Naona Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr.W.Slaa alikuwepo anafuatilia uzi huu nadhani atakuja na neno. Akina Mwita Maranya Molemo njoo na hoja manake naona ZeMarcopolo amekuja na hoja fikirishi hapa.
Nitamshangaa Dr. kujihusisha na upuuzi ulikithiri
mshunami
Katika chapisho langu HAKUNA sehemu niliposema kuwa chadema ni chama cha kikanda au cha kidini.
Mkuu onyesha basi upuuzi wa hoja kwa hoja badala ya kusema tu kwamba ni upuuzi! Basi Molemo ama Tumaini Makene atakuja na kusema kwa niamba ya Chama na kuonyesha kwamba huo ni upuuzi.
CHADEMA ni chama kinachoendeshwa kwa misingi ya ulaghai. Chama kama hiki mtu yeyote atakayetaka kukiunga mkono kwa hoja anajikuta anakwazika.
Mkuu Fisadidagaa msamehe huyu ZeMarcopolo yuko possessedZe marcopololozigo!
Soma uzezeta wako kundi Namba 1 kipengele kidogo (i)na (ii),ukidanganya kumbuka.
Mkuu toa pia ushauri nini kifanyike ili CHADEMA wawe kama CCM.
Nikukumbushe kuwa ukiona vyaelea vimeundwa,Muda mwingi wa viongozi wa CDM umeelekezwa kwenye kukemea rushwa na kutoa elimu ya uraia.CHADEMA inamaanisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo,hivi sasa, watanzania wengi wana uelewa wa kutosha juu ya haki zao, Taifa lao linahitaji nini na ni aina gani ya chama kinaweza kuwaletea Tanzania waitakayo.Misingi ya haki haiwezi kusimamiwa na chama kinachoendeshwa kama chadema.
Je, kufuta matokeo ya uchaguzi uliompitisha mwenyekiti wa baraza la wanawake kuwa mbunge wa viti maalum na kumpa nafasi hiyo mkazi wa Marekani ndio misingi ya haki tunayotaka?
Hivi kweli ZeMarcopolo kuna ulaghai unaoweza kuzidi huu wa kukusanya kodi kutoka kwa mtu masikini kwa kipindi cha miaka mitano alafu anashindwa kumpati hata dawa tu badala yake unampeleke tisheti, kanga na kofia?.
Vyama vyote vinavyovitwa walaghai vimelaghai nini kwa wa-Tanzania?. Njoo na hoja nyingine.
Watu tunaviunga mkono vyama pinzani baada ya kulaghaiwa na walio na jukumu la kututumikia, lakini wanatumikia matumbo yao na kutugeuza sisi ngazi za mafanikio yao.
Kwa staili hii tuna safari ndefu sana.Mwenyezi Mungu shusha roho za ufahamu kwa waja wako wanaangamia kwa kukosa maarifa.Na kwa taarifa yako sina maslahi na chama chochote kile cha siasa naishi kwa jasho langu tena kwa jembe la mkono na ufugaji mdogo mdogo huku kijijini kusini mwa nchi.Ila nasikitishwa sana na baadhi ya vijana wasomi kama nyinyi ambao tunawategemea mtukomboe kutoka kwenye lindi kubwa la umaskini na ujinga tulionao kwa jinsi mnavyojiingiza kwenye siasa za majitaka na za kipuuzi.Wengi wenu mmejaaa tamaa za utajiri wa haraka na uchu wa madaraka HAMNA JIPYA.Lazima tuwapigie kelele mbadilike hatuwezi kuvumilia mkifanya ujinga wenu kupitia migongo ya vyama vya siasa.Njooni porini mjifunze maisha halisi ya Mtanzania na sio kubwabwaja tu hovyo hovyo.Msalimie Shigela na Nape hapo lumumba.
Namuomba mungu aniepushe na lugha chafu ( ma2si ) kwakua wazee wangu wamenilea ktk misingi ya heshima napenda kuheshimu na kuheshimiwa. Ila sikatazi mtu akiamua kunitusi.Niamini kweli we ni Kitoabu kitu kinachopendwa sana na warabu na huliwa gizani hasa kipindi cha baridi.