jinsi ya kui defend,ila kwa hapa jf naamini hawatadumu,kama hawataweza kuwa neutral kama ritz,watasepa kama faiza fox,au wataolewa.
   
 16. babalao 2

  babalao 2 JF-Expert Member

  #16
  Sep 19, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,218
  Likes Received: 1,271
  Trophy Points: 280
  Hii sasa kali inamaana mtu kuwa dj ni kikwazo katika uongozi wa siasa mbona kuna makonda waganga wa kienyeji wapo ni viongozi huko ccm.
  Kuhusu biashara za mbowe ule ni urithi wa wazazi wake na pia ni halali kabisa. Sasa bila uwekezaji kwenye hizo guest unataka wageni waletwe nyumbani kwako?
  Huwezi dharau bar kwani ndio mishahara ya watumishi hutokea huko au huelewi pato kubwa la mapato ya serikali yako ni kwa walevi na wavuta sigara.
  Kwa taarifa yako casino na bar ndipo TBL MALI YA UMMA HUUZA BIDHAA ZAKE.
  HEKIMA NA BUSARA NDIYO KILA KITU. ELIMU TUNANUNUA WALA HATUENDI SHULE.
   
 17. Munambefu

  Munambefu JF-Expert Member

  #17
  Sep 19, 2012
  Joined: Jun 24, 2012
  Messages: 896
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 60
  Loh!huyu Mbowe inaonekana ndani ya CCM anatajwa kwa hofu mara nyingi kuliko mtu yeyote,kila kukicha Mbowe Mbowe!na kwa taarifa yenu tunamuongeza term nyingine mtokwe povu zaidi.M4C Mbeleee!
   
 18. D

  DAVIES JF-Expert Member

  #18
  Sep 19, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 513
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Unapotosha tu huna jipya na hoja zisizo na msingi. Kwanza nakusikitikia sana kwa thread yako hii ambayo umekurupuka na kuandika pasi kufikiria, nakushauri fuatilia mkutano wa pinda mwanza ndipo utagundua nyinyiem na cdm kipi kinapendwa ndipo uweke upuuzi wako huu
   
 19. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #19
  Sep 19, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,841
  Trophy Points: 280
  Nilidhani unataka mjadala kumbe wewe unataka kejeli na matusi.


   
 20. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #20
  Sep 19, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,841
  Trophy Points: 280
  Weka hoja zako achana na vijembe na kejeli
   
Loading...