Chadema zingatia haya

Chadema zingatia haya

rosemarie

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2011
Posts
6,887
Reaction score
3,446
Pesa ni kwa ajili ya kujenga chama na kusaidia katika kampeni mbalimbali kama za udiwani zilizopita,money matters,kama chama kinashindwa kusaidia wagombea kifedha kushinda itakuwa ni ngumu sana kupata ushindi,chama kilete mipango mipya ya kukusanya fedha za michango kutoka kwa watanzania na kuzitawanya sehemu mbalimbali kusaidia wagombea na ofisi za chama zipate fedha kutokana na michango hiyo.

Chama kitafute wagombea wanaofaa na kukubalika,ni vyema mgombea yeyote kutoka ngazi ya chini kabisa mpaka juu ajulikane background yake na uhusiano wake na wapiga kura iwe kata,kijiji,jimbo hata taifa, Chama kujenga uhusiano mzuri na vyombo muhimu vya habari ni muhimu kuliko tunavyofikiri, chama kitafute smart consultants watakayofanyia kazi strategy za chama... hapa sitaki kuingia ndani manake ccm nao wanachungulia hapa.

Chama kisiwalaumu wapiga kura kama wamemkataa mgombea wa ,lazima kutakuwa na sababu,zile issue za kununua vitambulisho vya kupigia kura na hongo tuviweke pembeni kwa sasa,tunaongea uchaguzi usiohusisha rushwa at all. Chama kitumie vijana hasa wanaongia miaka 18 sasa hivi na hawajawi kupiga kura,chama kiongee na hawa vijana wadogo kuhusu mambo yao je wanataka nini na wangependa viongozi wa aina gani???

Hawa vijana wadogo watakipa chama nguvu ya kushinda Wananchi kutoka kwenye vitongoji na kata wahusishwe moja kwa moja kwenye process nzima ya uchaguzi kuanza kupata mgombea wanayemtaka mpaka uchaguzi,wapewe mafunzo na vifaa vyote vya kazi vinavyostahili,muhimu sana kwa kuwa hawa ndio wenye uwezo wa kuwashawishi wapiga kura kubadili mwelekeo.

Chama kitumie mitandao kama facebook,twiter etc,inasaidia kwa kuwa wapiga kura wengi wanapitia Kwa nini ccm wanatumia sana wasanii??kuvutia watu waje wasikilize??nafikiri chama kifikirie kutumia baadhi ya wasanii japo sio lazima,kuna umuhimu wake vilevile
 
nimeipenda na ni wazo zuri na la kujenga, naamini kuwa wapo viongozi nwanaopita humu jf, wachukue maoni haya na kuyafikisha kwa wahusika, pia naomba pia chama wajaribu kuangalia suala la media ya chama mfano tv redio na hat magazeti ili watu wapate taarifa ikiwa sahihi bila kuchakachuliwa, thanks
 
Hatari ya hili la kuiangalia CCM
kuwa itaanguka au kuwa iko
karibu kuanguka inasahau jambo
moja kubwa kuna wakati ambapo
inabidi uisaidie ianguke. Kwa
wale ambao wamewahi kukata
miti mikubwa wanajua kuwa
kuna wakati ukisha kata mti
hauukati ukaumaliza bali unaukata
halafu unatafuta mahali ili kuvuta
kamba na kuuangusha; yaani
unausaidia uanguke. CCM iko
katika hali ya kuanguka na kila
sababu ya kuanguka ipo; hata
hivyo CHADEMA bado inaonekana
haiko tayari kuiangusha CCM na
matokeo yake ni haya ya kucheza
‘hiki na hoko’.
CHADEMA inapozidi kujiandaa na
chaguzi nyingine zijazo inapaswa
kuanza kujiuliza maswali ya akili
badala ya kuendelea na kampeni
isiyolipa. Maswali haya ni mengi
lakini naomba nipendekeze
machache tu.

1. Je, ni maslahi ya CHADEMA
kushiriki uchaguzi wowote ule
bila ya sheria inayosimamia tume
ya uchaguzi kubadilishwa?

2. Je, ni maslahi ya CHADEMA
kuendelea kushiriki chaguzi hizi
mbalimbali bila kufanya
mabadiliko katika mfumo wa
kuandikisha wapiga kura ili
kuhakikisha wenye haki ya kupiga
kura wanaandikishwa katika kila
uchaguzi?

3. Je, ni maslahi ya CHADEMA
kuendelea kushiriki uchaguzi
chini ya mfumo ambao
umetengenezwa ili kuzuia
upinzani usije kushika madaraka?

4. Je, CHADEMA inahitaji kufanya
nini ili kuimaliza kabisa CCM
badala ya kuiacha iwe kama
mzimu usio kubali kufa?

5. Je, CHADEMA itaendelea kushiriki
chaguzi ambazo wanachama
wake na mashabiki wake
wanauawa na kujeruhiwa mpaka
nani auawe ndio wajue kuwa CCM
haitoachia madaraka kwa
vigelegele?

Bila kujaribu kujibu maswali haya
na mengine CHADEMA itaendelea
kutuhutubia kitu ambacho tayari
tunakijua waanze kufanya
tusivyovijua ili tuone wakishinda
uchaguzi tena siyo kidogo bali
uwe wa kishindo. Vinginevyo
watakapoanguka 2015 watatupa
maelezo ya kwa nini mkono
utaanguka 2020!
 
Chadema naona kama mmepwaya au mmetishwa ? Mazoea nilioyazoea kuona M4C inashika kasi na kufurahia moyoni kuwa mkombozi amekaribia na WaTanzania kuwa huru ndani ya nchi yao.
Mko wapi na mnafanya nini ? Msipunguze kasi na kumpa adui cha kufikiri.
 
We are strategizing, usiwe na papara. Unapopambana na wahuni kama hawa ccm, lazima uwe na mipango ya akili kuwapoteza maboya. Angalia idadi ya kura za udiwani KWA UJUMLA za ccm na CDM kwenye uchaguzi wa udiwani ndo utaziona athari za M4C.
 
Back
Top Bottom