CHADEMA yazoa zaidi ya 1,000 Morogoro

Eeka Mangi

JF-Expert Member
Jul 27, 2008
3,173
481
Kweli ukichokwa! Yaani CDM imezoa wanachama wapya zaidi ya 1000 Morogoro leo. Kwisha habari yao 2015 tunapata mbwa mwenye uwezo wa kumsukuma Kalumekenge aende shule.

Source: ITV
 
Anayeipenda ccm ni kwa ajili ya kutetea ka mrija kake ka ufisadi tuu!si kutokana na maendeleo ya nchi
 
kazi ipo,na huo ni mwanzo mzuri kwani mwisho wa uchaguzi ni maandalizi ya uchaguzi mwingine
 
Usiseme Morogoro sema katika chuo cha Mzumbe kilichopo Morogoro

tena tambuwa kuwa ktk vyuo ambavyo ccm ilijimalisha ni Mzumbe,kwani nimemaliza SUA nilikuwa na juwa A to Z zao,wakimbiza mwenge wote wapo pale Mzumbe,vyuo ambavyo ccm ilikuwa haivigusi ni SUA -CDM na chuo cha waislamu CAF na hivi vyuo viwili nilivyo vitaja mwaka 2009 havikua na uongozi wa serikali ya wanafunzi baada ya washindi ambao walitoka CAF na CDM kushinda ushindi wao ulipingwa mahakamani na kwa pale CHUO CHA WAISLAMU ilipelekea hata mwalimu wao maalufu wa lugha ya kiswahili kunyimwa mkataba baada ya kushabikia CUF
Kwa hiyo kupata wanachama 1000 ktk ngome ya ccm ni jambo jema kwao
 
kwa mtindo huu kufikia 2014 mwishoni chadema itakuwa na wanachama hai karibia milioni 20.
 
jana jumapili kingunge alienda mzumbe hali aliyokutana nayo hakuamini kwani alilazimika kuahirisha mkutano baada ya kukosa watu. amewalaumu sana wakufunzi mzumbe.
 
jana jumapili kingunge alienda mzumbe hali aliyokutana nayo hakuamini kwani alilazimika kuahirisha mkutano baada ya kukosa watu. amewalaumu sana wakufunzi mzumbe.
Alienda kufanya nini huyo babu wa watu si angekaa tu nyumbani aendelee kula mafao yake,ona kaenda kupata aibu ya mwaka huyo mzee wa watu.Hilo liwe fundisho kwa wanamagamba wote kuwa hawaiwezi Chadema na namna yoyote.
 
Kweli ukichokwa! Yaani CDM imezoa wanachama wapya zaidi ya 1000 Morogoro leo. Kwisha habari yao 2015 tunapata mbwa mwenye uwezo wa kumsukuma Kalumekenge aende shule.

Source: ITV

wewe mangi..hujamsikia nape kua hayupo CDM kwa kuwa ni cha wachaga???sasa una fanya nini magambani huko....??au unajipendekeza..
 
mtashika nchi na hao wanachama 1000. huu ni upuzii mtupu. sasa jumla ya wanachama ni wangapi?
 
kwani chuo cha mzumbe kiko wapi? iwe mzumbe au wapi lkn ni morogoro, mi nadhni yuko sahihi
Siyo hivyo mkuu, ni kweli Mzumbe iko Morogoro lakini kwa hoja iliyopo hapa ingefaa zaidi akisema Mzumbe. Main theme ya ujumbe wake ilikuwa kuelezea idadi ya watu waliojiunga na Chadema, sasa ukisema watu 1000 wajiunga na Chadema Morogoro haina uzito. watu 1000 ni wachache sana kwa population ya mkoa wa Morogoro! lakini watu 1000 kwa population ya Mzumbe ni wengi sana. Mzumbe ni Morogoro lakini Siyo Morogoro yote ni Mzumbe.
 
Back
Top Bottom