Chama cha Kilaghai Tanzania...

Chama cha Kilaghai Tanzania...

Nafikiri uko sawa kabisa na hasa ukiangalia jinsi Chadema wanavyouwa watu kama hapa Mwangozi anavyouawa.

Usiingie huko maana siku wakikugeukia kama Kolimba, itakula kwako. Chezea Chadema wewe.

mwangosi_tanzania_misatanzania_468.jpg
 
hiki chama cha majambazi. kila mmoja anatakiwa wakae mbali nacho. kama kimeanza kuteka na kudhuru watu hakijafika ikulu kikijakufika hali itakuwaje? mungu atuepushie mbali na hili janga liitwalo chadema.
 
Lengo la sisiemu ni kuimaliza nguvu CHADEMA, kila simu mnatengeneza kashfa, lakini hamjui ndio mnajimaliza nguvu wenyewe......Wananchi ndio wanazidi kufunguka kwa uhuni wenu mnaofanya.
 
hiki chama cha majambazi. kila mmoja anatakiwa wakae mbali nacho. kama kimeanza kuteka na kudhuru watu hakijafika ikulu kikijakufika hali itakuwaje? mungu atuepushie mbali na hili janga liitwalo chadema.

Ati??? Chama Cha Majambazi unaita CHADEMA...kumbe hamjui ndio kirefu cha jina la CCM...inaonekana we ni bendera fuata upepo, huijui ccm yako...jambazi mwenyewe
 
Ati??? Chama Cha Majambazi unaita CHADEMA...kumbe hamjui ndio kirefu cha jina la CCM...inaonekana we ni bendera fuata upepo, huijui ccm yako...jambazi mwenyewe
mkurugezi wa usalama aka utekaji amepanga kwenda kumteka nani baada ya kibanda?
 
Ni wakati muafaka wa viongozi wakuu wa cdm kutoa tamko kujisafisha dhidi ya hii mbinu chafu ya ccm.na isiwe kwa majibu mepesi.
 
mkurugezi wa usalama aka utekaji amepanga kwenda kumteka nani baada ya kibanda?

Technic hii ya magamba ni ya Kichina haiuziki sokoni. Yaani mnatengeneza video na Polisi wenu nao wanakimbia kumkamata mtu. mwigulu alisema ana huo mkanda mlimhoji. Mmesubiri mmemtaka kibanda ndo mnaleta huu upuuzi wenu. Hii kama ni movie basi stearing amekufa. Sasa cjui hapo deck ndo mbovu!
 
hiki chama cha majambazi. kila mmoja anatakiwa wakae mbali nacho. kama kimeanza kuteka na kudhuru watu hakijafika ikulu kikijakufika hali itakuwaje? mungu atuepushie mbali na hili janga liitwalo chadema.

Mkuu wakati una post ulikuwa lindo la wapi leo na muda huu wa saa 9 sio mzuri kabisa usingiz ndio unakuwanga mtam.... pole sanaaa nenda sasa kalale vizur.
 
Na wewe usiyeitambua ccm ulishaingia mkenge siku nyingi sana,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
 
Ati??? Chama Cha Majambazi unaita CHADEMA...kumbe hamjui ndio kirefu cha jina la CCM...inaonekana we ni bendera fuata upepo, huijui ccm yako...jambazi mwenyewe
hata wale polisi wanaoonekana wamemzunguka Marehem Mwangosi ni polisi wa chadema. kweli ccm wameishiwa hila
 
Walioua watu Arusha kwa risasi,kumteka Ulimboka ni Chadema..ama kweli magamba mnatufanya wa Ngumbaru
 
Mazombi ebu acheni ku2tafutia ban.M2 mzima unayejiita baba unakuja na u2mbo huu nataman ukapime DNA n wtt wako
 
Hivi CDM Ni tatizo kubwa kuliko matatizo tuliyonayo Tanzania? CCM Ndio Tatizo na matatizo ya Watanzania, CCM Imeshindwa kuondoa matatizo ya msingi ya Watanzania, na tukitaka kuwa Wazalendo wa kweli tusijadili vyama, bali tujadili matatizo ya msingi ya nchi na tuje na majibu ya namna ya kushughulika nayo. Kimsingi huwezi kulinganisha madudu ya CDM na CCM,
CCM Wanatawala, CDM ni chama Pinzani, Katika mazingira ya Sasa hakuna namna amabayo unaweza kusimamisha kasi ya chama kama CDM, Kwa kuwa sehemu kubwa ya Watanzania wanajua kuwa CCM limekuwa ni Genge la watu fulani amabao wanataka ku-maintain Status Quo.
Watanzania wanayo macho,Wanaona jinsi Watawala wanavyopigana vikumbo kuakikisha kuwa wanaweka watoto wao, ndugu na jamaa zao katika nafasi za kisiasa na kitendaji ili waendelea kumiliki mfumo huu mbovu, Kwao Tishio kubwa ni Chama kama CDM, Kwanini ? kwasababu wameshapiga mahesabu na kuona kuwa CDM Ikitawala Fate yao ni mbaya. Watakimbilia wapi na mali waliyojilimbikizia?

Kwahiyo kwa gharama yoyote watahakikisha kuwa CDM Inapotea.Kwa hiyo udhaifu mdogo uliopo ndani ya CDM Utatumiwa kuposha ukweli,Ili CDM Kionekana kuwa chama kisichofaa, kwanini sio TLP,CUF, au NCCR? Wanajua hawa wanachokitaka CDM, Kuweni makini.

Kwa upande wa CDM, CDM Lazima ijisafishe kama kweli inataka kuwa chama cha Watanzania wanyonge ambao wanaipenda nchi yao,na wako tayari kuona inakombolewa na kuwa huru kutoka mikononi mwa wanaCCM Wabadhirifu.
Mtu mwenye akilli Timamu hawezi kushambulia Chadema kwa kutumia Mfano wa Watu wawili kuonyesha matatizo ya CDM.
 
CHADEMA ni chama kinachoendeshwa kwa misingi ya ulaghai. Chama kama hiki mtu yeyote atakayetaka kukiunga mkono kwa hoja anajikuta anakwazika.
Hii imesababisha CHADEMA kuungwa mkono zaidi na makundi mawili ya watanzania:

1. wale ambao ni bendera fuata upepo.
2. wale wenye malengo ya kupanda haraka na kwa urahisi kwenye arena za kisiasa za kitaifa.

Nitayachambua makundi haya mawili kama ifuatavyo:

1. Wale ambao ni bendera fuata upepo. Katika kundi hili kuna watu wa aina tatu:

i) Wale ambao wamedanganyika na propaganda kuwa chadema ni chama cha kikabila au cha kikanda na kwa vile wao wanatoka kwenye kanda hizo basi wanajisikia ukaribu zaidi na chadema. Hapa utaona kuwa propaganda za kukichafua chama kuwa ni cha kikabila au cha kikanda kimeweza kuwaongezea chadema nguvu katika maeneo inayoshutumiwa kuyapendelea.

ii)Wale ambao wamelaghaika na propaganda za kuwa chadema ni chama cha udini. Kuna waumini wengi wameviunga mkono vyama vya chadema na CUF kwa sababu tu wamekuwa wakisikia kuwa vyama hivyo vinashabiiana na dini zao. Hawa ni bendera fuata upepo ambao hawachuji ukweli wa taarifa na hawajiulizi chama kinaweza kuwanufaishi vipi kama waumini wa dini husika.

iii)Kundi la tatu katika bendera fuata upepo ni vijana ambao wanaona kuwa chadema ni kama fashion. Ukikaa nao chini vijana hawa kuwauliza kwanini wanaiunga mkono chadema hawana lolote la kuongea. Mfano wa watu waliomo kwenye kundi hili ni members wa jamiiforums ambao hurusha matusi kwa kila mtu anayehoji jambo juu ya chadema.

Makundi haya matatu ya bendera fuata upepo huwa ni rahisi sana kuvunjwa moyo na kukikimbia chama mara tu upepo utakapoelekea upande tofauti. Kwa mfano, iwapo chadema itafanya jitihada za kuhakikisha jamii inajua ukweli kuwa siyo chama cha ukanda wala ukabila, basi makundi haya mawili i) na ii) yatatoweka.
Vilevile iwapo chadema itasambaza elimu ya uraia na kuwawezesha wananchi kuchagua vyama vyama vya kuviunga mkono kwa hoja, basi makundi yote iii),ii) na i) itayapoteza.
Hizi ni changamoto zinazohitaji political calculations kudeal nazo.

2. Wale wenye malengo ya kupanda haraka na kwa urahisi kwenye arena za kisiasa za kitaifa:
Katika kundi hili wamo wanasiasa kama Dr. Wilbroad Slaa na Shibuda. Misingi ya wanasiasa wa aina hii kuhama kutoka kwenye chama kimoja mpaka kingine ni kuhakikisha tu kuwa wanaendelea kuwepo kwenye shughuli za kisiasa katika nafasi za uongozi. Hawana ugomvi wa kiitikadi na CCM.

Kimsingi hawa ni watu ambao iwapo leo hii CCM itawahakikishia kuwa watapata fursa ya kuwa viongozi wa juu, basi wako tayari kujiunga nayo. Wamejitoa CCM kwa sababu tu walinyimwa fursa ya kuwa viongozi katika ngazi walizogombea. Iwapo chadema itawanyima fursa ya kuwa viongozi, wataikimbia pia.
Mfano mzuri umeonekana hivi karibuni Lushoto ambaye kijana mpya katika siasa Deogratius Kisandu aliikimbia chadema kwa kukosa fursa za uongozi ambapo kimsingi alijiunga chadema kwa kuamini kuwa fursa hizo atazipata kwa urahisi zaidi ndani ya chama hicho.

CHADEMA imekosa uungwaji mkono katika misingi ya itikadi. Hii imesababishwa na ukweli kwamba cHADEMA imechukua itikadi zilezile za CCM, TANU na ASP na kushindwa kuwapa wananchi chaguo jipya. Zaidi ya hayo, hata kwenye ilani za uchaguzi za chadema hakuna offer tofauti na zile ambazo wananchi wanapewa na CCM. Kuthibitisha hili, chadema imepata wakati mgumu sana kupokelewa katika maeneo ambayo kuna chama kingine cha upinzani kilichojijenga kama Zanzibar. Iwapo chadema wangekuwa na itikadi au sera mpya ambazo utekelezaji wake unaelezeka, isingekuwa vigumu kupata wafuasi katika maeneo hayo.

Kwa vile CCM imeshapewa fursa ya kutawala, mapungufu yake yameonekana. Jukumu la chadema kwenye hili linatakiwa ni kuja na mkakati unaoelezea kwa undani ni vipi watafanya tofauti na CCM. Badala yake, kazi pekee inayofanywa na chadema ni kuainisha matatizo na kuyahubiri majukwaani bila kuelezea iwapo wana mkakati wowote mpya ili wananchi waupime. Hii inasababisha hata wasomi wanapovifananisha hivi vyama wanakosa zile tofauti za kuzijadili na mwishowe hujadili tabia za viongozi vya vyama na utendaji wao badala ya kujadili sera zake na itikadi.


Ulaghai wa CHADEMA ni sababu nyingine iliyofanya chama hiki kupoteza wafuasi makini. Mtu yeyote atakayejaribu kuichunguza chadema kidogo tu atagundua kuna mambo mengi yasiyofaa yanayofanywa na viongozi wake. Viongozi hawa hufanya hivi kujinufaisha wao wenyewe na familia zao. Kwa vile umaarufu wa chadema umetokana na uhubiri wa ufisadi, uwepo wa ufisadi ndani ya chadema umewavunja sana moyo wananchi walioamini kuwa wamepata tumaini jipya. Wale wanaoishabikia chadema kwa kufuata upepo wanapojua ulaghai huu, huvunjwa moyo na kuikimbia. Mfano wa hili ni kijana Mtela Mwampamba ambaye aliamini kuwa chadema ni tumaini jipya mpaka pale alipojionea mwenyewe kwa macho yake uhalisia wa mambo ndani ya chama hicho.

Hapa nitaainisha baadhi ya mambo yanayoiondoa CHADEMA usoni na moyoni mwa watanzania wanaotaka chama kinachopinga ufisadi.
1. Mmiliki wa jengo lililopangishwa na CHADEMA Kinondoni kama ofisi za makao makuu na bei ya pango kwa mwezi vimefanywa siri. Mara kadhaa swali hili limeibuliwa lakini hakuna jibu lililoweza kutolewa na uongozi wa CHADEMA.

2. Wanachama walioomba fursa ya kushiriki tenda ya kununua magari ya chama wamenyimwa fursa hiyo na hatimaye tenda hiyo imetolewa kwa usiri mkubwa. Chris Lukosi amekuwa akishutumiwa kuwa sababu ya kujitoa kwake CHADEMA ni kunyimwa tenda hii, lakini pale wadau walipohoji baada ya Lukosi kunyimwa tenda hiyo ni nani amepewa na kwa vigezo vipi?, kinaibuka kigugumizi.

3. Swala la Katibu Mkuu wa chama kujikopesha mamilioni ya shilingi zilizochangwa na walalahoi kwa ajili ya shughuli za chama. Ikumbukwe kuwa watu waliochangia M4C walifanya hivyo kwa vile waliamini kuwa michango yao itakiwezesha chama kujiimarisha. Taarifa kuwa pesa zimetumika kifisadi zimewavunja watu moyo.

4. Taarifa za Josephine Mushumbusi kulipwa mamilioni ya shilingi za chama kwa kazi anayoiita ya kujitolea. Wadau walihoji kuwa na wao wangependa kujitolea kwenye shughuli za chama ili walipwe hayo mamilioni. Ilidhihirika kuwa Josephine alipata fursa hiyo kwa upendeleo.

5. Pesa za ruzuku zimekuwa zikiishia Makao Makuu. Watendaji wa chama mawilayani wamekuwa wakifanya kazi bila nyenzo. Hii ilisababisha mpaka kukawa na mtafaruku huko Mpanda kwa kukosa ofisi ya wilaya ambayo kimsingi ni jukumu la chama makao makuu kuhakikisha chama kina ofisi za wilaya. Ikumbukwe pia kuwa matumizi haya mabaya ya fedha yalikuwa sababu ya mvutano wa kisiasa kati ya marehemu Chacha Wangwe na kiongozi Mkuu wa Chama.

6. Kumekuwa na taarifa za matumizi mabaya ya pesa za Sabodo jambo ambalo limeelezewa kuwa sababu ya kumfanya Sabado kuahirisha ahadi yake ya kuijengea CHADEMA ofisi za makao makuu na chuo cha siasa.

7. Katibu Mkuu wa CHADEMA ni miongoni mwa washutumiwa wa ufisadi wa mamilioni ya pesa za mradi wa maji wa Karatu.

8. Viti Maalum vya ubunge vimetolewa kwa upendeleo ambapo akinamama waliojitolea kukijenga chama wameachwa pembeni na nafasi hizo kupewa akinamama walio karibu na viongozi wa juu wa chama. Hapa ikumbukwe kuwa mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA) wa Taifa alishinda nafasi ya uchaguzi wa viti maalum, lakini akatolewa kwa kuambiwa kuwa hajakidhi vigezo vya kuwa mbunge ingawa amewaongoza wanawake wenzake kwa muda mrefu ndani ya chadema. Wakati huohuo mwanamama anayeishi Marekani, Leticia Nyerere amepewa Ubunge wa viti maalum kutokana na "kufahamiana" na mwenyekiti wa chama. Hili limewavunja moyo wengi walioanza kuiamini chadema.

9. Vijana kama Kafulila walioonekana kuwa na ari ya mabadiliko ndani ya chama wamekuwa wakinyimwa nafasi ya kugombea uongozi kinyume na katiba.

10. CHADEMA kukanusha kauli ya Nape kuwa wanapewa msaada na chama cha siasa cha Ujerumani, baadae ikadhihirika kuwa ni kweli wanapokea msaada huo. Hii imedhihirisha kuwa CHADEMA sio wawazi katika utendaji wao. Wadau wanajiuliza chama hicho cha siasa kinataka nini Tanzania mpaka kikipinge chama kilichoasisiwa na wapigania Uhuru na kutaka chadema iingie madarakani? Ikumbukwe kuwa muasisi wa CHADEMA Mzee Mtei, alikataa kushiriki harakati za kupigania uhuru na pia alikataa kujitolea kuijenga nchi baada ya Uhuru.

11. Hesabu za pesa zinazochangwa na walalahoi kwa ajili ya M4C imekuwa ni jambo la siri kubwa ndani ya CHADEMA.

Wewe sema utaloweza sisi hatuiachi hii Chama imeleta mambo makubwa kwa watanzania na watanzania wamekubali sana.
 
muda wote huo unatumika kuwahadaa watanzania kwamba leo sasa CDM ni chama cha kigaidi? Sina uhakika haya mengine mliyoyahusisha nacho mmeyafuta?
a) Mlikuja na UDINI (CDM mali ya Wakatoriki)
b) Mkaja na UKABILA (CDM mali ya wachaga)

Sasa hii kasi ya CDM kwenda hadi vijijini -- kuweka sera ya Majimbo na nyie kwa badala ya kuja na majibu kama chama tawala sasa mmekuja na UGAIDI wa CDM. (CDM imeanza mikakati ya kuua / Kutesa wanahabari)

Poleni sana, hii nchi ni mali ya watanzania wenyewe na amini usiamini ni vigumu sana kwa sasa kuwabadilisha wananchi wa Tanzania waliochoka na maisha kwa kutumia hizi propaganda zilizokufa.
 
Back
Top Bottom