Chama cha madaktari (MAT) hakina uwezo wa kisheria kuitisha migomo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chama cha madaktari (MAT) hakina uwezo wa kisheria kuitisha migomo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Teroburu, Mar 8, 2012.

 1. T

  Teroburu Member

  #1
  Mar 8, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chama cha Madaktari Tanzania ni Chama Cha hiyari na si Chama cha Wafanyakazi ambacho kina UWEZO WA KUITISHA MIGOMO. Kwa mujibu wa masharti ya usajili wa TMA, hakuna kipengele kinachotoa mamlaka kwa MAT kuitisha migomo. Kitendo cha kuitisha migomo ni sababu tosha kwa Msajili wa Vyama vya Hiyari kukifuta Chama hiki ambacho kinaenda nje ya majukumu yake kisheria. Tembelea tovuti ya Chama hiki utakuta kuwa chama hiki kinaongozwa pia na MAADILI (medical ethics). Welcome to Medical Association of Tanzania

  "To promote the medical and allied sciences, to maintain the honour and interests of the medical professions and to uphold a high standard of medical ethics and conduct among its members. To act as representative body of the medical profession in Tanzania and to liaise with and advise the Government on health and medical matters. To ensure, maintain and safeguard the interests privileges and welfare of its members.

  Moja ya maadili ya madaktari ni kutosababisha madhara kwa wagonjwa.

  Kwa sababu uchumi wetu ni wa soko huria, madaktari ambao hawapendi kufanya katika sekta ya umma wawe na ujasiri wa kuondoka na kupeleka huduma zao hospitali binafsi na huko ni soko huria ambalo litawachuja wazuri na wasio wazuri.

  Hatua zinazostahili kuchukuliwa:

  1. Msajili wa Vyama vya Hiyari afanye kazi yake na arejee usajili MAT ili ajiridhishe kama MAT bado inastahili usajili kama chama cha hiyari;
  2. Kila daktari ana mkataba binafsi wa kazi. Asiyehudhuria kazini asilipwe mshahara mwisho wa mwezi huu. Kuhudhuria kazini sio kusani kitabu cha mahdhurio na kuondoka;
  3. Mwanasheria Mkuu wa Serikali akaombe tamko la Mahakama ya Kazi kuwa MAT hawana mamlaka kuitisha migomo na pia madaktari wanaotoa essential services wana utaratibu wa kugoma ambao haukufuatwa.
  4. Madaktari kutoka nchi za nje wanaotaka kufanya kazi Tanzania wakaribishwe na wapewe vibali vya kufanya kazi;
  5. Hatua za Kisheria zichukuliwe dhidi wa wafanyakazi wanaotoa huduma maalum (Essential Services) wanaogoma kinyume na sheria.

  Mgomo wa madaktari unahatarisha usalama wan chi yetu kwa sababu sasa unabeba sura ya kisiasa kupitia chama cha hiyari. Hatua zisipochukuliwa, vyama vingine vya hiyari vitafuata mkumbo wa kuvunja sheria. Usalama wan chi uko hatarini pale wenye taaluma na elimu nzuri wanapovunja sheria bila hatua madhubuti kuchukuliwa. MUNGU IBARIKI TANZANIA.
   
 2. Avanti

  Avanti JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2012
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 1,209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  kwa kweli nao wamezidi< hata hatupumui sasa< kila kitu serikali serikali< mwishowe wakiondoka hao mawaziri itakuwa zamu ya pinda sasa kuondoka> these people just want to unmake the government as they do not consider principles of natural justice
   
 3. s

  sent items Member

  #3
  Mar 8, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa Madaktari ni wanyama mmetaka mganga mkuu na katibu mkuu wa wizara waondolewe serikali imefanya hivyo. Saizi mnapa tena amri rais nyie kweli makanjanja wala hamna huruma na binadamu wenzenu.
   
 4. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2012
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Kama ungekuwa unajua unachokiongea...hayo uliyoandika hapo juu ungeupeleka kwa msajili...sio JF!
   
 5. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  endeleeni na propaganda tu baada ya kusolve tatizo
   
 6. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #6
  Mar 8, 2012
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Aisee!

  Naona sasa mmeanza kufanya Home Work zenu.

  Mgomo ni mgomo.

  Sijui kama kunamgomo halali mbele ya serikali yeyote Duniani.

  Ukifuta Chama cha Hiari watu Madaktari watakutana kwa hiari bila kuwa na Chama.

  Zisi pipo bwana!

  Government has failed to fulfill its obligations now it is trying to assassinate the character of Dr's unity.
  You might ban all organisations,you might stop all gathering , you might condemn all citizens in the effort to stop being attacked by Truth but you will never be able to stop the Will and Power of the PIPO.
  What made Drs to come together is not their Organisation but it is the reality of the situation they face every day in their effort to provide services to their fellow Tanzanian.
  So many patients have died in their hands simply because they don't have right equipment and medications.
  Patient have to be admitted in the wards which have no running water and full functional toilets.
  So much funding for Hospitals welfare have been swindled by Government officialls denying patients from full Drs services
  We have beautiful laws and rules in our books, but laws without accountability is a big source of chaos.
  The CCM Government is not accountable to itself and the PIPO who put it there.
  Physically and By Definition we have Government.
  Functionally, the CCM Government is DEAD and all Government officials including Jakaya Mrisho Kikwete are either schizophrenia or walking Zombie
   
 7. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #7
  Mar 8, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  We chizi kweli watu wakidai haki yao eti hawana haki ya kugoma. Nchi hii bwana ukitaka kugombana na mtu dai haki yako.
   
 8. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #8
  Mar 8, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Haya nyie semeni hawana uwezo. Mbona wameongoza mgomo na wanagoma, sasa hapo utasemaje hawana uwezo?

  Jueni kuwa serikali haina uwezo wa kuuzima mgomo huu kwa porojo isipokuwa imewaondoa Mponda na Nkya.
   
 9. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Your days are numbered and the writings are on the wall! Si mmekuwa mnadhani Watanzania watakuwa wajinga siku zote? Leo ndio mnakumbuka kuwa kuna sheria? Ukimfukuza sana mjusi hugeuka nyoka. Enough is enough, sasa ni zamu yenu, na huu ni mwanzo tu.
   
 10. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #10
  Mar 8, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  100% Perfect. Big up. Wapishe hao Madaktari wasiotaka ajira ya serikali kwa nini wang'ang'anie?
   
 11. Kirode

  Kirode JF-Expert Member

  #11
  Mar 8, 2012
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 3,573
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nilipe nisepe........
   
 12. Mbutunanga

  Mbutunanga Senior Member

  #12
  Mar 8, 2012
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 183
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  Nakumbuka kwenye madai yao waliyomtumia waziri mkuu tena kwa maandishi waliainisha bayana kuwa viongozi wanne pale wazarani wameshindwa kutekeleza majukumu yao.

  Walianza kumtaja kinara wao kuwa alikuwa ni Blandina, ambaye waliandika kabisa kuwa likuwa na kejeli kwa madaktari na watumishi wengine wa afya pale wizarani, na madudu mengine yalikuja jitokeza mbele ya safari.

  Mtasiwa: yeye aliwatukana wazi madaktari kwenye vyombo vya habari

  Mponda: yeye wakati fukoto la mgomo linaendelea yeye alidai hawezi wasikiliza madaktari bali muda wake anautumia kuwasikiliza wakulima na wafugaji jimboni mwake ( sasa anapewa nafasi ya kwenda kukaa zaidi na wananchi wake wa jimboni, kwa nini hataki kwenda?) Je ule uwongo alioutoa bungeni hastahili kuwajibishwa? Hivi inakuwaje hamuoni makosa ya hawa?

  Nkya: huyu ndio usiseme, ya kwake tuliyasikia kwa redio.


  Waziri mkuu aliwaambia atawaondoa wote, kinachomfanya abadili kauli ni nini? Au mpaka atengenezewe documentary kuonyesha kuwa aliwahadaa madaktari?
   
 13. Atukilia

  Atukilia JF-Expert Member

  #13
  Mar 8, 2012
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 643
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Hapa kuna mambo mawili
  1. Serikali ilishafanya mazungumzo nao hivyo hiyo ni implied condition kuwa wanatambua. Sio unazungumza ukishindwa unataka kukimbilia kwa msajili kudai upande mwingine sio halali. Kwa jinsi hali ilivyo la maana ni kupata ufumbuzi na sio kuanza kunyosheana vidole.
  2. Vyama vya wafanyakazi vinaelekea kufa na huenda likaibuka wimbi lingine la vyama vipya vya wafanyakazi kwa vile vilivyopo vinachukua muda mrefu sana kujadiliana na serikali. Generation ya sasa sio watu wa kusubiri kwa muda mrefu ki hivyo. Wanataka nyumba na maisha bora sasa sio mambo ya kununua mabati ukistaafu.
   
 14. E

  Escherichia Coli Senior Member

  #14
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umesahau kubold "TO MAINTAIN THE HONOUR AND INTERESTS OF MEDICAL PROFESSIONS".
   
 15. 4

  4change JF-Expert Member

  #15
  Mar 8, 2012
  Joined: Mar 4, 2012
  Messages: 535
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  hey man/woman!last strike was not organised by MAT,remember!
  Napita tu ntarudi baadae.
   
 16. p

  politiki JF-Expert Member

  #16
  Mar 8, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Hapo pekundu pamejibu swali lako la uwezo wa chama kuitisha maandamano kwani maandamano ni moja ya njia ya kuakikisha hilo jukumu lilotamkwa hapo pekundu limefikiwa kwahiyo ni ni dhairi MAT inafanya kazi inavyotakiwa.

  kuhusu haki ya kuandamana ni haki yao kama raia wa tanzania kama raia wa Tanzania. wapiga debe waligoma hamkuwauliza wamepata wapi haki ya kugoma leo hii wamegoma madaktari mnauliza walipopata haki ya kugoma acheni hizo.
   
 17. W

  WildCard JF-Expert Member

  #17
  Mar 8, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  TAZARA nao wamegoma. Wanataka Omar Nundu ajiuzulu. Nadhani watafuata Walimu, watataka Dr Shukuru Kawambwa ajiuzulu. Watakuja Polisi na askari Magereza, Mh Shamsi Nahodha aondoke. Wanajeshi nao watatafakari. Watakumbuka yale mabomu. Watagoma, Mh Hussein Mwinyi aondoke. Haya mambo ni sawa na kula nyama ya mtu.
   
 18. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #18
  Mar 8, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,317
  Likes Received: 2,604
  Trophy Points: 280
  mkuu hakuna mtu anayeng'ang'ania ajira ya serikali...
  madaktari wameweka rehani ajira zao kwa ajili ya maslahi ya afya ya watanzania...jaribu kurejea mapendekezo na mashinikizo waliyoyabainisha kwa serikali...
  hivi jukumu la kuhakikisha taasisi za afya zina mazingira na vitendea kazi stahiki ni nani kama sio serikali?...au unadhani udaktari ni taaluma tu isiyo hitaji mazingira na vitendea kazi madhubuti?....
   
 19. W

  WildCard JF-Expert Member

  #19
  Mar 8, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Madaktari bingwa wananufaika zaidi na mgomo huu. Zahanati zao na hospitali zao zinatengeneza pesa kwelikweli kipindi hiki. Nilipita Tumaini na TMJ jana kulikuwa kumependeza sana. Sisi wengine tuendelee tu kushabikia hali hii kama mazuzu! Mgomo ungekuwa ni kwa MASLAHI ya NCHI hakuna DAKTARI hata mmoja angeenda kazini hata wale wa hospitali binafsi.
   
 20. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #20
  Mar 8, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Umenena vema, maana umeainisha sekta zenye matatizo zaidi. Na kumbuka hukukaa uka-google ili kupata hiyo info, ni self-evident. Sijui kama ulikusudia ama la kusema ulichosema, but your internal self admits to this fact. So what does this tell us? YOU HAVE UNCONSCIOUSLY ADMITTED TO THE FAILURE OF THE ENTIRE GOVERNMENT! Thank you very much!
   
Loading...