Chaguzi za ndani ya CCM: Lowassa awabwaga Kikwete na Sitta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chaguzi za ndani ya CCM: Lowassa awabwaga Kikwete na Sitta

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mikael P Aweda, Oct 23, 2012.

 1. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #1
  Oct 23, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Leo baadhi ya magazeti yakiwepo magazeti yenye majina makubwa yamempigia Chapua kigogo wa siasa za chama cha Mapinduzi, Edwad Ngoyai Lowasa kuwa washabiki wake wengi wameshinda.
  Gazeti la Mwananchi imeiweka ktk ukurasa wa Mbele kuwa Lowassa azidi kuinyanyasa CCM na kutoa maelezo mengi kujenga hoja yake.
  Nimesoma pia gazeti la Fahamu lililo na kichwa cha habari Lowasa ambwaga Kikwete, Sitta.
  Msingi wa hoja ya magazeti hayo ni ushindi wa maswahiba wa Lowasa ktk mikoa kadhaa yaliyotajwa ambayo mingi kidogo

  Pili wamezungumzia ushindi wa maswahiba wa Kigogo wao huyo Lowasa ambaye pia anaonekana kupata washabiki ktk jumuiya za Chama ikiwepo UWT ambao wamemaliza uchaguzi wao majuzi.

  Binafsi nimepata kuongoea na watu wa Nyumbani, yaani mkoa wa Manyara ambako kuna madai kuwa wapo washabiki wa Lowasa walioshinda ndani ya ccm.
  kwa upande wangu baadhi ya Shughuli zangu inaniwezesha kutembelea wilaya nyingi za mkoa wa Pwani ambako pia kuna baadhi ya maswahiba wa Lowasa kushinda ktk baadhi ya wilaya.

  Jana nilipata fursa ya kuongea na Classmate wangu wa Udsm ambaye pia aliniambia kuwa nyumbani kwao mkoa wa Musoma wako washabiki wengi wa Lowasa ambao wameshinda ikiwemo musoma mjini.

  kwa hiyo basi mimi najiuliza;
  Pamoja na kwamba ni ngumu kuthibitisha kwamba huyu mfuasi wa x na yule wa y, bado kuna uwezekano wa Lowasa kuwa na nguvu ndani ya ccm. Hata hivyo, mimi bado natafakari jambo hili na linanisumbua kidogo.
  Hivi kweli Lowasa binafsi na wafuasi wake (+ pasco wa JF) Wanadhani kwamba wakishinda kihalali au kimizengwe kwa kutumia fedha ndani ya ccm watakuwa uwezo wa kutumia mbinu hizo kupambana na Chadema na kushinda uchaguzi?
  Au wanategemea kubebwa na Tume ya Uchaguzi kama ilivyokuwa 2010?
  Au
  Wanasubiri zile dua za Wasira kwamba Chadema itasambaratika kabla ya 2015 halafu siku chache baadaye akina Estha Wasira wanajiunga Chadema?
  Niseme kweli,
  Binafsi sijaelewa, nahitaji kusaidiwa kuhusu hili. Kwa maoni yangu ni ngumu sana ccm kurudi ikulu kwa mgongo wa Edward Lowasa anayeshinda kwa fedha. kura zake zitakuwa kama za uhuru Kenyatta aliyebebwa na Arap Moi, wakaumbuka. Kashfa ya Richmond bado itakuwa mjadala wakati huo. Kinachonishangaza ni ujasiri wa hao wanaoipenda chama chao ccm na ambao wanadhani kwamba Lowasa ndiye atakayewavusha. Nataka kujua ujasiri ulioko ktk akili za hawa. Kwa kuwa ni watu wa wazima wakiwemo mawaziri lazima kuna kitu kinachowaaminisha kuwa tukishinda ndani ya ccm tutashinda pia uchaguzi mkuu. Ni nini hicho wanachokiamini wakati sisi tunatengeneza katiba mpya itakayoleta tume huru na kuzuia wizi wa kura. Au katiba mpya na tume huru ni changa la Macho? Sijapata jibu.
   
 2. M

  MR.PRESIDENT Member

  #2
  Oct 23, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna siku nitakayofurahi kama Lowasa akiwa mgombea Urais kupitia CCm maana kaburi la ccm litakuwa wazi kabisa.
   
 3. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #3
  Oct 23, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkuu,
  Ni kweli Lowassa ana nguvu sana ndani ya magamba, na hakuna wa kumuzuia kwa namna yoyote, kutokana na ukwasi mkubwa alionao, na magamba kuhalalisha kupata uongozi ni lazima kutoa rushwa. kwa kifupi hakuna mtu ndani ya magamba atakae mzidi kwa rushwa Edo.

  Ukiachilia mbali hao wadau uliowasiliana nao, leo ni Uchaguzi wa UVIVUCCM, hao vijana wanaingia wote ni wa timu mmoja tu, ya Edo, so kwa vyovyote vile team ya Edo kwa hao vijana wa VIVUCCM, atashinda kutokana na ile kitu Mlungula.

  Kwa vyovyote vile, ile katiba tayari, tume huru ya uchakuzi ama bla bla bla LAZIMA CHADEMA kushinda 2015, ni LAZIMA...Wacha wajipange kuwa chama pinzani 2015.
   
 4. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #4
  Oct 23, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  du mungu mkubwa acha wachafuane cdm njia nyeupeee ....bado membe atakuja na wale watu 11 aliosema hadharani atawavua nguo
   
 5. C

  Concrete JF-Expert Member

  #5
  Oct 23, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Anajua akiteuliwa kuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM kwa hali na mali lazima mfumo mzima wa serikali na dola umbebe iwe kwa haki au hila, hivyo suala la yeye kuteuliwa kutaka kuteuliwa na CCM ni vita yake binafsi tena sasa, lakini akishateuliwa na CCM vita ya kupambana na Chadema ni ya chama kizima, serikali na vyombo vyote vya dola.
   
 6. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #6
  Oct 23, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Pompo and Mr. President,
  Mimi nakubaliana na nyinyi wote kuwa Lowasa akiteuliwa na CCM ni sawa kuiweka rasmi Chadema ikulu 2015 kama tutamchagua mgombea mzuri.

  Lazima kutakuwa kura ya uasi hata ndani ya ccm, watake wasitake. kuna wanaodhani kwamba Lowasa akianza kujieleza atasafisha hali ya hewa. Siamini hivyo.
   
 7. Mpitagwa

  Mpitagwa JF-Expert Member

  #7
  Oct 23, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,296
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Kaka hoja yako hii ilishajibiwa na mchadema mwenzio Mkumbo (PhD). Na kama nakumbuka alisema hivi, ndani ya siasa za CCM hakuna wa kumshinda Lowasa. Ni kigogo kweli kweli, lakini ukija kwenye siasa za kitaifa, Lowasa ni mwepesi sana na hasa akipambanishwa na mtu kama Slaa (phD). Hivyo basi CCM, wapende wasipende lazima watacheza mdundo wa Lowasa. Ina maanisha hivi, either Lowasa mwenyewe atasimama kama mgombea urais, pili atampendekeza mtu wake wa kumuongoza kwa remote, tatu hata Chadema, Lowasa akiamua kuwajia kwa syle yake ya eagle msidhani atawavuruga kidogo. Lowasa mnamkosea kidogo katika uchambuzi wenu, mnadhani hakuna kabisa watu wanaomkubali Lowasa kwa hoja. Mnadhani wote wanampendea hoja. Tumia JF, na facebook, utagundua kuwa kuna kundi kubwa la watanzania wanampenda Lowasa na wanasema wanampendea kuwa anauwezo wa kufanya na kusimamia maumizi yake. Wanasema pia Lowasa tofauti na wansiasa wengine, mkikubaliana hakugeuki, anachoongea mbele yako na ukiondoka ataongea hicho hicho.
  Na mwisho, nyie kama viongozi wa CDM, msifanye makosa wanayofanya CCM kwa kutumia muda mrefu kuwajadili nyinyi badala ya kero za wananchi. Nyie viongozi wa CDM, tumieni muda mwingi kujadili MBADALA. Jichunguzeni kama CDM, mnamapungufu gani, watu kama akina Mwanakijiji wameshajadili hapa jamvini wanayoyaona kama mapungufu ya CDM, yachambueni kwa undani na muone yapi ni kweli na myawekee mikakati ya kuyashughulikia. Vinginevyo tusubiri malalamiko yenu kuwa atakayekuwa rais toka CCM ameiba kura. itakuwa too late
   
 8. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #8
  Oct 23, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Sikubaliani na wewe, hiyo ni historia.
  Nina uhakika kama Lowasa akishinda Samweli Sitta atahama ccm ama atamhujuma ndani kwa ndani. Vivyo hivyo, Samawel Sitta akishinda Lowasa ama atahama Chama au atamhujumu ndani kwa ndani. Na ikifika hapo, ngome inogile.
   
 9. REMSA

  REMSA JF-Expert Member

  #9
  Oct 23, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,569
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Lowasa hasafishiki hata wangekusanya maji yote ya Tanzania nzima ya mito na maziwa na bahari
  na sabuni wakusanye zote viwandani na Imported,hawawezi msafisha Lowasa kwa Watanzania.
   
 10. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #10
  Oct 23, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,052
  Likes Received: 4,609
  Trophy Points: 280
  How & why mods allowed you to be registered with similar ID like mine..?? I will claim you to CHANGE UR ID ASAP...


  Kuhusu Lowassa sioni kizuzi chochote kwa yy kutokuwa Rais 2015.... No one can RESIST HIM.... he is capable, likeable, Eligible, he has interest to be President, Hardworking.... active too... He has all...
   
 11. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #11
  Oct 23, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mkuu,
  Asante kwa ushauri wako. Hata hivyo, ni ngumu sana Shekh au Askofu kuhubiri mwaka mzima bila kumtaja shetani. Atazungumzia nini? Vivyo, mijadala ya Chadema lazima pia iendane na mikakati, hoja na mashambulizi toka ccm.Mitandao ya kijamii ni njia mojawapo ya kujilinda. Na hii Ndo siasa yenyewe.
  Hata hivyo, nakubaliana na wewe pia kuwa tunahitaji kuja na suluhisho la matatizo ya wananchi pamoja na kupambana na hoja, mikakati na mizengwe ya ccm. Chadema iko fiti ktk maeneo hayo.
   
 12. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #12
  Oct 23, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mr. President,
  Are you serious?
   
 13. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #13
  Oct 23, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Mgombea mzuri ndani ya cdm zitto kabwe tu na hakuna mwingine, bila yeye cdm isahau kuingia ikulu hata km mgombea wa ccm wakiweka jiwe, huo ndio ukweli na hakuna ubishi, hatutegemei kuona wagombea wazee wakitoka cdm
   
 14. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #14
  Oct 23, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Napata wasiwasi sana kufikiria huwa unawaza nini, km mnajua suluhisho la matatizo ni kujenga hoja za suluhisho la matatizo ya wananchi, kila siku barabarani huwa mnafuata nini? cdm kuweni weledi wa mambo ya siasa mnaonekana km mnajifunza siasa
   
 15. s

  sinshoo Member

  #15
  Oct 23, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  El ana mipango, uwezo wa kuunganisha timu ya ushindi pia anajua nini anafanya, Huu ni muda wa kufanya kazi za siasa kwa CDM achana na Lowasaaaaaa afanye kazi yake ya kisiasa ndani ya CCM fainali 2015

   
 16. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #16
  Oct 23, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,259
  Likes Received: 10,244
  Trophy Points: 280
  Lowassa hana mpinzani akiwekwa kugombea Uraisi awe Slaa awe Mbowe hawataweza kupambana naye. Hii ni kweli wala sio propaganda. Acheni mchezo Lowassa ananguvu sana hapa nchini. Keep watching.
   
 17. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #17
  Oct 23, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,052
  Likes Received: 4,609
  Trophy Points: 280
  What..?? LIKEABLE ... u mean Lowassa isn't likeable or u suffer with spelling @ ur age..!!!!?? Go & search.... Don't get obsessed with British English, American English is there too...!!! So where are u at!!??

  Lowassa. HANA MPINZANI CCM 2015 MARK MY WORDS.... KEEP THIS..!!!!
   
 18. JUST

  JUST JF-Expert Member

  #18
  Oct 23, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
   
 19. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #19
  Oct 23, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Hakika out of all ccm wanaoweza kupata kura yangu ni yeye, naamini anaweza, ana sifa. Binafsi sipendi majungu na uonevu, nimesoma ripoti ya kina mwaki kuhusu richmond from pg one to the last zaidi ya maramoja sijaona cha maana, nimefuatilia mashtaka ya Gire mpaka kushinda ile kesi nakaa najiuliza hv ni kwanini niwe shabiki kwa wapiga domo kwa manufaa ya watu flani? huo ufisadi usio na vidhibiti ndani ya ccm nani atakaetoka ndani ya ccm? mtazamo wangu ni **** cdm itashinda pale wananchi watakapokubali mabadiliko makubwa, lkn El atapata kura za haki kusimama. na of coz jamaa amedeliver. Mnune tu lkn huo ndo ukweli. Nami nashangaa Cdm kuingia kichwakichwa against El, au ndo ile MoU na Sita? na siku Sita akigombea Cdm jueni wazi atakosa kura za wapenzi wa Cdm wanaompenda edo na wale wa nje including ccm ambao ni pro edo live alone kura za adhabu za jumla za uasi wa mwanaCcm.
  ukitaka kubisha, bisha au kejeli lkn huo ndo UKWELI wenyewe.
   
 20. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #20
  Oct 23, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  mkuu badili id yako isomeke mrithi wa sheikh yahaya ?
   
Loading...