Chama cha ECONIMIC FREEDOM FIGHTERS(EFF)

Chama cha ECONIMIC FREEDOM FIGHTERS(EFF)

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
27,743
Reaction score
63,010
EFF: ECONIMIC FREEDOM FIGHTERS

EFF Ni Chama cha Siasa cha tatu kwa Ukubwa nyuma ya Vyama Vikongwe DA(Democratic Alliance) na ANC(African National Congress) ambacho ni Chama cha Siasa kikongwe zaidi nchini Afrika Kusini.

EFF kiliundwa Tarehe 28/7/2013.Miaka mitatu(3) iliyopita,chini ya Rais na Amiri Jeshi mkuu(President and Commander In Chief,CIC) Comrade JULIUS SELLO MALEMA,Alimaarufu kama JUJU na Viongozi wengine kadhaa waliokihama Chama kikongwe ANC.

CIC,JULIUS MALEMA alikua Kiongozi wa Tawi la Vijana la ANC Kitaifa,ANC-Youth League mpaka alipojitoa ANC na Kuunda Chama Kipya cha Siasa EFF mwaka 2013 Baada ya kutofautiana na Rais JACOB ZUMA na wana ANC wengine alipoonekana ni tishio kwa Rais ZUMA na wana ANC wengine km Makamu Rais CYRIL RAMAPHOSA kwani alihatarisha nafasi zao Siku za usoni alipoonekana kujijengea uungwaji mkono mkubwa Ndani na nje ya Chana hicho.

EFF ni Chama kilichopata Uungwaji mkono mkubwa ndani ya Muda mfupi,Kwani ktk Uchaguzi mkuu wa Afrika Kusini mwaka 2014,mwaka mmoja tu tangu kuundwa kwake kilikua tishio kwa ANC na DA,kwani ktk Uchaguzi mkuu ule kilipata Viti vya UBUNGE Ishirini na tano(25) kikiwa nyuma ya ANC na DA kwa wingi wa Wabunge Bungeni.

Pamoja na Kuwa na na Wabunge 25 kati ya Wabunge 400 wa Bunge la Afrika Kusini,EFF na Wabunge wametikisa Bunge la Afrika Kusini na Serikali ya ANC. kwa kuendesha Vuguvugu mbalimbali km
#ZUMA must fall,

#Guptas must Go,

#Marikana massacre movement,

#Nkandla.Ambapo kampeni zilikua dhidi ya Ubadhilifu wa Rais zuma kujenga makazi Binafsi NKANDLA-Kwa Zulu Natal kwa pesa ya Umma,Mauaji ya Wachimbaji wa Mgodi wa MARIKANA zaidi ya 30 waliopigwa Risasi na Polisi chini ya Maelekezo ya Makamu Rais CYRILL RAMAPHOSA na Kufunguliwa kwa Kesi dhidi ya Rais Zuma ktk Mahakama ya kikatiba #Constitutional Court dhidi ya Matumizi mabaya ya fedha za umma kujenga Makazi binafsi kule Nkandla-KZN ambapo Mahakama #Concourt ilimwamuru Rais ZUMA kurejesha Fedha za Umma zilizotumika kujenga makazi yake Binafsi #Nkandla

EFF inainyima usingizi ANC,Zuma na DA pia.EFF imejikita kutetea maslahi ya Masikini wa Afrika Kusini hawa Weusi walio wengi wanaoishi km Wakimbizi ktk Nchi yao,kwa kukosa ARDHI,AJIRA,ELIMU,Huduma za Afya,Nishati n.k kwani Maeneo yote yanayokaliwa na Waafrika(Predominantly Black) mfano SOWETO kuna Umasikini wa Kutupwa.EFF ni Chama kilichojipambanua Kua Chama cha mrengo wa kushoto(Far-Left),Kinachoamini ktk Ujamaa,U marxi-U lenin(Marxist-Leninist),Umajumui wa Afrika(Pan-Africanism),U-Sankara(Sankarism) kikiongozwa na misingi ya Ujamaa na Umajumui wa Afrika uliopiganiwa na Wana wa Afrika km KWAME NKRUMAH,PATRICE EMERY LUMUMBA,THOMAS SANKARA,SAMORA MOISES MACHEL,Mwl.J.K NYERERE,AHMED SEKOU TOURE n.k

EF ni Chama KINACHONIVUTIA ZAIDI ULIMWENGU MZIMA kwa Aina ya siasa yao ktk Bara zima la Afrika na Ulimwengu kwa Ujumla,NAIPENDA EFF kwa namna Vijana wazalendo wa Afrika Kusini wakiongozwa na JULIUS MALEMA(President,CIC),FLOYD SHIVAMBU(Deputy President),DALI MPOFU(National Chairperson),Katibu Mkuu,GS(GODRICH GARDEE),Msemaji wa Chama Taifa(National Spokesperson),MBUYISENI NDLOZI walivojitoa kupigania Taifa lao.Ni vijana ktk Rika la miaka 30s-40s wanaofanya makubwa kwa Taifa siyo KULAMBA VIATU VYA WAKUBWA km Wafanyavyo Vijana WASAKA TONGE ktk Nchi yetu.

Leo hii Tarehe 03/08/2016.Wananchi wa Afrika Kusini wanaamka kwenda ktk Vituo vya Kupigia KURA kuchagua MADIWANI(Councillors) na MAMEYA(Mayors) Ktk Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Kitaifa Nchini AFRIKA KUSINI.EFF Chama chenye Umri wa Miaka 3 kinatarajiwa kufanya Vizuri sana ktk Uchaguzi huu,Kwani tangu kuzinduliwa kwa Kampeni Miezi mitatu iliyopita #EFF imepata Uungwaji mkonk mkubwa zaidi kuwahi kutokea.Tangu Siku walipozindua Kampeni zao #ORLANDO STADIUM,SOWETO mpaka Kuhitimisha Juzi wameonesha Wana Nafasi ya kufanya Mageuzi Makubwa ktk Siasa za Afrika Kusini

Nawatakia EFF ushindi mkubwa na Wananchi wa Afrika Kusini waipe Ridhas EFF na Imani itafanya makubwa kwa Wana wa AFRIKA YA KUSINI

#VoteEFF

#EFFwayawaya

#NkosiSikeliAfrika

#NaipendaEFF

Mussa Leonard Mdede.
 
Siasa za EFF zinawezekana kwa nchi yenye mfumo wa wazi kama Afrika Kusini,na angalau kwao demokrasia iko juu,Malema angekuwa Tanzania kila siku angekuwa anatolewa bungeni,NATAMANI SANA TANZANIA KUNGEKUWA NA CHAMA KAMA EFF,NINGEKUWA MFUASI WAKE MTIIFU
 
Wakati Zitto anaondoka CHADEMA nilijua anaenda kutengeneza chama radical kama EFF,na Nlikuwa nshajipanga kuzamia huko,kumbe Zitto hataki harakati anataka siasa,siasa ya upinzani bila harakati inawezekana Marekani tu
 
Back
Top Bottom