Makala Jr
JF-Expert Member
- Aug 25, 2011
- 3,395
- 1,112
Habari zenu wana JF, Awali ya yote napenda kuanza na wahenga waliosema riziki ni mafungu 7, walipoona bado ndani ya jamii kuna waroho wa madaraka na mali ambao wakipewa kiti wakae wanadai watakaa milele, hapo wahenga walisema "mwisho wa ubaya ni aibu na mchimba kisima huingia mwenyewe" . Leo asubuhi nimesikiliza kipindi cha 'WATANZANIA TUZUNGUMZE MAGAZETI-RFA' ndipo niliposikia eti gazeti la Mtanzania na Habari leo wameandika CCM wameibua kashfa nzito CHADEMA, kuhusu kuua baadhi ya polisi na wananchi. Nikakumbuka msemo wa wahenga, "Zimwi likujualo halikuli likakwisha", nikajiuliza ni lini CCM hawajakashifu upinzani? Licha ya kukumbuka "Moyo wa mtu ni msitu" nikajiuliza, CHADEMA waue polisi na raia kwa lengo gani? Baadaye nikakumbuka "Ya kale ni dhahabu" nikajiuliza mtu kama Mwangosi aliwakosea nini polisi? Ndipo nikagundua ni propaganda, CCM jiulizeni CHADEMA wameruka vingapi?