Chain Of Command: Dkt. Mpango hajui mipaka yake

Chain Of Command: Dkt. Mpango hajui mipaka yake

Waacheni wasaidiane kuongoza nchi si kazi ndogo.

ndio maana Katiba inatakiwa kuwa reviewed.
 
Kinachoshindwa kueleweka ni ukweli kuwa makamu wa rais ni rais msaidizi. Anafanya kazi kadri ya maagizo ya rais. Anapotoa maagizo mbele ya umma anafanya hivyo kwa makubaliano kati yake na bosi wake.

Ndio maana Rais kule Dodoma akiongea na viongozi wa dini akasema yeye na hayati JPM ni kitu kimoja. Wote ni washirika wa cheo cha urais.

Mleta mada kakariri maana ya jumla ya makamu wa rais.

Hakika.

Na Rais akimuagiza VP wake kufanya kazi yoyote ile au kufuatilia jambo lolote lile, hautangazii ulimwengu kuwa amefanya hivyo!
 
Nadhani siku anamuapisha kasema pamoja na majukumu yake ya kikatiba lakini anamtaka akamsaidie katika ukusanyaji wa mapato na kubana matumizi ya serikali ingekuwa ushauri tu wala asingesema ila kampa majukumu nje majukumu ya kikatiba.
Heija,
Nakuelewa vema hata mimi niliisikia hiyo kauli ya mama na niwazi kuwa mama anatarajia ushauri wa Mpango linapokuja swala la kifedha na uchumi ila kwakua mama bado hajamahishia docket ya wizara ya Fedha katika ofisi ya VP naamini ushauri wa VP unatarajiwa kuwa behind the closed door na sio otherwise.
 
Mdogo mdogo ataelewa, hakuwai tegemea cheo Kama Cha Sasa , viongonzi huandaliwa,ila pia ni kipaji that's tumeona alichokifanya mh Makongoro wakati anaapishwa WATU wanashangaa na kuponda kwamba ni maigizo,ila ukweli Makongoro ni kiongozi na hakutakiwa kuwa pale maana anajua nini afanye wakati gani mda gani uliosahii, ukimfuatilia tangu Kipindi Cha kutia nia 2015, Kama ni mapungufu mengine basi ni yale tu ya kibinadam ,but yupo smart sana
Makongoro yuko smart?

Kweli akili ni nywele na kila mtu ana zake.
 
Kinachoshindwa kueleweka ni ukweli kuwa makamu wa rais ni rais msaidizi. Anafanya kazi kadri ya maagizo ya rais. Anapotoa maagizo mbele ya umma anafanya hivyo kwa makubaliano kati yake na bosi wake.

Ndio maana Rais kule Dodoma akiongea na viongozi wa dini akasema yeye na hayati JPM ni kitu kimoja. Wote ni washirika wa cheo cha urais.

Mleta mada kakariri maana ya jumla ya makamu wa rais.
JK aliwahi kusema urais ni wangu na sina ushirika na mtu yoyote yule.
 
Asaidie kumshauri lakini sio kusimama hadharani na kutoa maagizo na maelekezo yanayopaswa kutolewa na Rais tena akiwa hai mwenye afya na yupo nchini. Mkuu unadhani Mamlaka ya Rais na Makamu wa Rais yako sawa? La hasha, Kikatiba VP hayuko kabisa kwenye Chain of Command ya Utendaji wa Kila Siku wa Serikali. Yeye kapewa Majukumu ya Kumsaidia Rais kwenye Mazingira na Muungano. Pia kumshauri President kwenye kutenda. labda kama tunahitaji kuibadili katiba na kumuongeza VP kwenye utendaji basi sawa, tubadili Katiba kwanza.
Duh tungeisoma hiyo sehemu ya Makamu wa Rais tungejua km ni kweli haruhusiwi kusema lolote mpaka Rais
Mimi nijuavyo bado ana Mamlaka ya kutoa amri za kazi pasipo kusubiri Rais
Mfano juzi kawaambia Wakuu wa Mikoa waache ULEVI,UZINZI na kujifanya vinuri
na kwa vile Bara anapajua kuliko Mama yeye ndiye mshauri Mkuu wa Seriklali huenda faili la Ole Sabaya ndio amelisimamia ndio maana wengi sasa wanamuogopa wakijua anaona wasiofaa km kina Makonda kutosogelea utawala huu
 
Kwa Kumbukumbu Kawawa alikuwa Waziri Mkuu. Hata kama alivikwa cheo cha Makamu wa Pili wa Rais bado alikuwa na Authority kama Mkuu wa Shughuli za Utendaji Serikalini. Lakini Makamu wa Rais sidhani kama Chain of Command inampasa afanye
Wewe unataabika na nini juu ya hilo? Kuwa wewe unajua kuliko yeye?
Au unadhani amepata nafasi hiyo kwa kubahatisha?
Muache afanye kazi zake, hutaki, hama nchi.
 
Sasa wewe unaejua vifungu njoo na hivyo vifungu tuone Umahili wako Mkuu. Majukumu ya VP kwenye Muungano yako Mahsusi Kikatiba. Sasa wewe unaetaka kuhalalisha Maajukumu mengine kiutendaji njoo na Hivyo Vifungu
mngetuwekea hiyo Chain of Command au Katiba inayomuwekea VP mipaka kwanza ndipo tuendelee
km haipo muacheni Makamu wa Rais awakemee hawa wazinzi na wala Rushwa wanaotamani Ukuu wa Mikoa na Wilaya kujifanya Marais huko waliko
 
Kumbe humu jamvini kuna watu vilaza kweli2! MR ana mamlaka makubwa kumfuatia Rais sema wengi huwa ni wapole, lakini anaweza kuchukua hatua kwa kiongozi yoyote kasoro boss wake. Kama mambo hamyajui ulizeni siyo ujinga kufanya hivo!
 
Tangu ateuliwe Kama Makamu wa Rais Dr. Mpango amekuwa akitoa kauli za Kiutendaji bila kujali Mipaka ya Majukumu yake.

Mara ya Kwanza alisikika akimuagiza Waziri wa Fedha akusanye Tilioni 2. Bila kujua kwamba Mamlaka hayo ni ya Rais kwenda kwa Waziri wa Fedha kisha Kamishna Mkuu TRA.

Pili, Tena kasikika akiwaagiza Wakuu wa Mikoa Masuala ya Kinidhamu bila kujua kwamba, Mamlaka ya uteuzi na maagizo ya Kinidhamu yako Ofisi ya Rais - Tamisemi.

Huyu Dr anasahau kuwa yeye ni reserve wa Rais endapo litatokea (Mungu aepushe mbali). Na kwamba Mamlaka yake ya Maagizo ya Kiutendaji yako kwenye Mazingira na Muungano.

Afundwe huyu.

Nikweli anapenda sana matamko
 
Hesabu iko hivi, kuna kitu CCM wa bara wanafanya kwa kuwa hawakudhania mambo yangekuwa yalivokuwa - disobedience!! Ilianza siku Dr. Mpango alipopewa nafasi ya kushukuru na kuaga Bunge. Yeye akatumia nafasi hiyo kueleza misimamo ya serikali na huku hata Rais hajapata nafasi ya kulihutubia Bunge.

a) Huko Bungeni kuna wengine wanadai wafanyiwe vitu majimbo mwao.
b) Wengine wanakiri uonevu wa wafanyabiashara na makundi mengine ya wananchi.
c) Wengine wanapinga chanjo.
d) Mara matatizo ya Tanesco, Bandarini nk.

2025 kutakuwa na watia nia wa kutosha!!
 
Makongoro yuko smart?

Kweli akili ni nywele na kila mtu ana zake.
Ukiachana na kwamba anapiga mvinyo Jambo ambalo sio dhambi maana iyo ndo burudani yake naomba unipe mapungufu mengine ya Mackongoro ,mtu kua smart sio kwamba alazima asiwe na mapungufu KWA 100%, Binafsi nauona uongonzi mzuri ndani yake tena wa kiwango Cha juu kuliko watu mnavyomchukulia katika Mambo madogo madogo ya kijamii, tunao viongozi wapo tu KWA sababu ya bahati, au kubebwa lakin nakwambia mtu kama hujampa nafasi ya kutenda hutojua uwezo wa mtu, hivyohivyo kwenye jamii tunao watu bora Sana tatizo kupata nafasi kuonyesha uwezo wao ndo shida
 
Mpango ni makamu kutoka bara
Ni kweli na hapa katika Katiba ya 1977 inakubali lkn baada ya Muundo wa Vyama vingi naona ilibadilika ndio tunayoitafuta na tunayoizungumzia, je ni kweli Mkamu haendi Visiwani Kikazi?
na je haruhusiwi kufanya kazi zozote isipokuwa kwa kuagizwa na Rais? na ile ya Mazingira?
1621589979634.png
 
Back
Top Bottom