CHADEMA Zanzibar watoa Tamko, Wasikitishwa na madai ya Said Issa Mohamed kuwa aliishtaki CHADEMA kwa niaba yao

Mawele

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
403
Reaction score
1,185
Kufuatia madai ya aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, Said Mohamed, kwamba amefungua kesi kwa niaba ya chama hicho kuhusu mgawanyo wa mali, CHADEMA Zanzibar imesema kesi hiyo ni yake binafsi pamoja na watu wanaomshawishi au kumtuma.

Chama hicho kimefafanua kuwa Said Mohamed hana nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama na kwamba kauli zake hazina uhalali, hivyo wananchi wanapaswa kupuuza taarifa hizo zinazodaiwa kupotosha umma.

CHADEMA 1.jpg

ChADEMA 2.jpg
Soma Tumekuwa kimya kwa sababu tukizungumza tutaivua nguo CHADEMA
 
Huyu kwanini anang'ang'ania asipotakiwa ndo kazi za chama tawala hizi sio bure kila uchwao mgawanyo wa mali kupoteza muda tu yeye amekuwa kwenye hiyo nafasi miaka dahari kwanini hakuona kasumba hilo au ndo hila zake tu?
 
Kufuatia madai ya aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, Said Mohamed, kwamba amefungua kesi kwa niaba ya chama hicho kuhusu mgawanyo wa mali, CHADEMA Zanzibar imesema kesi hiyo ni yake binafsi pamoja na watu wanaomshawishi au kumtuma.

Chama hicho kimefafanua kuwa Said Mohamed hana nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama na kwamba kauli zake hazina uhalali, hivyo wananchi wanapaswa kupuuza taarifa hizo zinazodaiwa kupotosha umma.

Soma Tumekuwa kimya kwa sababu tukizungumza tutaivua nguo CHADEMA
Du aisee kwa hiyo hiyo kesi ni ya issa peke yake a ha ha ha
 
Hii inekuja kwa kuchelewa! Wale wahuni na genge lao, walipaswa kutengwa muda sana.
 
Hao cdm Zanzibar nao walikuwa wapi muda wote kutoa tamko la namna hii? Maana hiyo kesi ina muda sana ikiwa imefunguliwa na hao wahuni. Ama na mimi sielewi.
Hio kauli wametoa baada ya hao wafungua kesi kutoa madai yao kwamba hata uongozi wa Zanzibar uko nyuma yao, hio kauli nadhani wametoa kama sio jana leo
 
Hao cdm Zanzibar nao walikuwa wapi muda wote kutoa tamko la namna hii? Maana hiyo kesi ina muda sana ikiwa imefunguliwa na hao wahuni. Ama na mimi sielewi.
Inashangaza sana
 
Said Mohamed anatumika na CCM sasa mwisho wao ni aibu. Maana CCM mwisho wao umefika. Yaani Kwa heli CCM majambazi.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Zanzibar kimekanusha madai yaliyotolewa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho visiwani humo, Said Mohamed, kwamba amefungua kesi kwa niaba ya chama kuhusiana na mgawanyo wa mali.

Kupitia taarifa yake kwa umma, CHADEMA Zanzibar kimesema kesi hiyo si ya chama bali ni ya Said Mohamed binafsi pamoja na watu wanaodaiwa kumshawishi au kumtuma kufungua shauri hilo.

Chama hicho kimeeleza kuwa kwa sasa Said Mohamed hana nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama, hivyo hana mamlaka ya kukiwakilisha chama katika masuala ya kisheria au kutoa matamko kwa niaba yake.

Aidha, CHADEMA Zanzibar kimesisitiza kuwa kauli na hatua zinazochukuliwa na Said Mohamed hazina uhalali wowote kwa mujibu wa taratibu na katiba ya chama, na kwamba hazipaswi kuchukuliwa kama msimamo rasmi wa chama.

Kutokana na hali hiyo, chama kimewataka wanachama na wananchi kwa ujumla kupuuza taarifa hizo, kikidai kuwa zina lengo la kupotosha umma na kuichafua taswira ya chama.

Hata hivyo, hadi sasa Said Mohamed hakuwa ametoa ufafanuzi wa ziada kuhusu msimamo wa chama juu ya kauli yake wala kujibu hoja zilizotolewa na uongozi wa CHADEMA Zanzibar.
1772639449000.jpg
 
Hao cdm Zanzibar nao walikuwa wapi muda wote kutoa tamko la namna hii? Maana hiyo kesi ina muda sana ikiwa imefunguliwa na hao wahuni. Ama na mimi sielewi.
Basically hakunaga chadema zanzibar haya mambo ya uzanzibar na ubara wameyaleta CCM baada ya hii kesi. Kumbuka kichama zanzibar ina "kamati maalum" tu ambayo inakua chini ya Naibu katibu Mkuu-zanzibar so basically bado ipo chini ya mfumo wa kitaifa zaidi. So akitoa kauli NKM ni kama tu kamati maalum imetoa msimamo maana ni kitu kile kile.

CCM inapenda sana kuleta migawanyo, walipofeli issue ya wachagga na issue ya wakristo sasa wanataka kuigawa kwa msingi wa uzanzibari na bara.
 
Wapuuzi mno ccm.
 
Breaking News;

Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam imeyatupilia mbali mapingamizi yaliyowekwa na Said Issa Mohammed na wenzake kupinga Lissu kuunganishwa katika Kesi ya Mgawanyo wa Mali inayowakabili Katibu Mkuu wa CHADEMA na Bodi ya Wadhamini.

Uamuzi huo umetolewa na Jaji Hamidu Mwanga leo Machi 03, 2026 baada ya kutupilia mbali mapingamizi mawili yaliyowekwa na Wakili wa walalamikaji(Said Issa Mohammed na Wenzake)

Kwa msingi huu maombi ya msingi ya Lissu yatasikilizwa Ijumaa saa tatu asubuhi mbele ya Jaji Hamidu Mwanga.

Taarifa kamili tutakuletea hivi punde
1772645582558.jpg
 
Kufuatia madai ya aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, Said Mohamed, kwamba amefungua kesi kwa niaba ya chama hicho kuhusu mgawanyo wa mali, CHADEMA Zanzibar imesema kesi hiyo ni yake binafsi pamoja na watu wanaomshawishi au kumtuma.

Chama hicho kimefafanua kuwa Said Mohamed hana nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama na kwamba kauli zake hazina uhalali, hivyo wananchi wanapaswa kupuuza taarifa hizo zinazodaiwa kupotosha umma.

Soma Tumekuwa kimya kwa sababu tukizungumza tutaivua nguo CHADEMA
Hao nao walikuwa wapi siku zote tangu kesi kufunguliwa mpaka CHADEMA kusimamishiwa shughuri zote. Wangekataa muda mrefu na wangethibitishia mahakama pia kwa barua ya pamoja na kuisambaza kwenye vyombo vya habari
 
Back
Top Bottom