Chama Cha Waalimu Tanzania (CWT): Hatutaichagua CCM

Chama Cha Waalimu Tanzania (CWT): Hatutaichagua CCM

Huyu jamaa Wa ajabu kweli,hivi kwani walimu wrote wamesoma arts na hakuna walimu Wa sayansi? halafu hiyo sayansi anayoisema ni IPI ambayo haijaweza kutengeneza sindano,kiberiti na kutumia mwarobaini kupata tiba ya malaria?

Huyu hajitambui achana naye,
 
Kama wewe ni kijana alafu ni mccm uzeeni lazima uwe mchawi

Hahaha..kweli mkuu,ndio maana jana usiku walikesha pale Jangwani wakizindika na kufanya mambo yao ya kishirikina.
 
Habarini wadau,

Tokea Alhamisi asubuhi mpaka jana jioni kulikuwa na meeting katika ofisi mpya ya CWT iliyojengwa kwa mfuko wa waalimu kuanzia june 2013, Kwakweli ingawa halikuwa katika agenda,ila Ghafla

Asilimia 80% ya waalimu walisema kuwa CCM imekuwa ikiwadanganya waalimu kama watoto wadogo,yaani wakitoa ahadi ambazo hawazitekelezi kwa miaka yote.

Aliyekuwa katibu wa CWT Mkoa naye alisema tatizo la kutopandishiwa mishahara au kupandishiwa kwa asilimia ndogo sana,Waalimu kutopandishwa madaraja na Malimbikizo ya mshahara ndilo limewafanya waalimu wasiwe na imani na serikali ya CCM tena.

Naye Mwalimu mkuu kwa muda wa miaka 15 kazini alisema kuwa: Hatuwezi kuwapigia kura viongozi wa serikali wanaotudharau na kudharau fani yetu ya ualimu,aliendelea kusema kuwa Waalimu wa taifa hili wamekuwa wakipuuzwa na hata kutukanwa tofauti na wafanyakazi wa taasisi zingine,na wamekuwa wakionekana bora tu wakati kipindi cha kampeni na sensa ya watu na makazi.

Mwishoni kwa kumalizia,Katibu wa CWT kwa waalimu wa shule za msingi yeye alisema tu wanachotaka ni Mabadiliko,ije serikali nyingine labda itawajali waalimu kwa kazi zao ngumu na zisizo na overtime wala marupurupu.
hiki kikao ni cha cwt ngazi gani taifa, mkoa(gani), wilaya(gani), au tawi(gani)? sababu sijaelew naomba ufafanuzi.
 
Komaa nao kabisaa, hawana lolote, sasa hivi wanaona walimu wanataka mabadiliko ndo wanataka kuitumia UKAWA kama kivuli cha kujifichia.

Walimu tunawajua wabaya wetu wote, tuna akili timamu tunajua zuri na baya....Tukutane oktoba 25



barua yangu nliipitisha kwa mkuu wa shule hadi leo ananiuliza nliwaza nin kuiandika na ni ubahili ulopitiliza, nkamcharukia huyo nkamwambia kwakuwa yeye sio mbahili anipe 10,000/ kwa mwezi bila kuhoji!! hana mbavu
 
Kukariri misemo ya kijinga na ya kizamani kwa karne hii ni kujivua nguo na kuonesha usivyo na uwezo wa kupambanua mambo kulingana na mazingira na wakati!!

Huyo mtu hajielewi anaandika tu pumba
 
Habarini wadau,

Tokea Alhamisi asubuhi mpaka jana jioni kulikuwa na meeting katika ofisi mpya ya CWT iliyojengwa kwa mfuko wa waalimu kuanzia june 2013, Kwakweli ingawa halikuwa katika agenda,ila Ghafla waalimu kwa pamoja walilizungumzia na walikubaliana kutomchagua Mgombea yeyote wa CCM.

Asilimia 80% ya waalimu walisema kuwa CCM imekuwa ikiwadanganya waalimu kama watoto wadogo,yaani wakitoa ahadi ambazo hawazitekelezi kwa miaka yote.

Aliyekuwa katibu wa CWT Mkoa naye alisema tatizo la kutopandishiwa mishahara au kupandishiwa kwa asilimia ndogo sana,Waalimu kutopandishwa madaraja na Malimbikizo ya mshahara ndilo limewafanya waalimu wasiwe na imani na serikali ya CCM tena.

Naye Mwalimu mkuu kwa muda wa miaka 15 kazini alisema kuwa: Hatuwezi kuwapigia kura viongozi wa serikali wanaotudharau na kudharau fani yetu ya ualimu,aliendelea kusema kuwa Waalimu wa taifa hili wamekuwa wakipuuzwa na hata kutukanwa tofauti na wafanyakazi wa taasisi zingine,na wamekuwa wakionekana bora tu wakati kipindi cha kampeni na sensa ya watu na makazi.

Mwishoni kwa kumalizia,Katibu wa CWT kwa waalimu wa shule za msingi yeye alisema tu wanachotaka ni Mabadiliko,ije serikali nyingine labda itawajali waalimu kwa kazi zao ngumu na zisizo na overtime wala marupurupu.
hicho kikao cha cwt ni cha ngazi gani? taifa, mkoa, wilaya au tawi? kimefanyika wapi?
 
Tunataka Usawa Katika Mishahara,waalim Tulipwe Sawa Na Madaktari, Nasisi Ni Madaktari Na Kila Siku Tunakarabati Vichwa Vya Watoto Wenu ("Wapumbavu" kwa Mujibu Wa Rais Mkapa,) KUFULI TUTALIVUNJA NA POMBE TUTAIMWAGA.

Mkuu Mwaka huu ndio CCM itawatambua waalimu wa Tanzania hii,usiache kwenda kupiga kura.
 
hicho kikao cha cwt ni cha ngazi gani? taifa, mkoa, wilaya au tawi? kimefanyika wapi?

Kama wewe ni mwalimu wa aidha sekondari au Msingi ungejua utaratibu wote wa vikao vya CWT,kama sio mwl. basi elewa na ondoka na mada husika, waulize viongozi wote wa CWT mikoa.
 
Kama wewe ni mwalimu wa aidha sekondari au Msingi ungejua utaratibu wote wa vikao vya CWT,kama sio mwl. basi elewa na ondoka na mada husika, waulize viongozi wote wa CWT mikoa.
nimeuliza sababu habar yako haijataja hayo. hicho kikao kimefanyika wapi?unataja vyeo husemi aliyekua katibu wa cwt mkoa wa wapi? kwanza sijawahi kusikia cheo cha katibu wa cwt kwa shule za msingi. halafu huyo katibu ni wa wapi? nimeuliza tu km huna jibu sema huna jibu au hujui
 
Walimu ni kama watumishi wengine ndani ya nchi hii hawana special needs kama mataahira kinachofanyika kwao ni kilekile kinachofanyika kwa watumishi wengine wasijone wao ndiyo wateule, hivi mwalimu anaweza kufundisha akiwa mgonjwa hivi mwalimu anaweza kuingia darasani wakati mabomu yanapigwa nyuma ya nyumba yake? au mwanaye kapigwa risasi, Serikali nyingine wanayoitaka niya Dr Magufuli itawafaa sana ni kweli shemeji yao kwaachia jembe.
umeongea vizuri mkuu walimu ni km wafanyakaz wengine kwa nn wahtaj special treatment? kwanza hakuna mwl wa degree analipwa chini ya laki sita baada ya makato labda km amejilipua. naona hata walimu hawajiamini kabisa ndo maana wanaona wanadharaulika.
 
nimeuliza sababu habar yako haijataja hayo. hicho kikao kimefanyika wapi?unataja vyeo husemi aliyekua katibu wa cwt mkoa wa wapi? kwanza sijawahi kusikia cheo cha katibu wa cwt kwa shule za msingi. halafu huyo katibu ni wa wapi? nimeuliza tu km huna jibu sema huna jibu au hujui

Mkuu usiseme kitu ambacho hukifahamu labda,hebu ulizia shule zote za msingi na sekondary kilimanjaro,Dsm,Arusha na mikoa mingine baadhi kama haina makatibu wa pande zote,kwani lazima niandike kila kitu?
 
umeongea vizuri mkuu walimu ni km wafanyakaz wengine kwa nn wahtaj special treatment? kwanza hakuna mwl wa degree analipwa chini ya laki sita baada ya makato labda km amejilipua. naona hata walimu hawajiamini kabisa ndo maana wanaona wanadharaulika.

Na hapa umeandika uongo,hebu chukua salary slip ya mwl yeyote wa bachelor aliyeajiriwa recently kisha angalia take home salary ni shilingi ngapi,jitahidi kuandika vitu vyenye ushahidi na uhakika.

Kuhusu waalimu kuwa treated the same na fields zingine,nimeshalielezea na kuna utofauti mkubwa.
 
Mkuu usiseme kitu ambacho hukifahamu labda,hebu ulizia shule zote za msingi na sekondary kilimanjaro,Dsm,Arusha na mikoa mingine baadhi kama haina makatibu wa pande zote,kwani lazima niandike kila kitu?
unajua unapoleta habari jitahidi iwe imekamilika ili usiulizwe maswali. nimeuliza tu kutaka kufahamu wala hatubishani ni wapi hicho kikao kimefanyika? umesema katika ofisi mpya ya walimu iliyoko wapi? tanzania nzima ina ofisi mpya sema ni wapi huko? naomba weka pich ya hiyo salary slip ya huyo mwl aliyelipwa chini ya laki sita baada ya makato ktk mshahara wa mwez wa saba.
 
Walimu wa Tanzania wana taraja zuri Sana wote ni mafirst ladies Na mashemeji wa marais wa Tanzania, wamefaidishwa Na maisha bora ya uwama. Ccm juu!
 
Nashindwa hata cha kuandika nilivyo na hasira na CCM.
 
Back
Top Bottom