Chama cha mapinduzi hakipo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chama cha mapinduzi hakipo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mundali, Oct 28, 2011.

 1. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2011
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Wana JF salaam.
  Najua wengi mtashangazwa na thread yangu, lakini kwa kusukumwa na utashi na hisia za mabadiliko ya kifikra, kisiasa na kiuchumi wa taifa letu, na ili kujibu hoja dhaifu za wafuasi wa CCM. Kwa mtazamo wangu chama cha mapinduzi (CCM) hakipo.
  Kwa tafsiri isiyo rasmi, chama cha kisiasa ni muungano wa watu wenye nia na lengo moja la kisiasa. Muungano huu huwezesha wanachama kutengeneza mkataba ambao watauamini na kuutekeleza katika kutimiza malengo yao. Mkataba huo huitwa KATIBA. Hivyo chama kinaishi kwa kutokana na uwepo wa wanachama na katiba (mtazamo wangu).
  Turejee mambo muhimu na ya msingi katika katiba ya CCM (Toleo la14 la mwaka 2010).

  IMANI YA CCM (Ibara ya 4)Ibara ya 4(1) Binadamu wote ni sawa.
  Ibara ya 4(2) Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake.
  Ibara ya 4(3) Ujamaa na kujitegemea ndio njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru.

  MALENGO NA MADHUMUNI YA CCM (Ibara ya 5)

  Ibara ya 5(3) Kuhimiza ujenzi wa ujamaa na kujitegemea kwa mujibu wa Azimio la Arusha.
  Ibara ya 5(9) Kuona kwamba nchi yetu inatawaliwa kwa misingi ya kidemokrasia na ya kijamaa.

  SEHEMU YA PILI
  WANACHAMA
  Ibara ya 7. Raia yoyote wa Tanzania mwenye umri usiopungua miaka 18, anaweza kuwa mwanachama wa CCM iwapo anakubali Imani, Malengo na Madhumuni ya CCM.

  WAJIBU WA MWANACHAMA (Ibara ya15)
  Ibara ya 15(5) Kukiri kwa imani na kutekeleza kwa vitendo siasa ya CCM ya ujamaa na kujitegemea.

  Pia katiba ya CCM imeweka ahadi za mwana CCM, zipo 9. Hapa ntaongelea ahadi tano tu.
  Ahadi ya 4: Rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa.
  Ahadi ya 5: Cheo ni dhamana, sitatumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu.
  Ahadi ya 6: Nitajielimisha kwa kadiri ya uwezo wangu na kuitumiaelimu yangu kwa faida ya wote.
  Ahadi ya 8: Nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko.
  Ahadi ya 9: Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa CCM na raia mwema wa Tanzania na Afrika.

  Kwa mujibu wa vipengele hivyo vya katiba ya CCM, mambo yafuatayo yanakitokea CCM haina viongozi (kwa sababu hawaamini katika katiba yao), ama haina wanachama, kama isemavyo ibara ya 7. Vinginevyo wanachama wa CCM na viongozi wake wanatekeleza malengo na madhumuni ambayo hawakujiwekea kwa mujibu wa katiba yao, hivyo wanakiuka katiba. Chama kinachopingana na katiba yake kimekufa.
  Uwezekano wa pili ni kwamba CCM haina katiba, ama wana katiba ya nyuma ya pazia. Sababu CCM kupitia kwa viongozi wake wameikana katiba ya sasa na wameukana wajibu wao kama isemavyo ibara ya 15.
  Hivyo basi CCM haipo kwa mujibu wa katiba yao, na haistahili kuongoza nchi.
  Nawasilisha.
   
 2. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  mkuu uliyoyaandika nakubaliana nayo mia kwa mia.na hii inadhihilisha ulivyo na akili sana.sasa hivi chama kinachotambulika kitaifa na kimataifa na ambacho kipo kwa ajili ya wanyonge na watanzania wote kwa ujumla bila kujari itikadi zao ni CHADEMA.mia
   
 3. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  CCM ilikufa toka 1992 wakati mfumo wa vyama vingi ulipoanza, hakikusajiliwa upya kama katiba ilivyotamka, hivyo kinaweza kujikuta kikifutwa endapo mtu makini atashika ofisi ya Msajili wa vyama.
   
 4. SILENT ACtOR

  SILENT ACtOR JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  The fact ni kwamba chama bado kipo, isipokuwa kimepoteza uhalali wa kuiongoza Tanzania, wanatumia mbinu chafu kuendelea kutawala.
   
 5. f

  firehim Member

  #5
  Oct 28, 2011
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 94
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  .

  naomba utuwekee na ya CHADEMA kama utaipata
   
 6. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,437
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mkuu umenena!! kudos!! Kama bado katiba yao ndiyo hii basi hii CCM sio yenyewe!!!
   
 7. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #7
  Oct 28, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Tunaomba sasa utueleze chama kilichopo Na kivipi kipo
  eg CHADEMA, CUF na NCCR - MAGEUZI

  (ila nasikia CHADEMA hawana falsafa ya chama kama )
   
 8. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #8
  Oct 28, 2011
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Tembelea www.chadema.or.tz, utapata kila unachokihitaji kuhusu chama hicho.
   
 9. Alexism

  Alexism JF-Expert Member

  #9
  Oct 28, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 2,442
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  Mkuu niliwai kuandika na kupost kama mara sita hivi nikiwa ninauliza uhalali wa CCM kama chama lakini mods walipotezea mpaka nikawa na tasfiri mbaya dhidi yao.
  CCM siyo chama halali kulingana na political party act 1992.
  Kwani hakikufuata sheria hizo.
   
 10. M

  Makupa JF-Expert Member

  #10
  Oct 28, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Hata cdm wanatekeleza malengo nje ya katiba mfano swala la kitumia nguvu za giza ila kuvuta umati wa watu kwenye mikutano yao
   
 11. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #11
  Oct 28, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 280
  Soma thread vizuri. Kipo wapi? Hakina katiba , hakikusajiwa upya kama sheria invyosema, Kinaongoza taifa la kufikirika linaloamini siasa za UJAMAA NA KUJITEGEMEA. kwa hiyo hakipo ndio maana kimepoteza huo uhalali unaouzungumzia.
   
 12. Alexism

  Alexism JF-Expert Member

  #12
  Oct 28, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 2,442
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  umetoroka jera au vipi?
   
Loading...