Chagua mke/ mume uliyeridhika naye kwa 100%

Chagua mke/ mume uliyeridhika naye kwa 100%

Bernard bakari

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2016
Posts
407
Reaction score
781
Ni jambo la busara na hekima kubwa kumchagua mpenzi, mchumba, mke au mume ambaye umeridhika naye kwa 100%.

Ipo tabia ya watu kumchagua mwenza wao kwa sababu fulani tu yawezekana ikawa kufata mali ya mwenzake au chochote kile wakati ndani ya moyo wake hajaridhika naye hata kidogo.

Madhara ya jambo hili ni kubwa hupelekea migogoro ya mara kwa mara ndani ya nyumba, michepuko isiyoisha, kuachana pindi kile alichokifata kinapokosa thamani tena kwake na mambo mengine yanayoendana na hayo.

Binadamu wote walikuja duniani wakiwa watupu mali wamezipata hapa duniani sasa kwanini ujirahisishe uwe na mtu usiyefurahi naye kisa ya mali. Tafuteni zenu na ridhikeni na hala zenu.

Mapenzi matamu bwana hasa upate unayeridhika naye na uliyempenda kwa dhati kutokana na jinsi alivyo. Uliyeshawishika na umbo, tabia na mwonekano wake si mali wala jambo la kujifanya ujioeleke kwake ili upate kitu fulani.
 
Mkuu haya mambo hayana ujanja ni kuomba Mungu akupe mwenza mtakae ishi nae kwa amani. Maana unaweza kukaa nae kwenye uchumba/upenzi mtu akawa ana pretend, mkiingia ndoani ndio inakua shughuli rangi halisi zinaonekana
 
Tatizo kuu ni moja
Binaadamu anabadilika kulingana na mambo kadha wa kadha,
Hivyo unaweza kuridhika nae katika hali hii
Akabadilika kuwa kwenye hali nyingine,
Hapo utafanyeje ?
 
kuna mtu amekunanga kuw wewe ni spy lkn bahati mbaya uzi umefutwa, akatupa tahadhari kuw tujiepushe na wewe katika kila hali.
wapi huko mkuu? mi sikuona ndo maana niliona watu pm wananilaumu eti miss kumbe wewe tiss .tiss ndo nini kwanza? ni nani huyo mkuu?
 
Hapo unatakiwa ujifungishe ndoa/kujioa mwenyewe!

Na sidhani hata kujioa mwenyewe nako kutakuridhisha kwa hiyo 100%!

Dadaz wengi hawaridhiki na baadhi ya maumbile yao!

Akina sisi wengi haturidhiki na madushe yetu!

Sasa hiyo 100% itatoka wapi?! Ikiwa dushe lako mwenyewe tu huridhiki nalo na hivyo kuona haupo 100% OK, ni namna gani unatarajia hiyo 100% itoke kwa mwenzako?!
 
Akinitaka kunioa nitakubali sababh tu nampenda yakitokea yakutokea huko mbeleni sawa pia.
Hakuna mkamilifu shost!
Ukikuta ana sifa mbili tatu unazozihitaji unamkubali,mengine utayavumilia mbele kwa mbele.
 
Back
Top Bottom