Chama Cha Upinzani BJP chashinda Uchaguzi India

NGARUKA

JF-Expert Member
May 5, 2014
401
70
jamani niko live naangalia live Mgombea kupitia chama cha upinzani BJP,Mr. modi anawasili makao makuu ya chama kuongea na waandishi.
BJP wamekishinda chama tawala Congress kupitia mgombea wao Mr. Modi ndani ya miaka 67.
Chadema wakiacha danganya toto wanaweza fanya haya la sivyo?
Wasubiri kesho kwenye gazeti la Tanzania Danganya watakavyopamba "UPINZANI "WAINGIA IKULU" tofauti na ushindi wa ANC kule A.kusini hatukusikia kitu.
WANANCHI SI KUDANGANYA bali wa kuambiwa ukweli. Usiwalazimishe wakuonee huruma kwa matakwa yako"
WAPINZANI NA CCM JIFUNZENI
=================================================

BJP yashinda uchaguzi wa India
Narendra Modi anaelekea kushinda uchaguzi wa India na kupata idhini ya kuanzisha ajenda yake ya kuufufua ukuwaji wa uchumi na kuunda nafasi mpya za ajira kwenye taifa hilo la pili kwa idadi ya watu duniani.

Waziri Mkuu mteule wa India, Narendra Modi, akibarikiwa na mama yake baada ya kushinda uchaguzi wa India.
0,,17640425_303,00.jpg

Waziri Mkuu mteule wa India, Narendra Modi, akibarikiwa na mama yake baada ya kushinda uchaguzi wa India.

Waziri Mkuu Manmohan Singh amempigia simu Modi kumpongeza kwa ushindi wa chama chake cha Bharatiya Janata (BJP). Hiyo ni baada ya matokeo ya awali kuonesha kuwa chama hicho na washirika wake tayari wameshajizolea zaidi ya idadi ya viti 272 vinavyohitajika kuwa na wingi wa kutosha kwenye bunge la nchi hiyo lenye viti 543.
Kwa mujibu wa takwimu za Tume ya Uchaguzi, Modi anaongoza kwenye majimbo yote mawili aliyogombea, Vadodara lililo Gujarat na mji mtakatifu wa Wahindu wa Vanarasi.

Ravi Shankar Prasad, kiongozi BJP katika mji mkuu New Delhi, ameuelezea ushindi wa chama chake kama ujumbe wa kuvunjika moyo wa wapiga kura.
"Watu wamechoshwa na uongozi mbaya ambao umeifanya India kuwa masikini, yenye huzuni na nchi ya mateso. Na nauheshimu uwelewa wa watu wa India hii yenye maumivu kwa namna walivyopiga kura. Sasa matokeo yanaonesha kuwa serikali makini itakayofanya kazi, itaundwa chini ya uongozi wa Narendra Modi." Amesema Prasad.

Congress yaangukia pua
Mfuasi wa Narendra Modi akishangilia ushindi wa kiongozi wake mjini New Delhi.
0,,17640330_404,00.jpg

Mfuasi wa Narendra Modi akishangilia ushindi wa kiongozi wake mjini New Delhi.

Hadi sasa ni majimbo 50 yaliyothibitika kuongozwa na Congress, lakini baadhi ya viongozi wa chama tawala cha Congress, bado wana matumaini kuwa chama chao kitaendelea angalau kushikilia baadhi ya viti vyake, hata kama si kuendelea kutawala.
"Huu ni muelekeo tu wa matokeo na sio matokeo kamili. Kuna tafauti kati ya masaa machache na nambari na matokeo halisi. Hivyo, tafadhali subiri. Si lazima muelekeo wa matokeo uwe ndio matokeo hasa." Amesema Shobha Oja, kiongozi wa Congress.

Hata kiongozi wa kampeni za chama hicho, Rahul Gandhi, anaongoza kwa ushindi mdogo sana kwenye ngome ya familia yake, jimbo lake la Amethi, ambalo limewahi kushikiliwa na ami, baba yake Rajiv na mama yake, Sonia, kwa vipindi tafauti. Kulipoteza jimbo hili kutakuwa hasara kubwa kwa kirembwe hicho cha kiongozi wa uhuru wa India.

Waziri Mkuu mpya Narendra Modi

0,,17558597_404,00.jpg

Rahul Gandhi wakati wa kampeni za uchaguzi.

Ikiwa muelekeo wa matokeo haya ya awali utakwenda kama ulivyo, basi BJP watakuwa na wingi wa kutosha kwa kuwa na zaidi ya viti 272 katika Lok Sabha, au Baraza la Wawakilishi.

Matokeo haya yatamfungulia njia Modi, mwenye umri wa miaka 63, kuwa waziri mkuu na kuwatangaza wanasiasa wanaomtii kwenye nafasi muhimu katika baraza la mawaziri: fedha, mambo ya ndani, ulinzi na mambo ya nje.
Lakini ikiwa Modi atashindwa kupata wingi wa kutosha, atalazimika kuingia kwenye mazungumzo marefu ya kuunda serikali ya mseto na vyama vya majimbo, jambo ambalo litautia rehani utiifu wa kisiasa na yumkini kuilainisha ajenda yake ya mageuzi, aliyoiuza kwa wapiga kura wakati wa kampeni.

Chanzo:Deutsche Welle
 
jamaa anakubaluka muno huku kwa sera zake kashinda ushindi mnono hasa
 
jamani niko live naangalia live Mgombea kupitia chama cha upinzani BJP,Mr. modi anawasili makao makuu ya chama kuongea na waandishi.
BJP wamekishinda chama tawala Congress kupitia mgombea wao Mr. Modi ndani ya miaka 67.
Chadema wakiacha danganya toto wanaweza fanya haya la sivyo?
Wasubiri kesho kwenye gazeti la Tanzania Danganya watakavyopamba "UPINZANI "WAINGIA IKULU" tofauti na ushindi wa ANC kule A.kusini hatukusikia kitu.
WANANCHI SI KUDANGANYA bali wa kuambiwa ukweli. Usiwalazimishe wakuonee huruma kwa matakwa yako"
WAPINZANI NA CCM JIFUNZENI
Nitawashangaa sana Tanganyika Daima kushadadia mambo ya India
 
jamani niko live naangalia live Mgombea kupitia chama cha upinzani BJP,Mr. modi anawasili makao makuu ya chama kuongea na waandishi.
BJP wamekishinda chama tawala Congress kupitia mgombea wao Mr. Modi ndani ya miaka 67.
Chadema wakiacha danganya toto wanaweza fanya haya la sivyo?
Wasubiri kesho kwenye gazeti la Tanzania Danganya watakavyopamba "UPINZANI "WAINGIA IKULU" tofauti na ushindi wa ANC kule A.kusini hatukusikia kitu.
WANANCHI SI KUDANGANYA bali wa kuambiwa ukweli. Usiwalazimishe wakuonee huruma kwa matakwa yako"
WAPINZANI NA CCM JIFUNZENI

Kimerejea tena Madarakani kwani miaka kumi iliyopita kiliondolewa madarakani na Congress pamoja na washirika wake
 
India Election Result: Narendra Modi Sweeps To Victory, Indian Stocks Soar
The Bharatiya Janata Party has scored a major victory and appears on track to have won a majority of seats in the lower house of Parliament, pulling off the best election performance by a single party in decades and paving the way for Narendra Modi to become the nation’s next Prime Minister

The exit polls seem to have made the right call on India’s federal elections in which a record 550 million people cast their votes to select the country’s new prime minister: their choice is Narendra Modi, the fiery, business-friendly leader of the Bharatiya Janata Party (BJP) whose party has romped home to a resounding victory. Modi tweeted, “India has won. Good days lie ahead”
Within two hours after the counting of votes began, it became apparent that the BJP-led National Democratic Alliance was returning to power. The BJP which needed to win 272 seats to get a clear majority in the country’s 543-seat Parliament, looks set to cross the 300-seat mark with its allies. According to Times Now television, the BJP has so far been leading in 278 seats, crossing predictions of a 250-seat haul. For the first time in 30 years, a single party looks set to win a clear majority on its own steam, ending an era of coalition politics.
The ruling Congress Party ( CCM YA INDIA WITH FAMILIY LINKS )has suffered a devastating defeat, pulling in an abysmal tally of 52 seats, according to Times Now. Even as blame for the poor performance was being laid at the door of Congress scion Rahul Gandhi who at the time of writing is barely hanging on to his seat in Amethi in the northern Indian state of Uttar Pradesh, the traditional stronghold of the Gandhi family, party spokespeople were still defending him. The Congress-led United Progressive PGR +0.24% Alliance has overseen the country’s economic slide in the past five years amid a plethora of corruption scandals.
 
Ushindi wa ANC ni salamu tosha kwa CHADEMA na UKAWA yao
Tume ya uchaguzi nchini Afrika ya Kusini imekamilisha zoezi la kuhesababu kura na kutangaza kwamba, Chama tawala cha ANC kimeshinda kwa asilimia 62.2% na kwamba, Chama cha upinzani cha Democratic Alliance kinachoongozwa na Bi Hellen Zille, kimepata asilimia 22.23% ya kura zote zilizopigwa, ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 5%, ikilinganishwa na kura za mwaka 2009. Chama cha Economic Freedom cha Julius Malema kinachotaka kuwagawia maskini utajiri wa nchi kimepata asilimia 6.35%.

Taarifa inaonesha kwamba, wananchi wa Afrika ya Kusini waliojitokeza kupiga kura katika uchaguzi mkuu uliomalizika walikuwa ni sawa na asilimia 73% ya wananchi millioni 25 wa Afrika ya Kusini. Hii ni sawa na asilimia 50% ya idadi ya wananchi wote waliojiandikisha kupiga kura. Rais Jacob Zuma anasema anapania kuboresha huduma msingi za kijamii kwa wananchi wengi wa Afrika ya Kusini.

Ushindi huu ni ishara tosha kuwa vyama vya upinzani barani Afrika vina safari ndefu ya kuviangusha vyama vinavyopigania ukombozi wa kweli wa wananchi wake. Hapa kwetu baada ya vyama vya CUF na CHADEMA kufa kifo cha mende, vimeamua kuunda jukwaa lisilo rasmi lijulikanalo kama UKAWA ambalo nalo limepoteza muelekeo kutokana na kukosa ajenda kwa wananchi. Viongozi wa UKAWA ni kama watu wasio na uwezo wa kufikiri kwani kwa sasa wakati watanzania wanajikita kwenye Bajeti Mpya ya Serikali, wao wapo busy na Katiba ambayo waliamua kuisusia wakati wa Bunge la Maalum. Hellen Zille namfananisha na Dr Slaa. Wakati wa uchaguzi uliopita, alitamba sana kuwa uchaguzi wa mwaka huu angeweza kushinda. Sasa kaangukia pua japo chama chake kimeongeza kidogo kura baada ya waafrika weusi kuanza kukiunga mkono na hasa kutokana na matatizo ya ndani ya ANC. Dr Slaa naye akiendelea kung'ang'ania kuwa atagombea 2015 atashindwa vibaya mno.

Hizo ni salamu tu kwa wapinzani kwamba hamna chenu ndani ya siasa za Bara ya Afrika. Sijui mtajifunza kutoka nchi gani maana kila kona mnazidi kukabwa tu.
 
HII SI MLILETA UZI WAKE HAPA UKADHARAULIWA NA KILA MWENYE AKILI ! SAsa KWANINI UNAUCHOMEKEA KWENYE NYUZI ZA WATU ? MBONA UMEISHIWA MAWAZO KIASI CHA KUTISHA SANA !
 
ccm itaongoza nchi hii milele

Unaweza usijue akili ya mtu lakini neno lake moja tu linaweza kukuonyesha uwezo wa mtu kiakili,umilele ni kwa MUNGU tu mkuu,jitahidini siasa zisikufumbe macho na kumkufuru MUNGU!!binafsi bado naamini kuwa ccm wana nguvu kubwa fotauti na wapinzani wanavyofikiria!!lakini kusema watatawala milele nitakuwa nimeamua kujitoa ufahamu!!
 
na ushindi wa wapinzani india siyo salamu tosha ccm na interahamwe yao?
Ushindi wa ANC ni salamu tosha kwa CHADEMA na UKAWA yao
Tume ya uchaguzi nchini Afrika ya Kusini imekamilisha zoezi la kuhesababu kura na kutangaza kwamba, Chama tawala cha ANC kimeshinda kwa asilimia 62.2% na kwamba, Chama cha upinzani cha Democratic Alliance kinachoongozwa na Bi Hellen Zille, kimepata asilimia 22.23% ya kura zote zilizopigwa, ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 5%, ikilinganishwa na kura za mwaka 2009. Chama cha Economic Freedom cha Julius Malema kinachotaka kuwagawia maskini utajiri wa nchi kimepata asilimia 6.35%.

Taarifa inaonesha kwamba, wananchi wa Afrika ya Kusini waliojitokeza kupiga kura katika uchaguzi mkuu uliomalizika walikuwa ni sawa na asilimia 73% ya wananchi millioni 25 wa Afrika ya Kusini. Hii ni sawa na asilimia 50% ya idadi ya wananchi wote waliojiandikisha kupiga kura. Rais Jacob Zuma anasema anapania kuboresha huduma msingi za kijamii kwa wananchi wengi wa Afrika ya Kusini.

Ushindi huu ni ishara tosha kuwa vyama vya upinzani barani Afrika vina safari ndefu ya kuviangusha vyama vinavyopigania ukombozi wa kweli wa wananchi wake. Hapa kwetu baada ya vyama vya CUF na CHADEMA kufa kifo cha mende, vimeamua kuunda jukwaa lisilo rasmi lijulikanalo kama UKAWA ambalo nalo limepoteza muelekeo kutokana na kukosa ajenda kwa wananchi. Viongozi wa UKAWA ni kama watu wasio na uwezo wa kufikiri kwani kwa sasa wakati watanzania wanajikita kwenye Bajeti Mpya ya Serikali, wao wapo busy na Katiba ambayo waliamua kuisusia wakati wa Bunge la Maalum. Hellen Zille namfananisha na Dr Slaa. Wakati wa uchaguzi uliopita, alitamba sana kuwa uchaguzi wa mwaka huu angeweza kushinda. Sasa kaangukia pua japo chama chake kimeongeza kidogo kura baada ya waafrika weusi kuanza kukiunga mkono na hasa kutokana na matatizo ya ndani ya ANC. Dr Slaa naye akiendelea kung'ang'ania kuwa atagombea 2015 atashindwa vibaya mno.

Hizo ni salamu tu kwa wapinzani kwamba hamna chenu ndani ya siasa za Bara ya Afrika. Sijui mtajifunza kutoka nchi gani maana kila kona mnazidi kukabwa tu.
 
Chama cha upinzani nchini India BJP kimeshinda uchaguzi mkuu kwa kupata idadi kubwa zaidi ya kura kuliko chama kingine chochote.
Kiongozi wa chama BJP Narendra Modi,amesema kuwa wananchi wajiandae kwa mambo mazuri
Matokeo ya awali yalionyesha kuwa chama hicho kimepata kura nyingi kiasi cha kuweza kutawala bila ushirikiano wowote na chama kingine.

Wafuasi wa upinzani wanasherehekeakatika makao makuu ya chama hicho.
Chama tawala cha Congress kimeshindwa baada ya kuwa mamlakani kwa miaka kumi
Kura ambazo zimehesabiwa kufikia sasa zinaonyesha kuwa muungano wa vyama unaoongozwa na chama BJP, chini ya Bwana Narendra Modi, utashinda kwa wingi wa kura.
Tayari shangwe, vifijo na nderemo vimeshuhudiwa na kusikika katika makao makuu ya BJP huku wanachama wakicheza densi barabarani na fataki kulipuliwa.
Tume ya Uchaguzi ya India imesema kuwa matokeo ya awali yanathibitisha kuwa BJP kimeshinda viti 272, vinavyokiwezesha kutawala bila kushirikiana na chama kingine.
Zaidi ya watu milioni 500 walipiga kura ambayo ni asilimia 66 ya wote waliochaguliwa
source bbc

mytake:ccm ni vizuri mkaona yanayowakuta wenzenu maana zile dhana za ccm ni chama dume zimepitwa na wakati na kwa maneno ya mwalimu kama wananchi wasipopata maendeleo ndani ya ccm watayatafuta nje ya ccm yatakuwa yametimia
 
Back
Top Bottom