Chama cha Kilaghai Tanzania...


1. Huna sababu ya kumtukana Wassira kuwasilisha hoja yako.
2. Sijui kama tatizo lako ni uwezo wa kielimu au uwezo wa kuelewa lugha ya kigeni. Kwa sababu nimeelezea nepotism na nikataja cronyism. Ingawa hii cronyism sikuielezea kwa undani. Kama ungekuwa unaelewa maana yake, basi majibu ya maswali uliyoniuliza ungeshayapata katika maelezo niliyoyaandika hapo awali.

Tafuta dictionary nzuri inayoweza kukueleza maana ya Cronyism kisha utapata majibu ya maswali yako.
 

Weka CV yako kwanza.
 
Njaa mbaya sana,povu lote hili mtu anapata hela ya kula mchana tu.
 
Mkuu Kijakazi nimekupata, hapa nilipo kuna ulaghai wa TANESCO.

Kuhusu wabunge kukaa Dar hili linatokana na mfumo wa kiutendaji, kila mbunge anayefuatilia huduma za jimboni kwake lazima mda mwingi awe Dar.
Suluhisho la hilo ni kutegemeza wananchi katika maeneo yao (MAJIMBO) na CDM hilo wameishaliona wanalitangaza.
 
Last edited by a moderator:
Tunataka tujue kama wewe ndiyo walewale ambao "wanaopata" -A- masomo tisa form four lakini hawawezi kupata C masomo matatu form six.

"Tunataka tujue" wewe nani mwingine? Isitoshe hata kama sijaenda Shule kabisa, lkn sishindwi kujua kwamba Mbunge anatakiwa awe ofisini kwake kila siku, kwa maana amechaguliwa na wananchi ambao wanamuhitaji jimboni, na si vinginevyo!
 

Du!! Watu muna mang'ana!!!! Ngoja nkae pembeni nisijepigwa tena ban with no reason.
 
umesahahu kuweka kundi la walala hoi nao wanaunga mkono chadema,ujakosea, kwa kuwa ccm na chama cha wenye fedha(mafisadi) tutashindana kwenye kura tuone watashinda mafisadi au hayo makundi uliyoyataja. mtaangaika sana lakini mwisho wenu ni 2015 na lazima tutawawajibisheni kwa kututia umasikini kwa miaka yote mliokuwa madarakani,hatutawaacha hivihivi, kama ni mali mtarudisha na jela mtaenda.tuna usongo sana na nyinyi,kadri mnavyozidi kutudharau ndivyo tunavyozidi kuwa na hazira dhidi yenu,na kama wanaosema hayo wanasema kwa kujipendekeza kwa mafisadi basi wanawaaribia nyie mafisadi, maana lazima mrudishe kila mlichofisadi na muingie jela.
 
Naomba nimkumbushe mleta uzi.Mwampamba Mtella,hakuchukizwa na mwenendo mbaya wa cdm,hapo ni kuchanganya mambo,huyu sehemu ya vijana walioombwa kwa fedha ninyi na ccm,zoezi likiratibiwa na nape,mwigulu na mzee wasira,sikatai kutokuwepo mapungufu ndani ya cdm,la hasha na kama yapo basi ni kawaida sana katika uendeshaji wa chama,kinachokuwa kwa kasi kubwa kama cdm,vipandikizi za hoja zenye hujuma za kulazima kama unavyotaka kuwaaminisha watu kwamba ni chama cha kikanda,kikabila.hizo ni propaganda zilizozoeleka kusikika japo katika uhalisia sio kweli,na mleta uzi huu ni sehemu ya watu wanakereka sana kuiona cdm inavyozidi kukua,na sio kweli kwamba eti umekuja na uzi huu ili cdm ijirekebishe,dhima yako ni kuichonganisha kwa mambo ya uongo yasiyokuwepo,na kama ni hivyo si bora uache ili chama kife chenyewe ili ccm,i takeoff kama ulivyoshauri kwamba ni bora kuendelea na ccm,kuliko vyama vingine kama cdm,
 

one of the JF's great thinkers, humu ndani watu aina yako wamekuwa nadra sana,au kama wapo basi hawashiriki kwenye mijadala kama huko zamani, akili na uelewa wako wa mambo ni wajuu zaidi, kwa maana hiyo inawapa watu wengi humu tabu ya kuchambua na kuelewa maoni yako, ila tufanyeje na JF imeingiliwa?

MSAFARA WA MAMBA KENGE HAWAKOSEKANI.
 

Hata hiyo bado sio ishu, ishu ni kwamba kama wao wanataka kuwa tofauti na wa CCM wangetuambia kwamba hizi pesa wanazozilipwa za jimbo SIYO halali yao kwa maana wanalipwa ili wawe Ofisini karibu na Wananchi wao Jimboni, na ndio maana ya Mbunge kuwa na Ofisi na sio vinginevyo, sasa Wabunge wa CCM wamekuwa wakitudhulumu miaka yote, wengine miaka 5 hawajawahi kukanyaga Jimboni, na Wapinzani nao hivyo siku ukimuona basi labda Raisi anakuja Jimboni kwake sasa tofauti iko wapi?

Pili kulibadilisha hilo hauhitaji sijui kusubiri sera mpya ya CHADEMA ya Majimbo, ni swala la uamuzi tu, ambao unaweza kufanyika hata leo wakiamua, kwani hata ukiweka Majimbo bado Magavana watakuwa wanaishi Sinza au Kinyerezi, lkn ofisi zao ziko Majimboni.

Tatu hata kama hata kama inabidi waje Dar kushughulikia mambo fulani inaeleweka lkn sio ktk siku 365 ni siku 30 tu ndio wako Ofisini, hilo halina utetezi!

Mwisho mimi sio mwanachama wa Chama chochote bado, ninatoa maoni tu kulingana najinsi ninavyoona!
 

Nawe pia ni gamba?
 
ila mbona una harufu ya masalia?
umeplay very low kutuambia Z'bar pana demokrasia!
hawa wazenji wamejgawa kimakund,mweus vs mwarab,muumguja vs mpemba na uktaka kuprove ilo angalia matokeo ya pemba na cuf ssm na unguja.
CDM ishaingia zenj subr ukuaj wake ..
 
Lakini pia ukiangalia kwa makini, utabaini kuwa CDM wanategeamea watu yaani wanafanya siasa za watu kwanza, sera baadaye. Hii ndo inafanya watu kama Slaa kujiona kuwa wao ni zaidi ya Chadema na anafanya atakavyo kwa sababu tu bila yeye hakuna Chama. Kimsingi huu ni udhaifu uliopitiliza.

Pia hivi sasa let's say kwamba Wachaga waache au wasiendelee kuwa na matumaini na Chadema, itakuwa na hali gani? Au wakatoriki wanaomchukulia Slaa kama tumaini lao, wakiacha kuamini hivyo, Chadema itakuwa na hali gani?
 
Mkuu vichanzi usemayo ni kweli,
Kama hajapigwa ban basi hii thread itafagiliwa chini ya kapeti haraka sana
 
Last edited by a moderator:
Usiiidanganye akili yako ukatumia macho kufikiri.[QUO

1. wale ambao ni bendera fuata upepo.
2. wale wenye malengo ya kupanda haraka na kwa urahisi kwenye arena za
kisiasa za kitaifa.

Nitayachambua makundi haya mawili kama ifuatavyo:

1. Wale ambao ni bendera fuata upepo. Katika kundi hili kuna watu wa
aina tatu:

i) Wale ambao wamedanganyika na propaganda kuwa chadema ni chama cha
kikabila au cha kikanda na kwa vile wao wanatoka kwenye kanda hizo basi
wanajisikia ukaribu zaidi na chadema. Hapa utaona kuwa propaganda za
kukichafua chama kuwa ni cha kikabila au cha kikanda kimeweza
kuwaongezea chadema nguvu katika maeneo inayoshutumiwa kuyapendelea.

ii)Wale ambao wamelaghaika na propaganda za kuwa chadema ni chama cha
udini. Kuna waumini wengi wameviunga mkono vyama vya chadema na CUF kwa
sababu tu wamekuwa wakisikia kuwa vyama hivyo vinashabiiana na dini zao.
Hawa ni bendera fuata upepo ambao hawachuji ukweli wa taarifa na
hawajiulizi chama kinaweza kuwanufaishi vipi kama waumini wa dini
husika.

iii)Kundi la tatu katika bendera fuata upepo ni vijana ambao wanaona
kuwa chadema ni kama fashion. Ukikaa nao chini vijana hawa kuwauliza
kwanini wanaiunga mkono chadema hawana lolote la kuongea. Mfano wa watu
waliomo kwenye kundi hili ni members wa jamiiforums ambao hurusha matusi
kwa kila mtu anayehoji jambo juu ya chadema.

Makundi haya matatu ya bendera fuata upepo huwa ni rahisi sana kuvunjwa
moyo na kukikimbia chama mara tu upepo utakapoelekea upande tofauti. Kwa
mfano, iwapo chadema itafanya jitihada za kuhakikisha jamii inajua
ukweli kuwa siyo chama cha ukanda wala ukabila, basi makundi haya mawili
i) na ii) yatatoweka.
Vilevile iwapo chadema itasambaza elimu ya uraia na kuwawezesha wananchi
kuchagua vyama vyama vya kuviunga mkono kwa hoja, basi makundi yote
iii),ii) na i) itayapoteza.
Hizi ni changamoto zinazohitaji political calculations kudeal nazo.

2. Wale wenye malengo ya kupanda haraka na kwa urahisi kwenye arena za
kisiasa za kitaifa:
Katika kundi hili wamo wanasiasa kama Dr. Wilbroad Slaa na Shibuda.
Misingi ya wanasiasa wa aina hii kuhama kutoka kwenye chama kimoja mpaka
kingine ni kuhakikisha tu kuwa wanaendelea kuwepo kwenye shughuli za
kisiasa katika nafasi za uongozi. Hawana ugomvi wa kiitikadi na CCM.

Kimsingi hawa ni watu ambao iwapo leo hii CCM itawahakikishia kuwa
watapata fursa ya kuwa viongozi wa juu, basi wako tayari kujiunga nayo.
Wamejitoa CCM kwa sababu tu walinyimwa fursa ya kuwa viongozi katika
ngazi walizogombea. Iwapo chadema itawanyima fursa ya kuwa viongozi,
wataikimbia pia.
Mfano mzuri umeonekana hivi karibuni Lushoto ambaye kijana mpya katika
siasa
Deogratius
Kisandu
aliikimbia chadema kwa kukosa fursa za uongozi ambapo
kimsingi alijiunga chadema kwa kuamini kuwa fursa hizo atazipata kwa
urahisi zaidi ndani ya chama hicho.

CHADEMA imekosa uungwaji mkono katika misingi ya itikadi. Hii
imesababishwa na ukweli kwamba cHADEMA imechukua itikadi zilezile za
CCM, TANU na ASP na kushindwa kuwapa wananchi chaguo jipya. Zaidi ya
hayo, hata kwenye ilani za uchaguzi za chadema hakuna offer tofauti na
zile ambazo wananchi wanapewa na CCM. Kuthibitisha hili, chadema imepata
wakati mgumu sana kupokelewa katika maeneo ambayo kuna chama kingine
cha upinzani kilichojijenga kama Zanzibar. Iwapo chadema wangekuwa na
itikadi au sera mpya ambazo utekelezaji wake unaelezeka, isingekuwa
vigumu kupata wafuasi katika maeneo hayo.

Kwa vile CCM imeshapewa fursa ya kutawala, mapungufu yake yameonekana.
Jukumu la chadema kwenye hili linatakiwa ni kuja na mkakati unaoelezea
kwa undani ni vipi watafanya tofauti na CCM. Badala yake, kazi pekee
inayofanywa na chadema ni kuainisha matatizo na kuyahubiri majukwaani
bila kuelezea iwapo wana mkakati wowote mpya ili wananchi waupime. Hii
inasababisha hata wasomi wanapovifananisha hivi vyama wanakosa zile
tofauti za kuzijadili na mwishowe hujadili tabia za viongozi vya vyama
na utendaji wao badala ya kujadili sera zake na itikadi.


Ulaghai wa CHADEMA ni sababu nyingine iliyofanya chama hiki kupoteza
wafuasi makini. Mtu yeyote atakayejaribu kuichunguza chadema kidogo tu
atagundua kuna mambo mengi yasiyofaa yanayofanywa na viongozi wake.
Viongozi hawa hufanya hivi kujinufaisha wao wenyewe na familia zao. Kwa
vile umaarufu wa chadema umetokana na uhubiri wa ufisadi, uwepo wa
ufisadi ndani ya chadema umewavunja sana moyo wananchi walioamini kuwa
wamepata tumaini jipya. Wale wanaoishabikia chadema kwa kufuata upepo
wanapojua ulaghai huu, huvunjwa moyo na kuikimbia. Mfano wa hili ni
kijana Mtela
Mwampamba
ambaye aliamini kuwa chadema ni tumaini jipya mpaka
pale alipojionea mw
 
Ze Marcopollo , Kwani wewe ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CDM ? HOJA zako ni ndefu sana lakini hazina uzito wowote ! Ni muendelezo wa zile siasa zenu za maji taka , umejidhihirisha namna ulivyojaa dharau , kwa kuwaita baadhi kwa jina la WAFUATA UPEPO Maana hawajitambui siyo ! Kwa sisi wengine tunaoifahamu kidogo afya ya binadamu tunaamini kwamba , yeyote anayedhani anafahamu mambo fulani zaidi kuliko wengine basi bila shaka ana matatizo ya akili ! Umekosea sana kwamba kilichomtoa kisandu ni tamaa ya vyeo bali kilichomtoa Mwampamba ni kujitambua ! Very poor analysis !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…