SONGOKA
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 1,841
- 1,843
Katibu mkuu mashinji kapwaya kila kona, Mwenyekiti sasa kaanza kujutia uamuzi wake na kupuuza ushauri aliopewa na makamanda wakuu.
Toka achaguliwe hajaonyesha ubunifu wowote, sikuizi mbowe ndo anatoa matamko ya kitendaji ya chama. Hata shughuli za kawaida za kikamanda anazikacha. Juzi wakati wenzake wakipambana kuhusu haki ya mikutano ya hadhara Mwanza, yeye alikuwa anakula pilau katika uaskofusho wa class mate wake pale geita. Nasisitiza chama hakikumtuma huko
Hapa Ufipa tulishangaa sana na tutalijadili hili. Lakini hata makamanda maarufu wamezidi kumpuuza hasa baada ya kushindwa kuandaa program makini za kuendelea kukiweka chama juu.
Kimsingi hajui atoke vipi, ila makamanda wamepanga kumtumbua mkutano mkuu ujao, hili linaendelea kwa sili kubwa na umakini wa hali ya juu
Lowasa ndo hamtaki kabisaa, yani ni hatari kwelikweli. MAKAMANDA tujipange kwa kweli
update ;courtesy of 1000 digits
Toka achaguliwe hajaonyesha ubunifu wowote, sikuizi mbowe ndo anatoa matamko ya kitendaji ya chama. Hata shughuli za kawaida za kikamanda anazikacha. Juzi wakati wenzake wakipambana kuhusu haki ya mikutano ya hadhara Mwanza, yeye alikuwa anakula pilau katika uaskofusho wa class mate wake pale geita. Nasisitiza chama hakikumtuma huko
Hapa Ufipa tulishangaa sana na tutalijadili hili. Lakini hata makamanda maarufu wamezidi kumpuuza hasa baada ya kushindwa kuandaa program makini za kuendelea kukiweka chama juu.
Kimsingi hajui atoke vipi, ila makamanda wamepanga kumtumbua mkutano mkuu ujao, hili linaendelea kwa sili kubwa na umakini wa hali ya juu
Lowasa ndo hamtaki kabisaa, yani ni hatari kwelikweli. MAKAMANDA tujipange kwa kweli
update ;courtesy of 1000 digits
Mleta mada amefanya jambo zuri sana kueleza anayoyaona na anayoamini kwamba yakiachwa yatakidhoofisha chama.
Hakuna mtu anatependa kuona chama kikubwa kama CHADEMA au CUF kinakufa.
Hivi vyama vimejijenga kwa gharama kubwa sana ya kupoteza maisha ya wananchi ambao pengine hawakuwa hata wanachama zaidi ya wapenda demokrasia na mashabiki tu. Kwa hiyo viongozi wasidhani tena hivi vyama ni mali yao binafsi kama walivyokua wanavianzisha. Kazi yao ya kuanzisha vyama iliisha na ilikua nzuri pale walipoingia mitaani na kuvitangaza kuwa ni vyama vya kisiasa. Siasa ni ushawishi wa kujenga hoja. Kubishana na mwenye hoja ndiye anakubaliwa na kuungwa mkono na wananchi.
Sasa huyo Mashinji tangu ameingia madarakani kama katibu mkuu mpaka sasa nadhani hajulikani hata mkoani kwake au kijijini kwake kuwa ni katibu mkuu wa CHADEMA chama kikuu cha upinzani. Hakuweza hata kufanya ziara za kustukiza za kukagua matawi kijijini kwake achilia mbali wilayani kwake. Hili la mchana nalo kweli linahitaji kumulikwa kwa karabai .!!!
Mr Mashinji hata akipita Kariakoo hakuna hata mtu mmoja anayeweza kuacha shughuli yake akijua kuna Katibu Mkuu wa Chama kilichoponea chupuchupu kuingia madarakani miezi nane tu iliyopita. Huyu mnasena ni kiongozi kweli au ni kuishiwa pumzi kwa Mbowe au ni mikakati hafifu ya kukijenga chama.
Tulishauri tangu Mapema ,Mbowe awe msikivu na asikilize Wanayosema wakosoaji. Wapenda demokrasia wanampigia kelele Magufu na bunge lake kuwa hawasikilizi kelele zao lakini Mbowe naye anaiga mkondo huo huo anaoupinga akiwa majukwaani.
Tulishauri hizi kelele za UKANDA na UDINI zifanyiwe kazi.
Hata kwa akili ya Kawaida tu bila kuwa mwanasiasa chaguo la Mbowe halikuwa na Tija.Uchaguzi wa Mbowe ulitokana na kuyumba kisiasa baada ya uchaguzi.
Mashinji kwa hali ya kawaida kutokana na Ujio wa Magufuli hawezi kuwa Mpambanaji bora kuipinga serikali yake.
Hulka ya Mwafrika bado ina neno zimwi likujualo halikuli likakwisha. Na hii ndiyo siasa wanayocheza nayo CCM kwa miaka mingi.
Jambo ambalo hata CUF itachemka endapo itamrudisha Lipumba, itakua ni mnyukano wa kisiasa kwa vyama vya upinzani vyenyewe kwa vyenyewe mana sababu zilizomfanya amuunge mkono Magufuli bado zipo.
Mbowe alipaswa kuzingatia tuhuma za udini na ukanda kwa kumchagua Juma Mwalimu kuwa Katibu Mkuu.
Au hata Msigwa angefaa zaidi kwa kupunguza tuhuma za ukanda.
Potelea Mbali ni bora angempa Tundulisu au Hache.
Hawa ni watu Jasiri kwenye siasa ngumu za kiafrika za kung"ang"ania madaraka.
Hawa wanajulikana na wanauzika bila matangazo ya ziada kama ilivyo kwa Mashinji.
Hakuna vijana wa sekondari wanaomfahamu Mashinji ni nani na kwa bahati mbaya anasubiri Jeshi la Polisi limpe ratiba ya shughuli zake za kisiasa.
Juzi wanachama wa CCM waliandamana kisayansi kwa kutumia magari na wakakutwa wameshafikisha ujumbe wao kabla ya jeshi la polisi kuwashtukia. Siasa ni mbinu tu alimradi zisiwe mbinu za kupanga mauaji au kupindua serikali.
Mbinu za kisiasa kama hazipingani na sheria za kijinai na katiba ya nchi basi hazina madhara hata polisi wakiwakamata na kufungulia kesi mara nyingi wanaachiwa na mahakama.
Katibu mkuu bwana Mashinji hajui kuwa polisi wanajihami tu lakini wanaelewa sana kuwa wanachokifanya sio sahihi ila hawajamuona mtu wa kusimama na kujenga hoja ya kuweza kuwaumiza kichwa na serikali yao.
Kazi ya polisi ni kulinda watu wote wafanye shughuli zao kwa amani bila kubughudhiwa au mali zao kuharibiwa au kuibiwa.
Hapa ni kwamba hata shughuli za Katibu mkuu zinapaswa kufanywa kwa amani zikilindwa na jeshi la polisi. Katibu mkuu afanye shughuli zake za kujenga chama sio lazima aandamane na msururu wa wabunge wenye tuhuma za kufanya fujo bungeni.
Hii ndio inayotishia intelijensia ya polisi na kufanya wazuie mikutano yao. Kwa hali ya sasa ya woga wa Serikali ya Viwanda jeshi la polisi haliwezi kukubali kuona misururu ya magari ya wabunge wanavamia jimbo moja na kuanza kupiga siasa za kuanika hadharani uovu wa serikali. Walizuia bunge lisionyeshwe sasa wataruhusuje mikutano ionyeshwe kwa hoja ile ile waliyokuwa wanaificha?
Hapa ni kujiongeza tu na kuweka mikakati ya kisayansi zaidi!
Katibu wa Chama cha kisiasa ameajiriwa kwa ajili ya kufanya shughuli za kisiasa
hivyo ana haki ya kuliomba jeshi la polisi lihakikishe kuwa linamlinda ili afanye kazi zake za kisiasa kwa amani . Sawa na watukishi wengine wanoomba msaada wa polisi wakati wa kufanya oparation.
Ndio maana vikundi vya kidini vinaendesha shughuli zake za kukusanyika kwa na kutangaza imani zao pamoja na kwamba kila dini ina mtizamo wake. Kazi ya polisi sio kuwaamuru watu wa dini kuwa na imani mojo ; kazi ya polisi ni kusimamia amani ili kila mhuburi ahubirie waumini wake kwa imani yake na misimamo yake.
Tulikua tukimuona Dr. Slaa akienda mpaka Nchi za nje kujifunza mbinu za kuendesha chama na pia kuueleza ulimwengu changamoto wanazokutana nazo toka kwenye serikali na hujuma za kudumaza demokrasia.