Chaji Kwa Masaa 6!

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2009
Posts
16,202
Reaction score
8,787
Naomba kujuzwa.
Nimenunua battery ya simu nikaambiwa na wenye duka kuwa niichaji battery hiyo kwa masaa 6 ili idumu!
Lakini nilipoanza kuchaji baada ya masaa 2 tu ilionyesha kujaa kwa 100% na haikonyezi tena!
Je niendelee kuiacha kwenye moto hadi hayo masaa 6 yafike?...au ni ushauri wa mitishamba?
 
Hili jambo hata mimi huwa linanitatiza sana, ngoja wataalamu waje.
 
Unapaswa kuendelea kuiacha chaji hadi muda ulioshauriwa. Usijali inasemaje.
 
Unapaswa kuendelea kuiacha chaji hadi muda ulioshauriwa. Usijali inasemaje.
Sababu ninini broda?...ungetusaidia kueleza kuwa inaisaidiaje betri kuwa imara!
 
Wataalam wanasema kwa lugha ya malkia kuwa kufanya hivyo ni ku- condition the battery, kwa kuwa ndio mara ya kwanza kujazwa chaji.
 
Wataalam wanasema kwa lugha ya malkia kuwa kufanya hivyo ni ku- condition the battery, kwa kuwa ndio mara ya kwanza kujazwa chaji.
Well, huenda hapa kukawa na ukweli!
Lakini nijuavyo mimi battery huwa na chaji japo kiasi fulani tokea inaponunuliwa!
 
mimi mwenyewe siamini ktk hili. betri ikijaa hakuna haja ya kuendelea kuichaji. betri original hata usipo ichaji masaa sita bado itaendelea kuwa ngumu. kwa nini tukinunua laptop hatuchaji masaa sita? tatizo ni vibetri vya kichina hivyo wauzaji wanatafuta sababu pindi uendapo kulalamika. hiyo betri kama ni mbovu hata uchaji masaa kumi itaendelea kwisha fasta
 
Well, huenda hapa kukawa na ukweli!
Lakini nijuavyo mimi battery huwa na chaji japo kiasi fulani tokea inaponunuliwa!

Ni kweli PJ Battery huwa na chaji kiasi kuiwezesha kuanza kupokea chaji, sasa ukinunua ndio unaanza rasmi kuizoesha utamaduni wa kuwa na chaji full itakayotumika. Hujawahi kuishiwa kabisa chaji kwenye Battery mafundi huunganisha waya moja kwa moja waya kwenye contact terminal za Battery ili ku boost iweze ku chaji, la sivyo ukiweka chaji kawaida hukataa kabisa.
 
amna mkuu huo ni uongo mbona laptop hatu condition battery

Mfuatilie AK-47 utajifunza kitu mkuu...........

Batteries Care Instructions

Battery Do's:

A new battery comes in a discharged condition and must be charged before use (refer to the devices manual for charging instructions). Upon initial use (or after a prolonged storage period) the battery may require three to four charge/discharge cycles before achieving maximum capacity.


When charging the battery for the first time the device may indicate that charging is complete after just 10 or 15 minutes. This is a normal phenomenon with rechargeable batteries. Remove the battery from the device, reinsert it and repeat the charging procedure.


It is important to condition (fully discharge and then fully charge) the battery every two to three weeks. Failure to do so may significantly shorten the battery's life (this does not apply to Li-Ion batteries, which do not require conditioning). To discharge, simply run the device under the battery's power until it shuts down or until you get a low battery warning. Then recharge the battery as instructed in the user's manual.


If the battery will not be in use for a month or longer, it is recommended that it be removed from the device and stored in a cool, dry, clean place.


It is normal for a battery to become warm to the touch during charging and discharging.


A charged battery will eventually lose its charge if unused. It may therefore be necessary to recharge the battery after a storage period.


The milliamp-hour (mAH) rating of the Hi-Capacity battery will often be higher than the one on the original battery. A higher mAH rating is indicative of a longer lasting (higher capacity) battery and will not cause any incompatibilities. A Hi-Capacity battery will, in most cases, outperform the original by 30% to 50%.


Actual battery run-time depends upon the power demands made by the equipment. In the case of notebook computers, screen brightness, the use of the CPU, the hard drive, and other peripherals results in an additional drain upon the battery, effectively reducing the battery's run-time. The total run-time of the battery is also heavily dependent upon the design of the equipment. To ensure maximum performance of the battery, optimize the computer's power management features. Refer to the computer manual for further instructions.
 
Last edited by a moderator:

Umeuliza kitu cha maana mkuu, user manual huwa zinasemaje?
 
mkuuu haya mambo lazima uwe unafikiria mtu anayekuuzia elimu yake darasa la 7 hajui chochote kuhusu technolojia anakudanganya kachaji masaa sita na wewe unamuamini!???? we chaji betri ikijaa chomoa chaja anza kutumia!!! kibaya ni kutumia kabla hujaichaji kwa mara ya kwanza hapo kweli itakufa mapema vinginevyo walikudanganya
 
nimeipenda hii mada nimetafuta resource mbali mbali online nimepata hitimisho hili.

unatakiwa kuiacha battery masaa 2 au matatu zaidi pale inapojaa chaji ili kupata battery itayodumu zaidi. kama battery itajaa masaa 2 unatakiwa uiache masaa mengine mawili au matatu. ina maana battery kwa mara ya kwanza huchajiwa masaa 5 au 4. na ndio hapa hizo habari za masaa 6 zinapoanzia.

tusielewe kwa kufata mkumbo hebu tujiulize kuna hekima gani kuiacha battery kwa muda huo?

kwenye simu kuna sensor ambayo kazi yake ni kutoa taarifa kua sasa battery imejaa au ipo nusu au imeisha.

kakini hii sensor haijui ni kiasi gani cha chaji kipo kwenye battery inachofanya yenyewe ni kutumia mazoea kua baada ya masaa mawili battery inakua full. na pia inaeka rekodi kua battery inatumika hivi kwa hio baada ya matumizi haya itakua imeisha.

hivyo kutokana na tabia ya hio sensor kutokua na akili ya kuijua battery vizuri inaweza ikakwambia ipo full kumbe battery haipo full hivyo makampuni yanayotengeneza battery yakaamua kueka huo muda wa masaa 6 ili kuiwezesha hii sensor kuijua vizuri battery.

ina maana baada ya kuchaji mara ya 1 sensor itakua na taarifa zote za battery na haitakosea tena. ukichaji mara ya pili itakupa taarifa sahihi. kuanzia chaji ya pili na kuendelea ndio battery ikiandika full chomoa chaja, ila mara ya kwanza usiifatilize simu chaji masaa 4 hadi 6.

kwa wale wanaopenda kujisomea zaidi kuna link hizi hapa.

hawa ni seido watengeneza battery shuka chini utaona maneno mekundu ya msisitizo

SEIDIO | Innocell 3500mAh Extended Life Battery for HTC Shift 4G

pia nikapAta na habari ya nyongeza unatakiwa usiache battery ikaisha charge kabisa ikiwa hata na chaji nusu we ijaze.

battery hizi za lithium zinadumu mizunguko 300 hadi 500 pale inapoisha kabisa lakini ukiwah kabla haijaisha ina maana itakaa sana.

NOTE; BATTERY ZINAZOZUNGUMZIWA HAPA NI ZA LITHIUM TU AMBAZO NDO HUPATIKANA SIMU NYINGI. BATTERY NYENGINE KAMA CADMIUM HAZINA MASHART KAMA HAYA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…