Mikael Aweda
JF-Expert Member
- Dec 17, 2010
- 2,973
- 3,901
Leo baadhi ya magazeti yakiwepo magazeti yenye majina makubwa yamempigia Chapua kigogo wa siasa za chama cha Mapinduzi, Edwad Ngoyai Lowasa kuwa washabiki wake wengi wameshinda.
Gazeti la Mwananchi imeiweka ktk ukurasa wa Mbele kuwa Lowassa azidi kuinyanyasa CCM na kutoa maelezo mengi kujenga hoja yake.
Nimesoma pia gazeti la Fahamu lililo na kichwa cha habari Lowasa ambwaga Kikwete, Sitta.
Msingi wa hoja ya magazeti hayo ni ushindi wa maswahiba wa Lowasa ktk mikoa kadhaa yaliyotajwa ambayo mingi kidogo
Pili wamezungumzia ushindi wa maswahiba wa Kigogo wao huyo Lowasa ambaye pia anaonekana kupata washabiki ktk jumuiya za Chama ikiwepo UWT ambao wamemaliza uchaguzi wao majuzi.
Binafsi nimepata kuongoea na watu wa Nyumbani, yaani mkoa wa Manyara ambako kuna madai kuwa wapo washabiki wa Lowasa walioshinda ndani ya ccm.
kwa upande wangu baadhi ya Shughuli zangu inaniwezesha kutembelea wilaya nyingi za mkoa wa Pwani ambako pia kuna baadhi ya maswahiba wa Lowasa kushinda ktk baadhi ya wilaya.
Jana nilipata fursa ya kuongea na Classmate wangu wa Udsm ambaye pia aliniambia kuwa nyumbani kwao mkoa wa Musoma wako washabiki wengi wa Lowasa ambao wameshinda ikiwemo musoma mjini.
kwa hiyo basi mimi najiuliza;
Pamoja na kwamba ni ngumu kuthibitisha kwamba huyu mfuasi wa x na yule wa y, bado kuna uwezekano wa Lowasa kuwa na nguvu ndani ya ccm. Hata hivyo, mimi bado natafakari jambo hili na linanisumbua kidogo.
Hivi kweli Lowasa binafsi na wafuasi wake (+ pasco wa JF) Wanadhani kwamba wakishinda kihalali au kimizengwe kwa kutumia fedha ndani ya ccm watakuwa uwezo wa kutumia mbinu hizo kupambana na Chadema na kushinda uchaguzi?
Au wanategemea kubebwa na Tume ya Uchaguzi kama ilivyokuwa 2010?
Au
Wanasubiri zile dua za Wasira kwamba Chadema itasambaratika kabla ya 2015 halafu siku chache baadaye akina Estha Wasira wanajiunga Chadema?
Niseme kweli,
Binafsi sijaelewa, nahitaji kusaidiwa kuhusu hili. Kwa maoni yangu ni ngumu sana ccm kurudi ikulu kwa mgongo wa Edward Lowasa anayeshinda kwa fedha. kura zake zitakuwa kama za uhuru Kenyatta aliyebebwa na Arap Moi, wakaumbuka. Kashfa ya Richmond bado itakuwa mjadala wakati huo. Kinachonishangaza ni ujasiri wa hao wanaoipenda chama chao ccm na ambao wanadhani kwamba Lowasa ndiye atakayewavusha. Nataka kujua ujasiri ulioko ktk akili za hawa. Kwa kuwa ni watu wa wazima wakiwemo mawaziri lazima kuna kitu kinachowaaminisha kuwa tukishinda ndani ya ccm tutashinda pia uchaguzi mkuu. Ni nini hicho wanachokiamini wakati sisi tunatengeneza katiba mpya itakayoleta tume huru na kuzuia wizi wa kura. Au katiba mpya na tume huru ni changa la Macho? Sijapata jibu.