Chalamila amewaagiza watendaji wa serikali kuangalia upya utaratibu wa kuingia katika nyumba za wageni

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,753
218,366
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amewaagiza watendaji wa serikali kuangalia upya utaratibu wa kuingia katika nyumba za wageni maarufu kama gesti ikiwezekana kuwepo na vitambulisho ili kujihakikishia usalama zaidi.

Chalamila amesema hayo leo Januari 15, 2024 jijini Dar es Salaam kwenye kikao na watendaji wa Serikali kuhusu magonjwa ya mlipuko.

Amesema "Muda mwingine tembeeni hadi usiku kukagua madaftari kukagua watu waliongia, kuna vigesti vinatumika kama vichocheo vya uhalifu."

Katika hili yupo sahihi. Tunahitaji kuwa na ufuatiliaji mzuri, kuanzia serikali za mitaa mpaka ngazi ya mjumbe wa nyumba kumi. Ni muhimu sana kwaajili ya usalama wetu.
Wajumbe wa nyumba 10 hawamo ndani ya Katiba , hawa ushahidi unaonyesha kwamba wanalinda hata Wahamiaji haramu ili waipigie kura ccm
 
Yaani kama CDM mmealikana kuandamana, humohumo mnamolala mnafurumushwa, vinginevyo awe anatafutwa Joyce Mukya na mzee.
 
Katika hili yupo sahihi. Tunahitaji kuwa na ufuatiliaji mzuri, kuanzia serikali za mitaa mpaka ngazi ya mjumbe wa nyumba kumi. Ni muhimu sana kwaajili ya usalama wetu.
Ikiwezekana iwe lazima pia mtu akihama sehemu moja atoke na barua kutoka kwa mwenyekiti wa mtaa apeleke sehemu anayohamia. Asipokelewe mpaka awe na hiyo barua husika.
 
Yupo sahihi kabisa.Kuna watu hufia nyumba za kulala wageni kwa kuuwawa au vinginevyo.
Al-shabab waliofanya ugaidi Kenya kuna waliokua wakilala nyumba za wageni.
Ungeijua vizuri Nairobi usingesema hivyo, kwa taarifa yako Nairobi kuna eneo moja wanaishi wasomali, eneo hilo si gesti hausi ni makazi ya watu.
Makanisa mengi yana manabii feki toka nje ya nchi.
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amewaagiza watendaji wa serikali kuangalia upya utaratibu wa kuingia katika nyumba za wageni maarufu kama gesti ikiwezekana kuwepo na vitambulisho ili kujihakikishia usalama zaidi.

Chalamila amesema hayo leo Januari 15, 2024 jijini Dar es Salaam kwenye kikao na watendaji wa Serikali kuhusu magonjwa ya mlipuko.

Amesema "Muda mwingine tembeeni hadi usiku kukagua madaftari kukagua watu waliongia, kuna vigesti vinatumika kama vichocheo vya uhalifu."
View attachment 2873154
Ni kweli hizi issue za mauaji guest zimekuwa too much lazima utaratibu ubadilike ukiingia uache kitambulisho chako chochote ili ikitokea tatizo kama mauaji tujue pa kuanzia
 
Back
Top Bottom