Chama pinzani ndilo jina la milele la chadema

Wenyewe walimu, waandishi na wanajeshi wakisikia unawafananisha na Disc Jockey sijui kama watafurahi!

Huko BOT bila shaka aliingizwa na Mtei kama alivyoingizwa ndani ya Chadema.
Mtei alitoka BOT lini a Freeman alifanya kazi huko lini? Mbowe kazaliwa mwaka 1961 so wataka kusema aliingia BOT akiwa na miaka mingapi? Na high school alimaliza lini? Wakati anaingia BOT Mtei bado alikua ni gavana? Ooh poor you!!
 
Mkuu JK akurupuki kwenda tu nje ya as he wish, zile ni ziara za kitaifa, wewe usiniambie unavyoona wawekezaji wanakuja kwa kasi na msululu mkubwa, kuja kuwekeza katika maeneo mbalimbali hapa nchi, it just happened to be that way, HAPANA.

Hayo ni matunda ya mkuu wa kaya, wawekezaji wamesaidia kufufua na kuongeza ufanisi katika mashirika yaliyokufa na kuanzisha mengine mapya. Tumeona kwa kiasi fulani imesaidia kuchochea uchumi na kuzalisha ajira mpya.

Tunaona walimu wa kujitolea kutoka mataifa yaliyoendelea kuja hapa nchini kufundisha vijana wetu, walimu hawa wapo tayari kukaa mazingira hayo hayo magumu ambayo walimu wetu wazawa wamekuwa wakiyabeza kwa kipi kirefu sasa. Yote hayo ni matunda ya ziara ya mkuu wa kaya.

Kuimarisha ushirikiano na urafiki wa nchi yetu na mataifaa mengine ulimwenguni, ambayo hii inaleta faida nyingi kwa taifa haidha ya moja kwa moja au vinginevyo.

Wawekezaji hawaji TZ kwa kuitwa na rais, wanakuja kwa sababu ya 'opportunity' ya kupata mikataba inayowakandamiza watanzania na kuwanufaisha saaana wao.
Rais hahitaji kwenda nje kuita wawekezaji, kwenye ofisi za kibalozi kuna maofisa wenye kazi hizo za kuhamasisha uwekezaki, utalii, n.k.
Leo hii wawekezaji wamejaa TZ kwenye madini lakini watanzania ni maskini kuliko walivyokuwa hapo kabla ya wawekezaji kuja, sababu ?? Mikataba mibovu ya CCM.
 
Hisia zenu ambazo zinakoshwa na huyu mvaa magwanda zitaliponza taifa. Wananchi hawana imani nae hilo unaliongeleaje?

Chadema kibaki kuwa pinzani ili kiisimamie serikali vizuri, maana na magwanda yao hiyo kazi ya ulinzi ulinzi wanaiweza.

Hapo kwenye blue nakubaliana na wewe kabisa.
Chadema wanaweza saana kulinda fedha, mali na raslimali za nchi hii zisiporwe na 'wawekezaji'.
Chadema wanaweza sana kulinda nchi isiingie kwenye mikataba mibovu ya madini, gas, mafuta, n.k.
Kwa maoni yangu, hao Chadema ndio wanafaa kuongoza nchi ili walinde vizuri utajiri na mali za watanzania !!
Hapo vipi ??
 
Labda si tanzania hii nayoiona sasa nachojua CCM wapo kwenye maandalizi ya nguvu kila kukicha kuwa WAPINZANI mwaka 2005.
 
kuna harakati nyingi sana zinafanywa na hichi "chama cha wavaa magwandwa" katika operesheni tofauti tofauti kwa lengo la kutwaa dola.

Ingawa viongozi wa chama hiki wamekuwa wabunifu wa kutumia njia mbalimbali kama mikutano ya hadhara, maandamano yasiyo na vibali, fujo na shari, kutoheshimu mamlaka zilizopo na mbaya zaidi kutokuwa na nidhamu na ustaharabu wa wabunge wa chama hiki katika bunge letu tukufu la jamhuri ya muungano wa tanzania kwa kuathiri mara kwa mara shughuli za bunge kufanyika kama ilivyopangwa na kufanya heshima na thamani ya bunge kumomonyoka mbele ya jamii ndani ya nchi na hata nje ya nchi.

Yote haya wanafanya kwa lengo la kujipatia umaarufu, taifa liwatambue kuwa wao ndio tumaini la ukombozi wa taifa, liwajengee imani kuwa wao ndio watabadili hali za watanzania wa chini kabisa na kuwapa unafuu wa maisha.

Uongo wa waziwazi wa wavaa magwanda ndio huu, kujifanya wanajali kundi la walalahoi huku wao ndio vinara wa kula bata mjini, wanachukua pesa za wavuja jasho kwa kigezo cha kuchangia chama wakati wanapata ruzuku kutoka serikalini ambayo hatujui pesa hizo za walipa kodi wanafanyia nini.

Ila tunaona wananunua helikopta mpya na magari ya hanasa, hapo wananchi tunajifanya kama hatuoni matumizi mabaya ya hawa watu. Safari zisizoisha za marekani na mataifa mengine yaliyoendelea ndio desturi na tamaduni ya wavaa magwanda. Haya yote mnayafumbia macho na kujifanya hamuoni?

Ila bado kuna kundi kubwa la watanzania wazalendo, wapenda amani, wapenda muungano na mshikamano, wameonyeshwa kuchukizwa na siasa za chadema na kuomba kifutiliwe mbali ili kiepushe michafuko inayoweza kutokea kutokana na siasa yao chafu, ya uchonganishi na ya kibabe.

Wananchi wengi wameonyesha kutokuwa na imani na hiki chama cha demokrasia na maendeleo kufuatia ukosefu wa maadili wa viongozi wake. Ninawachambua kama ifuatavyo (m/kiti na katibu wa chama)

1. Mwenyekiti wa chama ni mmiliki wa kumbi za starehe kama nightclubs, bars na guest houses. Pia alikuwa dj katika kumbi za starehe kadhaa hapa mjini.

Kuhusu elimu naomba nisiliongelee kwani ndio mwenyekiti wa chama cha siasa mwenye kiwango cha chini kabisa cha elimu hapa nchini.

Vilevile ni mfanyabiashara mkubwa wa kimataifa, kama ilivyo ada siku zote,hakuna mfanyabiashara asiyekuwa mnyonyaji. Sasa kazi kwetu watanzania kuendelea kumuwekea imani mtu kama huyu.

2. Katibu wa chama hiki amekumbwa na misukosuko mingi hivi karibuni, kuna thread humu muitafute inaeleza ufisadi ndani ya chadema ili muweze kumjua huyu mtu vizuri.

Kwa taarifa zilizonyooka kabisa ni kwamba ni mzoefu wa mechi za mchangani na mechi za kirafiki, halafu ikumbukwe alikuwa padre na tunafahamu wote, misimamo ya ma-padre wote ulimwenguni ni ipi, sasa mtu huyu anaonyesha wazi kutoweza kuvumilia na kutokuwa na msimamo thabiti wa anayoyaamini.

Hafai kupewa taifa kwani ni rahisi kwa mtu huyu kushawishika na kubadili mwelekeo mzima wa maamuzi yake, ambayo yataathiri taifa. Hapa nawakumbusha ile kauli yake ya kutomtambua mheshimiwa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania, yeye na magwanda mengine ya chadema.

Baada ya muda mfupi tukamsikia anataja jina la jembe letu, mkombozi wetu wa taifa, kipenzi cha walalahoi na adui wa mafisadi, his excellency the president of united republic of tanzania dr. Jakaya.m.kikwete kwa upole, nidhamu na unyenyekevu wa hali ya juu.

Mnaweza mkapima wenyewe kuona mtu kama huyu anafaa kusimama kama rais wetu. Kwa niaba ya wengi nachukua nafasi hii kuwajibia. Jibu ni hapana.

Kwa hali hii ya vingozi wa chadema kutokuwa na sifa shindani na wale wa chama tawala nikimaanisha ccm, basi niitimishe kama ifuatavyo.
"chama pinzani ndilo jina la milele la chadema".

naona chadema kina wasemaji wengi sana hapa nchini,kila mtu anaisemea chadema.why kila mahali ni chadema chadema tu,hamna issue nyingine za kuzungumzia wadau na watz kwa ujumla? Nadhani kuna mambo ya muhimi ya kuzungumzia kuliko kukaa na kujitafutia umaarufu kwa mgongo wa chadema.watz wanajua kutofautisha mchele na pumba haina haja ya kuwasemea,wao wenyewe ndo wataamua kama chadema kiwe chama cha upinzani milele au ccm ndo kiwe chama cha upinzani. Hizi ni kama kelele za chura ambazo haziwezi kumzuia tembo kunywa maji.
Ni hayo tu.
 
Nadhani kuna mambo ya muhimu ya kuzungumzia kuliko kukaa na kujitafutia umaarufu kwa mgongo wa chadema.watz wanajua kutofautisha mchele na pumba haina haja ya kuwasemea,wao wenyewe ndo wataamua kama chadema kiwe chama cha upinzani milele au ccm ndo kiwe chama cha upinzani. Hizi ni kama kelele za chura ambazo haziwezi kumzuia tembo kunywa maji.
Ni hayo tu.

Mkuu Mzalendo wa ukweli, i salute to this comment... kama ni sisi wenyewe tutaamua, wasilete ngebe na kelele nyingi.
 
Kila nikijaribu kumjibu mleta hoja nasita maana naona ban inanukia. Bora niwe mpole nisome michango ya wengine.
 
INGEKUWA HIVYO basi magamba wasingekosa usingizi wakijadili namna ya kuidhibiti CHADEMA.sasa hivi ni kama NCHI ina chama kimoja cha upinzani CHADEMA.
 
Mtei alitoka BOT lini a Freeman alifanya kazi huko lini? Mbowe kazaliwa mwaka 1961 so wataka kusema aliingia BOT akiwa na miaka mingapi? Na high school alimaliza lini? Wakati anaingia BOT Mtei bado alikua ni gavana? Ooh poor you!!

Kumbe hujui undugunization unavyofanya kazi hapa Tanzania.

Utabakia hivyo hivyo kupigwa mchanga wa macho tu!
 
"CHAMA PINZANI NDILO JINA LA MILELE LA CHADEMA".
Last edited by HAMY-D; Today at 04:21.

NILIPOONA MILELE NIKAMKUMBUKA NECHARDNEZAR, SADAM, GADAFI, IDD AMINI, BANDA, MUSEVENI, MUGABE NA WENGINE WA SAMPULI HIO. ANAYETAWALA MILELE NI YEHOVA. WENGINE WOTE WATAPITA IKIWA NA PAMOJA NA CCM HAPO 2015
 
Kumbe hujui undugunization unavyofanya kazi hapa Tanzania.

Utabakia hivyo hivyo kupigwa mchanga wa macho tu!
Mwaka 1979 Mbowe alikua form 3 na he was 18! Na mwaka huo ndo Mtei alitoka BOT. Sasa wewe sema ni mwaka gani Freeman alikua BOT na uelezee involvement ya Mtei! Weka huo undugunaization hapa ili twende sambamba na cio kubweka nibaki hivyohivyo! We ndo ubakie hivyo as if you are in a solitary confinement!
 
Huyu gamba hana jipya.Hawa CCM wanaogopa sana kuachia ngazi kutokana na maovu mengi waliyofanya,wanatikiwa kutambua kuwa kila chenye mwanzo hakikosi mwisho.May god bless Tanzania.
 
Kuna harakati nyingi sana zinafanywa na hichi "chama cha wavaa magwandwa" katika operesheni tofauti tofauti kwa lengo la kutwaa dola.

Ingawa viongozi wa chama hiki wamekuwa wabunifu wa kutumia njia mbalimbali kama mikutano ya hadhara, maandamano yasiyo na vibali, fujo na shari, kutoheshimu mamlaka zilizopo na mbaya zaidi kutokuwa na nidhamu na ustaharabu wa wabunge wa chama hiki katika bunge letu tukufu la jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuathiri mara kwa mara shughuli za bunge kufanyika kama ilivyopangwa na kufanya heshima na thamani ya bunge kumomonyoka mbele ya jamii ndani ya nchi na hata nje ya nchi.

Yote haya wanafanya kwa lengo la kujipatia umaarufu, taifa liwatambue kuwa wao ndio tumaini la ukombozi wa taifa, liwajengee imani kuwa wao ndio watabadili hali za watanzania wa chini kabisa na kuwapa unafuu wa maisha.

Uongo wa waziwazi wa wavaa magwanda ndio huu, kujifanya wanajali kundi la walalahoi huku wao ndio vinara wa kula bata mjini, wanachukua pesa za wavuja jasho kwa kigezo cha kuchangia chama wakati wanapata ruzuku kutoka serikalini ambayo hatujui pesa hizo za walipa kodi wanafanyia nini.

Ila tunaona wananunua helikopta mpya na magari ya hanasa, hapo wananchi tunajifanya kama hatuoni matumizi mabaya ya hawa watu. Safari zisizoisha za marekani na mataifa mengine yaliyoendelea ndio desturi na tamaduni ya wavaa magwanda. Haya yote mnayafumbia macho na kujifanya HAMUONI?

Ila bado kuna kundi kubwa la watanzania wazalendo, wapenda amani, wapenda muungano na mshikamano, wameonyeshwa kuchukizwa na siasa za CHADEMA na kuomba kifutiliwe mbali ili kiepushe michafuko inayoweza kutokea kutokana na siasa yao chafu, ya uchonganishi na ya kibabe.

Wananchi wengi wameonyesha kutokuwa na imani na hiki chama cha demokrasia na maendeleo kufuatia ukosefu wa maadili wa viongozi wake. Ninawachambua kama ifuatavyo (m/kiti na katibu wa chama)

1. Mwenyekiti wa chama ni mmiliki wa kumbi za starehe kama nightclubs, bars na guest houses. Pia alikuwa DJ katika kumbi za starehe kadhaa hapa mjini.

Kuhusu elimu naomba nisiliongelee kwani ndio mwenyekiti wa chama cha siasa mwenye kiwango cha chini kabisa cha elimu hapa nchini.

Vilevile ni mfanyabiashara mkubwa wa kimataifa, kama ilivyo ada siku zote,hakuna mfanyabiashara asiyekuwa mnyonyaji. Sasa kazi kwetu watanzania kuendelea kumuwekea imani mtu kama huyu.

2. Katibu wa chama hiki amekumbwa na misukosuko mingi hivi karibuni, kuna thread humu muitafute inaeleza ufisadi ndani ya chadema ili muweze kumjua huyu mtu vizuri.

Kwa taarifa zilizonyooka kabisa ni kwamba ni mzoefu wa mechi za mchangani na mechi za kirafiki, halafu ikumbukwe alikuwa padre na tunafahamu wote, misimamo ya ma-padre wote ulimwenguni ni ipi, sasa mtu huyu anaonyesha wazi kutoweza kuvumilia na kutokuwa na msimamo thabiti wa anayoyaamini.

Hafai kupewa taifa kwani ni rahisi kwa mtu huyu kushawishika na kubadili mwelekeo mzima wa maamuzi yake, ambayo yataathiri taifa. Hapa nawakumbusha ile kauli yake ya kutomtambua mheshimiwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, yeye na magwanda mengine ya chadema.

Baada ya muda mfupi tukamsikia anataja jina la jembe letu, mkombozi wetu wa taifa, kipenzi cha walalahoi na adui wa mafisadi, his excellency the president of united republic of Tanzania dr. Jakaya.M.kikwete kwa upole, nidhamu na unyenyekevu wa hali ya juu.

Mnaweza mkapima wenyewe kuona mtu kama huyu anafaa kusimama kama rais wetu. Kwa niaba ya wengi nachukua nafasi hii kuwajibia. Jibu ni HAPANA.

Kwa hali hii ya vingozi wa chadema kutokuwa na sifa shindani na wale wa chama tawala nikimaanisha CCM, basi niitimishe kama ifuatavyo.
"CHAMA PINZANI NDILO JINA LA MILELE LA CHADEMA".

Wewe mtoa mada inatakiwa pia utuambie kwanini CCM watatawala muda mrefu, unawasifu kwa lipi?
 
Mwaka 1979 Mbowe alikua form 3 na he was 18! Na mwaka huo ndo Mtei alitoka BOT. Sasa wewe sema ni mwaka gani Freeman alikua BOT na uelezee involvement ya Mtei! Weka huo undugunaization hapa ili twende sambamba na cio kubweka nibaki hivyohivyo! We ndo ubakie hivyo as if you are in a solitary confinement!

Nenda ukaulize kwanza inakuwaje Dr Mwinyi ni waziri wa Afya na mwaka gani mwinyi alitoka kwenye urais.
 
Hisia zenu ambazo zinakoshwa na huyu mvaa magwanda zitaliponza taifa. Wananchi hawana imani nae hilo unaliongeleaje?

Chadema kibaki kuwa pinzani ili kiisimamie serikali vizuri, maana na magwanda yao hiyo kazi ya ulinzi ulinzi wanaiweza.

mbona we pamoja na kuuza utu wako unabaki tegemeo la kuuza sera za chama cha majambazi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom