Elections 2010 Chaguo Letu Bumbuli: January Makamba

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,695
1,696
Source ya Picha: Michuzi​

BUMBULI-1.jpg

Need We Say More?​
 
Superman, naona unaanza kupoza direction. Hivi ujasikia usemi usemao kuwa 'Lisemwalo lipo'. Sasa kama unakubaliana nami kuwa lisemwalo lipo basi kaa ukijua kuwa aliyesema 'lisemwalo lipo' huyo huyo alisema 'Mtoto wa nyoka ni nyoka' Be very careful my dear usijekuta chaguo lako badala ya kuwa nyoka wa kawaida, akawa CHATU MLA WATU. Utamezwa ukijiona.
 
Huyu anayajua kweli matatizo ya wana Bumbuli? Au tu kwa propaganda za chama TWAWALA wananchi wameanishwa kuwa huyo ndiye nabii wao?
 
Kama Kikwete kama January. Baada ya October 31 kama wakifanya makosa watu wa Bumbuli watabaki kwenye kilio kile kile kwa miaka mitano. Naomba mod uitunze thread hii kama ukumbusho.
 
Mchukia Fisadi said:
Kama Kikwete kama January. Baada ya October 31 kama wakifanya makosa watu wa Bumbuli watabaki kwenye kilio kile kile kwa miaka mitano. Naomba mod uitunze thread hii kama ukumbusho.

Mchukia Fisadi,

..January Makamba hana mpinzani ktk nafasi ya ubunge jimbo la Bumbuli. kwa sasa hivi, anasubiri kuapishwa tu.

..Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, naye hakupata mpinzani kwa hiyo na yeye anasubiri Nov aapishwe.
 
Habari ndio hiyo...
 
Mzee Mwanakijiji jifunze kusema hivi "Let it go";

Wewe na mimi na wa2 wa Bumbuli yanatuhusu nini? wewe ni mpiga kura wa jimbo hilo? hapana, wewe ni mwanachama wa CCM au chama chochote kilichosimamisha mgombea kwenye hilo jimbo? no... please mzee.
 
Mkuu, hebu tangaza nia 2015...
Mbona hii haina shida, kama watu wa Bumbuli wanamtaka huyo, baada ya 31st October itakuwa wazi tuu, labda kwa hali yao halisi wanaona ndio suluhisho. Kule Kagera kulikuwa na mbunge akiitwa Zimbihile alikuwa akichaguliwa kila kukicha pamoja na kuwa wakati wote akisinzia bungeni, pia Ruwangisa amabaye alidiriki kuwaambia wapiga kura kuwa pesa zangu ndio zimenichagua. Sasa huyu naye atasema kama si baba ..........mh ?all in all ndio siasa zetu za watu kudhalilishwa bali wakiendelea kusema kidumu chama cha ...... watamalizia wenyewe.
 
Mzee Mwanakijiji jifunze kusema hivi "Let it go";

Wewe na mimi na wa2 wa Bumbuli yanatuhusu nini? wewe ni mpiga kura wa jimbo hilo? hapana, wewe ni mwanachama wa CCM au chama chochote kilichosimamisha mgombea kwenye hilo jimbo? no... please mzee.

Mbunge wa Bumbuli haiingii katika bunge la Bumbuli, anaingia katika bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania, na hatungi sheria za Bumbuli tu, anatunga sheria za Tanzania.

Kwa hiyo huwezi kusema Watanzania wasiwe concerned na chaguzi za majimbo ya mbali, as long as majimbo haya yapo Tanzania yanatuhusu sana.

Sheria hii hii ya kipuuzi inayoruhusu mtu kuingia bungeni bila kuchaguliwa na wananchi wala kuwa kutoka special seats inaweza kumruhusu mbunge wa Bumbuli, Ilala au Kinondoni.
 
Hivi kwa mfano tarehe 31 Oct asitokee hata mtu mmoka kupiga Kura, yaani January hana kura hata moja Sheria inasema chochote katika hili?

Kwa mujibu wa sheria na majadiliano yetu hapa katika thread ya Mwanakijiji juu ya suala hili (kwa kutumia nukuu za katiba) tarehe 31 Oktoba January hana uchaguzi kwa sababu "amepita bila kupingwa". Kwa hiyo hamna watu kupiga kura, anaapishwa tu.

Sijui kama hili limebadilishwa since then. Ridiculous.
 
Sasa huyu naye atasema kama si baba ..........mh ?all in all ndio siasa zetu za watu kudhalilishwa bali wakiendelea kusema kidumu chama cha ...... watamalizia wenyewe.
wewe inaonekana wazi kuwa upo usingizini. January amekuwa chaguo la Bumbuli kutokana na msimamo wake juu ya maendeleo ya Wanabumbuli na Watanzania kwa ujumla.

Katika karne hii, tunahitaji watu wa aina yake, ambao wanaweza kubadilisha maisha ya wengi katika kuelekea katika maendeleo binafsi na ya taifa kwa ujumla. Zaidi wananchi wa Bumbuli wameona kitu ambao wewe hujakiona!
 
Mzee Mwanakijiji jifunze kusema hivi "Let it go";

Wewe na mimi na wa2 wa Bumbuli yanatuhusu nini? wewe ni mpiga kura wa jimbo hilo? hapana, wewe ni mwanachama wa CCM au chama chochote kilichosimamisha mgombea kwenye hilo jimbo? no... please mzee.

uliwahi kusikia kuna Bunge la Bumbuli? siku wakianza kuwa na Bunge lao, lenye kutunga sheria zao na mimi nitaacha kuuliza yanayotokea! Unless kama akiingia Bungeni la Muungano atazungumzia mambo ya Bumbuli tu!
 
wewe inaonekana wazi kuwa upo usingizini. January amekuwa chaguo la Bumbuli kutokana na msimamo wake juu ya maendeleo ya Wanabumbuli na Watanzania kwa ujumla.

Katika karne hii, tunahitaji watu wa aina yake, ambao wanaweza kubadilisha maisha ya wengi katika kuelekea katika maendeleo binafsi na ya taifa kwa ujumla. Zaidi wananchi wa Bumbuli wameona kitu ambao wewe hujakiona!

Unless sheria ya uchaguzi itabadilishwa, na watu wa Bumbuli watapewa nafasi ya kumpigia kura, January hawezi kuwa chaguo la Bumbuli kwa sababu ataingia bungeni bila kuchaguliwa.
 
Unless sheria ya uchaguzi itabadilishwa, na watu wa Bumbuli watapewa nafasi ya kumpigia kura, January hawezi kuwa chaguo la Bumbuli kwa sababu ataingia bungeni bila kuchaguliwa.

kwa Hiyo tarehe 31 Oct Wananchi wa Bunbuli hawatapiga Kura ua Ubunge ay
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom