Chama cha madaktari (MAT) hakina uwezo wa kisheria kuitisha migomo

Chama cha madaktari (mat) hakina uwezo wa kisheria kuitisha migomo
....To promote the medical and allied sciences, to maintain the honour and interests of the medical professions and to uphold a high standard of medical ethics and conduct among its members. To act as representative body of the medical profession in Tanzania and to liaise with and advise the Government on health and medical matters. To ensure, maintain and safeguard the interests privileges and welfare of its members.....​

Soma hayo malengo ya hicho chama.
 
Kwanini usiwashauri ndugu zako au wewe mwenyewe ukasomee udaktari ili usaidie watanzania? Watanzania mnalalamika sana bila kutoa majibu.

Hata kama una ndugu daktari au wewe mwenyewe haina maana kukosa kujua ubaya wa kuua wagonjwa.
 
Hawa Madaktari ni wanyama mmetaka mganga mkuu na katibu mkuu wa wizara waondolewe serikali imefanya hivyo. Saizi mnapa tena amri rais nyie kweli makanjanja wala hamna huruma na binadamu wenzenu.
Hapana madaktari sio wabaya, wabaya kuliko kawaida ni Pinda, Mponda na Lucy Nkya ambao wanalilia posho za vikao vya bunge badala ya kuboresha huduma za afya.
 
Wote sisi, hata wewe, hebu kumbuka tu, kama una akili utatambua hilo kama huna basi hutajua kwamba wazazi wako nao ni wanyama!
 
"..hakina uwezo wa kisheria..." lakini wana uwezo wa kiakili na utashi wa kutenda na kusimamia maslahi yao kama tunavyoona na kusikia! That's all matter, the rest is mere filling the air with hot vapour
 
Nilipoteza ndugu katika mgomo wa kwanza sitaki kusikia habari ya kugoma kwa njia hii ya kuweka rehani uhai wa binadamu.

Lakini serikali yako iko tayari watu wengine wapoteze maisha.
umefanya nini kwa hilo?
 
jamani, tuna tatizo la msingi katika hili. Na sidhani kama tatizo hilo la msingi ni MAT na usajili wake. Tuache haya masuala ya kutafuta mchawi, tutatue tatizo ili tusonge mbele
Mkuu nakubaliana na wewe, na kwakweli tatizo limezalishwa na serikali iliyoundwa na wanamtanandao bila malengo.
 
Kimsingi baadhi ya wachangiaji mnataka kifanya maada hii iwe na mfumo wa kisiasa na wakati kiasili hili ni swala la kitaaluma, Miiko kumkataza mtu kugama sio nafasi ya mwingine kumkandamiza, miiko sio laana kwamba umefungiwa nayo ili ufe nayo hata kama unakandamizwa, miiko ni miiko lakini ubinadamu, utashi na masilahi viko palepale. Kama kitaaluma wao wameona Mawaziri sio watu sahihi kuitetea taaluma yao na wanaidhohofisha, nafirikiri wachangiaji tunge jikita kutafuta ukweli baina ya pande hizi mbili kiutendaji na tuje na majibu sahihi juu ya suala halisi.

Wakati mwingine nashangaa sana, hivi kunatatizo gani kama Waziri au mtu yeyote( Ngazi yoyote) atagomewa na watendaji wake kwa sababu ya utendaji wake usio na masilahi kwa taasisi yake?. Kwa mtazamo wangu ni hoja mbovu kuogopa kama watendaji Hao wa afya watafukuzwa tutakuwa tumefuangulia watendaji kufukuzwa.

Nani asiyejua ubovu wa watendaji wa serikali ambayo mara nyingi mioyo yetu imeuma ikitamani wabadilike? je hatuoni kama hii ni njia njema ya kuwajibisha watendaji ikiwa kama ni kweli ni mizigo kwa taasisi husika?

Nafikiri wachangiaji tujiridhisha na tuhuma za kila upande kabla ya Kuhukumu. wenyewe (Madaktari na Serikali) wameanza kuhukumiana, sisi tusifuate Mkumbo tutafute ukweli.
 
"To act as representative body of the medical profession in Tanzania and to liaise with and advise the Government on health and medical matters."
They advised the government that the minister and his deputy should go, the govt. agreed, why is the govt. not implementing those decisions?
WaTZ tunashangaza moja ya madai ya madaktari ni serikali kuimprove huduma za afya. Tumesikia wagonjwa walio muhimbili wanatueleza mashine fulani imekufa, mashine fulani haifanyi kazi, dawa fulani hakuna, kwenye hospitali za mikoa na wilaya na hizo teule ndiyo kabisa, unalipa hela lakini ukiandikiwa dawa inawekewa X yaani kanunue mitaani. Huko bei ni kichaa na nyingine ni fake. Kwa nini tusiwaunge mkono?
Kuna mtu anasema waajiri madr. toka nje, anadhani hao utakuja kuwalipa shs 900,000? Nilifanya kazi kwenye hoteli moja. huo ni net pay ya banquet manager toka kenya, je Dr. wa uhakika! Labda upate wa kuchakachua.
Na huko Tazara, utapeleka wanajeshi kuendesha train? Na waalimu, utaajiri waalimu 34,000 toka nje. Tushughulikie kiini cha tatizo na si matokeo
Tatizo la madr, naona hawako united, Wangegoma wote Tanzania nzima,ndani ya siku 2 serikali ingesikiliza na hivyo madhara kwa wananchi yasingekuwa makubwa lakini hii mara hawa wamegoma hawa bado, hawa wanaingia na kutoka ni mbaya zaidi.
 
Nilipoteza ndugu katika mgomo wa kwanza sitaki kusikia habari ya kugoma kwa njia hii ya kuweka rehani uhai wa binadamu.

Hivi kama kweli mnaamini hili kwanini hamtaki serikali iwafukuze kazi hawa watu wawili? Kama watu wamechoshwa kweli na mgomo ni wakati wa kudai serikali iwaondoe hawa jamaa ili madaktari warudi kazini na majadiliano yenye maana yafanyike chini ya hali ya kuaminiana na siyo hali ya kutumiana.
 
MaDaktari wetu waondoe UNAFIKI wa wazi wanaounyesha hasa hawa wa hapa Dar. Wasigome kibiashara. Sidhani na siamini kuwa hali katika hospitali zetu ni mbaya zaidi kuliko ilivyokuwa miaka kumi iliyopita! Kwa nini mgomo sasa?
 
Nungana na wewe kuwa watanzania ni mazuzu,ingiene barabarani leo kama serikali yenu dhaifu haitakubali mchakato wa maboresho wa huduma za afya
 
Madaktari bingwa wananufaika zaidi na mgomo huu. Zahanati zao na hospitali zao zinatengeneza pesa kwelikweli kipindi hiki. Nilipita Tumaini na TMJ jana kulikuwa kumependeza sana. Sisi wengine tuendelee tu kushabikia hali hii kama mazuzu! Mgomo ungekuwa ni kwa MASLAHI ya NCHI hakuna DAKTARI hata mmoja angeenda kazini hata wale wa hospitali binafsi.


Mahospital binafsi watagoma tu watakapozidiwa, maana huko nako hakuko kuzuri kiasi hicho na ndipo tutakapolia na kusaga meno kweli ila sema tutafunguka tu!

Tuendelee na siasa kwanza, ngojea huu mgomo ufike miezi michache ndipo tutakapoona cha moto. Tatizo tunafikiria hawa madaktari wanatania na kuwa watahangaika na propaganda za hakuna mgomo au kila kitu kipo sawa. Hii generation ni tofauti na ile ya wakina mwalimu nyerere, na once generation ya kina kikwete nayo itakapotokomea hali itakuwa nzuri zaidi.
 
Chama cha Madaktari Tanzania ni Chama Cha hiyari na si Chama cha Wafanyakazi ambacho kina UWEZO WA KUITISHA MIGOMO. Kwa mujibu wa masharti ya usajili wa TMA, hakuna kipengele kinachotoa mamlaka kwa MAT kuitisha migomo. Kitendo cha kuitisha migomo ni sababu tosha kwa Msajili wa Vyama vya Hiyari kukifuta Chama hiki ambacho kinaenda nje ya majukumu yake kisheria. Tembelea tovuti ya Chama hiki utakuta kuwa chama hiki kinaongozwa pia na MAADILI (medical ethics). Welcome to Medical Association of Tanzania


“To promote the medical and allied sciences, to maintain the honour and interests of the medical professions and to uphold a high standard of medical ethics and conduct among its members. To act as representative body of the medical profession in Tanzania and to liaise with and advise the Government on health and medical matters. To ensure, maintain and safeguard the interests privileges and welfare of its members.

Moja ya maadili ya madaktari ni kutosababisha madhara kwa wagonjwa.

Kwa sababu uchumi wetu ni wa soko huria, madaktari ambao hawapendi kufanya katika sekta ya umma wawe na ujasiri wa kuondoka na kupeleka huduma zao hospitali binafsi na huko ni soko huria ambalo litawachuja wazuri na wasio wazuri.

Hatua zinazostahili kuchukuliwa:

  1. Msajili wa Vyama vya Hiyari afanye kazi yake na arejee usajili MAT ili ajiridhishe kama MAT bado inastahili usajili kama chama cha hiyari;
  2. Kila daktari ana mkataba binafsi wa kazi. Asiyehudhuria kazini asilipwe mshahara mwisho wa mwezi huu. Kuhudhuria kazini sio kusani kitabu cha mahdhurio na kuondoka;
  3. Mwanasheria Mkuu wa Serikali akaombe tamko la Mahakama ya Kazi kuwa MAT hawana mamlaka kuitisha migomo na pia madaktari wanaotoa essential services wana utaratibu wa kugoma ambao haukufuatwa.
  4. Madaktari kutoka nchi za nje wanaotaka kufanya kazi Tanzania wakaribishwe na wapewe vibali vya kufanya kazi;
  5. Hatua za Kisheria zichukuliwe dhidi wa wafanyakazi wanaotoa huduma maalum (Essential Services) wanaogoma kinyume na sheria.

Mgomo wa madaktari unahatarisha usalama wan chi yetu kwa sababu sasa unabeba sura ya kisiasa kupitia chama cha hiyari. Hatua zisipochukuliwa, vyama vingine vya hiyari vitafuata mkumbo wa kuvunja sheria. Usalama wan chi uko hatarini pale wenye taaluma na elimu nzuri wanapovunja sheria bila hatua madhubuti kuchukuliwa. MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Hapo kwenye namba 4 umechemka.Hivi kuna daktari kutoka nje anaweza kuja kufanya kazi Tanzania tena serikalini?
Pinda anaposema serikali imejiandaa kukabiliana na mgomo anataka kutuletea madaktari wa mifugo watibu binadam?
 
MaDaktari wetu waondoe UNAFIKI wa wazi wanaounyesha hasa hawa wa hapa Dar. Wasigome kibiashara. Sidhani na siamini kuwa hali katika hospitali zetu ni mbaya zaidi kuliko ilivyokuwa miaka kumi iliyopita! Kwa nini mgomo sasa?

Ndugu hali ni mbaya sana kuliko miaka kumi iliyopita. Wizara haina hata senti tano (imefilisika!) sijui bajeti yao ndio waliidhinisha kwa ajili ya kupeleka viongozi nnje au vipi. Endelea kupiga propaganda, ila ungekuwa makini ungenyanyuka hapo ulipo na kwenda kuangalia hali halisi, au uongee na viongozi wa nchii hii. NASHANGAA KWA NInI HAWATANGAZI HALI YA HATATARI! Ili waTanzania tujifunge mikanda!
 
Hivi kama kweli mnaamini hili kwanini hamtaki serikali iwafukuze kazi hawa watu wawili? Kama watu wamechoshwa kweli na mgomo ni wakati wa kudai serikali iwaondoe hawa jamaa ili madaktari warudi kazini na majadiliano yenye maana yafanyike chini ya hali ya kuaminiana na siyo hali ya kutumiana.
Mwanakijiji,
Tuwaombe na MAT iwafukuze wanachama wao wanaoendelea na kazi kwenye zahanati na hospitali binafsi. Bahati mbaya kabisa hao wanaogoma Muhimbili na Amana baadhi yao unawakuta tena Tumaini, TMJ, Hindu Mandal,..., mgomo ni azimio la NGO yao MAT. Wote walitekeleze azimio hili.
 
Madaktari bingwa wananufaika zaidi na mgomo huu. Zahanati zao na hospitali zao zinatengeneza pesa kwelikweli kipindi hiki. Nilipita Tumaini na TMJ jana kulikuwa kumependeza sana. Sisi wengine tuendelee tu kushabikia hali hii kama mazuzu! Mgomo ungekuwa ni kwa MASLAHI ya NCHI hakuna DAKTARI hata mmoja angeenda kazini hata wale wa hospitali binafsi.
Nchi=Selikali? Tafakari!
 
Kwa nini serikali inakwepa kuchukua hatua kwa visingizio vya kitoto? Mara viapo vya madaktari, mara chama chao (MAT) hakina mamlaka kisheria kuongoza mgomo! Kama MAT ni kanyaboya kwa nini Pinda alikutana nao? Kwa nini Pinda alifanyia kazi baadhi ya madai ya MAT i.e. kumsimamisha kazi Blandina Nyoni na mganga mkuu?

Naona kuna nguvu kubwa sana inatumika ili kufanya madai ya madaktari yaonekane kama ni mchezo wa kisiasa. Yupo mdau mmoja ameandika humu kuwa asilimia ya vifo vya watu wanaofanyiwa operation ni kwa sababu ya uchafu. Na madaktari walisimama mbele ya waziri mkuu week chache zilizopita na kumuueleza (tena kwa utulivu kabisa) kuwa wamachoka kuona wagonjwa wanakufa kwa kukosa tiba sahihi! Pinda amefanya nini tangu kurekebisha hilo?

Kwa nini hili kundi la watibiwa India (cabinet) wasingetumia muda wao kutatua matatizo yaliyoorodheshwa na madaktari badala ya kutumia nguvu kubwa kuwapaka matope hao madaktari?
 
Back
Top Bottom