Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 376,454
- 872,087
Ni kuhusu pesa ya ESCROW iliyorejeshwa na mmoja wa wanufaika ndugu William Ngeleja.
Kwa utashi wake mwenyewe ama kwa kuombwa au kushurutishwa kufanya hivyo na pengine pia kuhukumiwa na nafsi.... Ngeleja aliamua kurudishwa jumla ya Tsh 40, 000, 000/=
Ukisikia ujasiri na uthubutu ni huu.... Wengi kwa mamilion hawawezi, wasingeweza! Ngeleja kaweza
Mabezo yamekuwa mengi lakini yeye ana amani sasa, katua mzigo mzito sana.... Kama kuna jinai hicho ni kitu kingine
Mzigo alioutua Ngeleja umebebwa na mamlaka ya mapato, kupitia account yake halali ya kodi za ndani (domestic revenue) pesa ililipwa na kupokelewa... Siku chache zilizopita
Leo kupitia msemaji wa hizo kodi mamlaka imekana kuzitambua pesa husika (nimekumbuka vichwa vya treni bandarini)...... Kama ni kweli hawazitambui hizi pesa (kiuhalisia iko hivyo) na kwa kutumia weledi uliotukuka
WAZIRUDISHE ZILIKOTOKA kinyume chake majibu yatakuwa mapya kila uchao
Sent using Jamii Forums mobile app