Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,763
- 40,989
Chama kipya cha kisiasa cha AFTP kimepata usajili wa muda leo mbele ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa. Chama hicho ambacho lengo lake ni kuwavutia wakulima kinajulikana kama Alliance Farmers Party ambacho sasa hivi Mwenyekiti wake wa Muda ni Said Sudi Said. Bw. Said akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupata usajili huo wa muda alisema kuwa "tunawaendea wakulima kwa sababu wamesahauliwa na vyama vingi vilivyopo". Kwa mujibu wa sheria za vyama vya kisiasa, chama hicho kipya kinatakiwa kizunguke ndani ya angalau mikoa kumi na kupata wanachama angalau 200 ili kiweze kupata usajili wa kudumu.