Chama pinzani ndilo jina la milele la chadema

Mkuu HAMY- D, heshima,

Naomba nikukumbushe haya;

1. Uandishi na Matumizi ya Lugha:
Kiukweli nilipata shida sana kufika mwisho kutoka na na makosa ya kisarufi mfano, hanasa( badala ya anasa), Hichi(hiki), Hustaarabu(Ustaarabu)..nk..angalau uwe unapitia tena(proof read kabla ya kuandika hoja) lakini nadhani shida ni matumizi ya lugha yetu.

2. Katika kusoma HOJA yako, UMEJICHANGANYA MWENYEWE katika Aya ya kwanza na ya tatu, kusema CHADEMA wanataka kutwaa dola na pia wanatafuta umaarufu tu...tukueleweje?

3. Katika Aya ya nne, umeuliza "CHADEMA wanakusanya pesa za walalahoi ikiwa wanapata ruzuku, na "HAMJUI" pesa hizo za WALIPA KODI zinakwenda wapi" ... sasa ingawa si mwanchama wa CHADEMA naomba nikuulize

- Umesema/Kuonyesha ufuasi wako wa CCM, sasa pesa hizo za CHADEMA zinakuhusu nini wewe?
- Unaposema "HATUJUI" zinapokwenda..ni wewe na nani?
- Uliuliza kabla ya ku-post hapa?
-Unajua kazi ya pesa za ruzuku ni ipi?Je inatosha pesa yenyewe?
-Je chama cha CCM huwa hawakusanyi/kuchangia mfuko wa chama?..kumbuka Mlimani City, pale Dodoma n.k
- Pesa hizo huwa wanfanyia nini?

3. Unaposema kila mfanyabiashara mkubwa ni "MNYONYAJI" una maana gani? ..kama UNA UHAKIKA, hebu lete orodha ya majina ya "WANYONYAJI" kutoka CCM, tufanye ulinganifu.

4. Unaposema, "kwa niaba ya wengi unaamua kutujibia" kuwa viongozi wawili uliowataja wa hicho chama yaani (CHADEMA)..Nani amekupa RUHUSA hiyo?

- Kwa hoja yako ya elimu( zaidi ya nusu ya wabunge wa TZ hawana shahada, JE bunge livunjwe?..
- Je, bunge linaundwa na wanachama wangapi wa CCM?
- Je, wenye "elimu hii kubwa" wamelifanyia nini Taifa?


Hebu mkuu, niondolee dukuduku kwa kujibu maswali haya KWA UMAKINI na kisha tuendee.
 
Hii ndio akili ya wengi ndani ya CHADEMA, hojam nyepesi zilizosheheni maneno ya aibu na upuuzi ndio misingi ya kujenga kwao hoja.

Vijana wa CCM tupo hapa kwa uzalendo wetu kuja kutoa elimu ya uraia watu waelewe vizuri siasa, hii itasaidia katika kufanya maamuzi mazuri ya kiitikadi.

CCM haitufundishi kutukana, kudharau visivyodharaulika, kuleta shari na uadui, bali CCM inatufundisha tuwe na upendo, amani na umoja. Hivi vitu ndio misingi ya maendeleo ya taifa letu, mambo ambayo chadema wanafanya kazi usiku na mchana kuyapoteza.

Kamwe nchi inayopoteza haya mambo kwa makusudi kabisa(upendo, amani na umoja) haitakuja kuyarudisha tena katika taswira ya dunia.
Hapo kwenye rangi nyekundu umenifurahisha sana kijana mjinga wa CCM! hivi kuchochea udini, ufisadi na rushwa ni uzalendo? vijana wa CCM kule Nzega walioshikiana bunduki kwa uchu wa madaraka walikuwa wazalendo? vijana wa CCM kule Igunga walioendesha mauaji ya kikatili na kumumwagia mwenzao tindikali walikuwa wazalendo? Kijana Mwigulu aliyefumaniwa na mke wa kada mwenzake alikuwa mzalendo? Najua kijana umekuja na moto wa kifuu,lakini ukweli haulazimishwi, watanzania hatufundishwi amani na watu walafi kama ninyi!
 
Loh!huyu Mbowe inaonekana ndani ya CCM anatajwa kwa hofu mara nyingi kuliko mtu yeyote,kila kukicha Mbowe Mbowe!na kwa taarifa yenu tunamuongeza term nyingine mtokwe povu zaidi.M4C Mbeleee!

Chama cha mapinduzi akijajengwa kwa kuhofia mtu au kundi lolote la watu, kwa kuwa ni chama chenye wanachama makini na imara, umoja wetu na hekima ndio nguzo ya uimara wa viungio vyetu vinavyotuunganisha kati ya mwanachama na mwanachama.

Ndio maana anapopatikana mgombea kupitia CCM katika nafasi ya uenyekiti mara zote huwa anaungwa mkono na kila mwanachama wa chama cha mapinduzi. Huko kwingine tunashuhudia fujo kila kukicha mara huyu anataka kuwa huyu, yani ni uroho uroho tu wa madaraka. Jambo ambalo CCM halina nafasi.
 
Hakuna kiongozi au mwanachama wa chama cha mapinduzi anaeendekeza mambo ya ufisadi, wizi na ubadhilifu wa mali ya umma.

Hayo yote chama changu imekuwa ikiyakemea vikali. Hivi ujiulizi kwa nini mkuu wa kaya anafanya mabadililo ya mara kwa mara ya baraza la mawaziri? anafanya maamuzi magumu kwa maslahi ya wengi ili kuonyesha chuki aliyonayo na mambo ya namna hiyo.

Hakuna kama Kikwete Tanzania.

Finishi yako hapo kwenye blue ndio yenyewe mkuu !!!
Hebu check hapa chini...

Kiukwete ndio rais wa kwanza Tanzania kuweka historia ya kutoa ahadi ya '..Maisha bora kwa kila Mtanzania...'.
Na kweli, ameahidi na ametekeleza kama inavyoonekana katika picha hii...
 
Ndugu yangu wa kanda ya ziwa, CHADEMA hawana hao unaowasema wanaweza kuforecast hata miaka miwili ijayo, maana wangeweza wasingefanya vitu kama M4C ambavyo vimeonyesha kuleta machafuko tu na chuki kati ya raia na serikali yetu.

Swala la elimu, naomba na wewe uingie bungeni na hoja yako binafsi itakayosema kuwa dkt au profesa haina tija kama hutaweza kugundua matatizo, ili katika nafasi mbali za kiutendaji watoe vigezo hivyo, waweke utakavyoona wewe vinafaa.

Ukipata elimu umepata mapata maarifa thats why serikali iliyoundwa na chama cha mapinduzi imelifanya swala la elimu kuwa kipaumbele cha taifa.

Sasa ili huyo DJ wenu m/kiti wa CHADEMA akubalike na jamii kubwa ya wananchi watanzania inabidi akashiriki mafunzo ya elimu ya watu wazima ili apate maarifa, itamsaidia katika kufanya maamuzi yenye tija, sio kama sasa alivyo mropokaji.
Lazima wewe unamatatizo makubwa sana ya kufikiri! Kama kweli serikali ya CCM ingeweka Elimu kuwa kipaumbele cha taifa basi watoto wasingejiunga na kidato cha kwanza bila kujua kusoma na kuandika! Elimu uliyopata wewe ingekuwezesha kuchambua mambo na matatizo ya nchi hii kisomi na sio kipumbavu kama unavyofanya wewe, walah elimu hiyo ingekusaidia kuandika hoja zako kwa lugha fasaha na maneno muafaka na sio makosa unayoyaweka hapa! Hakika kabisa kipaumbele cha taifa cha CCM ni rushwa na ufisadi, kisha kuwachinja bila huruma watu wanaodhaniwa wabaya wao!
 
Wenyewe walimu, waandishi na wanajeshi wakisikia unawafananisha na Disc Jockey sijui kama watafurahi!

Huko BOT bila shaka aliingizwa na Mtei kama alivyoingizwa ndani ya Chadema.

Sijui alionga kiasi gani kupata heshima na fursa ya kugombea urais 2005? wakati hakidhi vigezo stahiki.
 
Kuna harakati nyingi sana zinafanywa na hichi "chama cha wavaa magwandwa" katika operesheni tofauti tofauti kwa lengo la kutwaa dola.
.
.
Baada ya muda mfupi tukamsikia anataja jina la jembe letu, mkombozi wetu wa taifa, kipenzi cha walalahoi na adui wa mafisadi, his excellency the president of united republic of Tanzania dr. Jakaya.M.kikwete kwa upole, nidhamu na unyenyekevu wa hali ya juu.

Mnaweza mkapima wenyewe kuona mtu kama huyu anafaa kusimama kama rais wetu. Kwa niaba ya wengi nachukua nafasi hii kuwajibia. Jibu ni HAPANA.

Kwa hali hii ya vingozi wa chadema kutokuwa na sifa shindani na wale wa chama tawala nikimaanisha CCM, basi niitimishe kama ifuatavyo.
"CHAMA PINZANI NDILO JINA LA MILELE LA CHADEMA".

Angalia sana hapo kwenye blue,
Unaweza kupoteza 'kazi' aka ajira yako ya kuandika posts hapa JF kwa kumdharau bosi wako mkuu JK.
Angalia vizuri jina la JK la mwishi umelianza kwa herufi ndogo, dharau ya hali ya juu sana kwa jamaa...

Anyway,
Turudi kwenye mada,
Umeandika kuwa huyo jamaa ni adui wa mafisadi ?? au nimesoma vibaya ??
Unajua kuwa fisadi namba moja hapa TZ ni Ridhiwani ?? Maana, dogo kamaliza chuo juzi-juzi tu na sasa tayari ni bilionea mkubwa !! Sasa, unataka kusema JK na dogo ni maadui ?? Mhhh, lako hilo, umelikoroga...mimi simo...!!
 
Chama cha mapinduzi akijajengwa kwawkuhofia mtu au kundi lolote la watu, kwa kuwa ni chama chenye wanachama makini na imara, umoja wetu na hekima ndio nguzo ya uimara wa viungio vyetu kati ya mwanachama na mwanachama.

Ndio maana anapopatikana mgombea kupitia CCM katika nafasi ya uenyekiti mara zote huwa anaungwa mkono na kila mwanachama wa chama cha mapinduzi. Huko kwingine tunashuhudia fujo kila kukicha mara huyu anatakaka kuwa huyu, yani ni uroho uroho tu wa madaraka. Jambo ambalo CCM halina nafasi.
wala hujakosea kiongozi,tumeshuhudia demokrasia ya hali ya juu pale mke wa JK na mwanaye walivyopita bila kupingwa.Inaonyesha jinsi CCM mlivyoekwa mfukoni na BABA,MAMA NA WATOTO.
 
Tatizo la wana Jamiizforum wengi no CDM na wana matusi mno. Sasa hiyo CDM mnaionyesha vipi kama ni matusi mnatukana muda wote, afu mimi nililua active sana CDM ila mwishowe nimeona ni ujinga, siku hizi serikali nzima ni vilaza tu, kila wanallfanya ni kupata umaarufu wa chama, sio CCM sik CDM badala ya kushughulikia mambo ya nchi.. Mfano juzi Mwanza Waziri mkuu aliwasili na Mbunge Wenje Sahara mwz, mkutano ulikua wa wananchi wa Mwanza na si wa kichama, speech ya Wenje ilikua ni kupondea CCM tu na kujionyesha yupo juu, hakuna aliloongelea kuhusu Mwanza.. huu ni upuuzi mtupu, sasa kidogo fujp zitokee kama ilivyokawaida CDM ina washabiki wa aina nyingi hasa vijana wadogo na vibaka wengii tu.. CDM wakiendelea na huu ujinga amini usiamini 2015 hawapati kitu tena CCM itawatoa kwa asilimia kubwa, watu wameanza kufunguka macho na kuona hawa ni wachocheaji tu... Ushauri wafanye mambo ya kunufaisha wananchi na si kushabikia chama daily, hata chama chao kina uchafu kama vingine tu.. Mi nakubali sana sera zao, sema uchochezi wananipa wacwac.... Very narrow minded
 
Angalia sana hapo kwenye blue,
Unaweza kupoteza 'kazi' aka ajira yako ya kuandika posts hapa JF kwa kumdharau bosi wako mkuu JK.
Angalia vizuri jina la JK la mwishi umelianza kwa herufi ndogo, dharau ya hali ya juu sana kwa jamaa...

Anyway,
Turudi kwenye mada,
Umeandika kuwa huyo jamaa ni adui wa mafisadi ?? au nimesoma vibaya ??
Unajua kuwa fisadi namba moja hapa TZ ni Ridhiwani ?? Maana, dogo kamaliza chuo juzi-juzi tu na sasa tayari ni bilionea mkubwa !! Sasa, unataka kusema JK na dogo ni maadui ?? Mhhh, lako hilo, umelikoroga...mimi simo...!!

Tusiwe watu wenye chuki za waziwazi kwa watu wanaochipukia katika mafanikio, mnata kumsikia Ridhiwani ni mfagiaji wa barabara au mbangua korosho ndio mjue kama kijana sio fisadi?

Lini amefanya ubadhilifu wa mali ya umma? Muacheni chipukizi ajenge taifa kama wananchi wengine wanavyofanya kuliko kumsakama kwa hadithi hadithi za mtaani.
 
Kuna harakati nyingi sana zinafanywa na hichi "chama cha wavaa magwandwa" katika operesheni tofauti tofauti kwa lengo la kutwaa dola.
.
.
Ila tunaona wananunua helikopta mpya na magari ya hanasa, hapo wananchi tunajifanya kama hatuoni matumizi mabaya ya hawa watu. Safari zisizoisha za marekani na mataifa mengine yaliyoendelea ndio desturi na tamaduni ya wavaa magwanda. Haya yote mnayafumbia macho na kujifanya HAMUONI?


"CHAMA PINZANI NDILO JINA LA MILELE LA CHADEMA".

Hapo kwenye green (nimeweka green makusudi),
Naona unampiga 'dongo' JK aka Vasco Da Gama. Maana jamaa haishi 'kuzuka' majuu kila uchao...
Rais pekee katika historia ya Africa ambaye amefanya safari nyingi za nje ya nchi.
 
Tusiwe watu wenye chuki za waziwazi kwa watu wanaochipukia katika mafanikia, mnata kumsiki Ridhiwani ni mfagiaji wa barabara au mbangua korosho ndio mjue kama kijana sio fisadi?

Lini amefanya ubadhilifu wa mali ya umma? Muacheni chipukizi ajenge taifa kama wananchi wengine wanavyofanya kuliko kumsakama kwa hadithi hadithi za mtaani.

Hapo umepotea...
Dogo juzi tu kamaliza chuo, hajafanya kazi yoyote, wala hajafanya biashara yoyote, kawaje billionea ??
Ingekuwa rahisi hivyo kuwa billionea, kila mtu angekuwa billionea.
 
HAMY-D nakuomba Usiusemee Moyo Wa Mtu.Sema wewe kama HAMY -D kuwa hauiamini CHADEMA au viongozi wake.Yaangalie madhambi ya hao unao waona ni Watawala mpaka kiama je wanakidhi matakwa ya watanzania?Ni bora hao unaowaita Wafanya FUJO maana wamenifumbua mimamcho yangu mie ambaye sijaenda shule.
 
Baada ya muda mfupi tukamsikia anataja jina la jembe letu, mkombozi wetu wa taifa, kipenzi cha walalahoi na adui wa mafisadi, his excellency the president of united republic of Tanzania Dr. Jakaya.M.kikwete kwa upole, nidhamu na unyenyekevu wa hali ya juu.


Angalia sana hapo kwenye blue, Umeandika 'kipenzi cha walalahoi' au umekosea ? Sijui kama uko Dar es Salaam, ila ukiwa Dar es Salaam, jaribu kutembelea Kigamboni. Unaifahamu Kigamboni ?

Eneo la Kigamboni limeuzwa kwa 'wawekezaji'. Hii imesababisha wakazi wazawa walalahoi wa Kigamboni kuishi kwa hofu ya kutimuliwa na 'wawekezaji', na hatimaye kuwa wakimbizi kwenye nchi yao wenyewe.

JK ni rais wa kwanza katika historia ya TZ kwa kuuza kipande cha ardhi ya nchi kwa 'wawekezaji.
Upo hapo? Walalahoi wa Kigamboni mpo hapo? Mnampenda JK?

Umemuona mnunuzi wa Kigamboni ?
 
mkuu nazani huyu mletamada amepata ufunuzi wakutosha naaka wafunue wenzake hukowalipo bilakumsahau aliye mtuma
 
Mkuu JK hakurupuki kwenda tu nje ya nchi as he wish, zile ni ziara za kitaifa, wewe usiniambie unavyoona wawekezaji wanakuja kwa kasi na msululu mkubwa, kuja kuwekeza katika maeneo mbalimbali hapa nchini, it just happened to be that way, HAPANA.

Hayo ni matunda ya mkuu wa kaya, wawekezaji wamesaidia kufufua na kuongeza ufanisi katika mashirika yaliyokufa na kuanzisha mengine mapya. Tumeona kwa kiasi fulani imesaidia kuchochea uchumi na kuzalisha ajira mpya.

Tunaona walimu wa kujitolea kutoka mataifa yaliyoendelea kuja hapa nchini kufundisha vijana wetu, walimu hawa wapo tayari kukaa mazingira hayo hayo magumu ambayo walimu wetu wazawa wamekuwa wakiyabeza kwa kipi kirefu sasa. Yote hayo ni matunda ya ziara ya mkuu wa kaya.

Kuimarisha ushirikiano na urafiki wa nchi yetu na mataifa mengine ulimwenguni, ambayo hii inaleta faida nyingi kwa taifa haidha ya moja kwa moja au vinginevyo.
 
Akili zako kweli mgando kama CCM yako,mnaotumia makamasi kufikiri badala ya ubongo
 
Unanishawishi nifikirie kuwa unafaidika mno tena sana na UFISADI unaofanywa na viongozi wetu wa ngazi mbalimbali waliochini ya CHAMA CHENU KITUKUFU (CCM).Nakuomba kama ukijana angalia kwa mtazamo mpana,je Mjukuu wako atafaidika na kasi ya kuondosha raslimali zote za Taifa?Je watawakuta Twiga na dhahabu?Au ndio itakuwa historia?
 
HAMY-D, Salute,

Nimependa uchambuzi wako wa kina na wenye ujenzi kwa taifa letu ni uchambuzi murua.

Endelea kutoa elimu ya uraia.

Elimu ya uraia ??? We wacha utani wewe !!!
Serlkali yenyewe haitaki watu waelimike, halafu wewe unazungumzia kutoa elimu !!!!
Serilaki imefikia hatua ya kuhakikisha kuwa wahitimu wa darasa la saba hawajui kusoma na kuandika. !!
Kama hiyo haitoshi, wakahakikisha kuwa hao ambao hawajui kusoma na kuandika ndio wanapelekwa sekondari !!!
Halafu wewe unazungumzia kutoa elimu ????
Yaani wewe unapingana na serikali ya rais wako JK ??
JK ni rais wa kwanza wa TZ kuweka historia ya kupeleka sekondari wanafunzi ambao hawajui kusoma wala kuandika !!
JK kweli ni Jembe !!!
Oooops, hivi Ridhiwani anajua kusoma na kuandika ???
 
Mkuu naomba uelewe kuwa sina matatizo ya vyama pinzani, bali nina shaka na wasiwasi na siasa wanazofanya chadema, CUF kwa kipindi kirefu wamekuwa sehemu ya vyama vya siasa ambavyo vinafanya na kutekeleza siasa safi. Kwanini niwaongelee wao? au UDP? AU CCJ? SIO CHADEMA WANAOTUMIA JINA LA DEMOKRASIA KULETA MACHAFUKO YANAYOSABABISHA MAUAJI ALAFU MIMI NILIFUMBIE MACHO. JAMBO LINALOPASWA KUKEMEWA VIKALI NA NYINYI WENYEWE WAPENZI WA HICHO CHAMA CHENU OR ELSE NA NYINYI MNA-ENTERTAIN HAYO MAUAJI.
KWA HIYO MWANGOSI KAUAWA NA CHADEMA? Mwenyekiti wa CDM taifa ni IGP Mwema? Director NCHIMBI? Kwa hiyo kamuhanda ni mwenyekiti wa CDM mkoa wa Iringa?, na tena CDM wanavaa nguo za FFU na kubeba silaha ktk maghala ya polisi? Ngoja nikaangalie faili la mshitakiwa!!,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom