CHADEMA yawataka wanaosema kuna matumizi mabaya ya fedha kwenye chama waweke ushahidi hadharani

Hao wamenunuliwa hivyo ni kuwapuuza tu!!
IMG_20200524_125954.jpg

Hapa ni kabla ya kuokotwa na chadema na kupewa ulaji
 
ushahidi gani tena mnataka nyinyi ufipa ?
viongozi kama waitara,dr mashinji,dr slaa,cecil ambao walikuwa ndani ya kamati kuu ya chadema wanathibitisha wizi wa mbowe.
mbona mmeshikiwa akili nyinyi makamanda !!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wabunge Viti Maalumu wa Chadema, walipotangaza adhima ya kukihama chama hicho na kujiunga na NCCR- Mageuzi mara baada ya Bunge la 11 kuvunjwa walitoa shutuma kadhaa ikiwamo unyanyasaji wa kingono.
AYYYAAAAAA!!!
KWELI HUKO CHADE KUNA VIJIMAMBO! DUH
 
CDM nilisema inamkosa katibu mkuu kweli katibu mkuu anayejua uongozi na si chama tu
Katibu atakayeweza kupambana na mkiti kwa hoja na katibu anapaswa kuwajibika kwa kila kitu

Ukisikia mkiti analalamikiwa na wanachama ujue katibu hafanyi kazi au wanakula pamoja na hawapangusi midomo kabla ya kutoka nje
Anapolaumiwa mkiti na katibu alaumiwe kwani pesa haitoki benki bila katibu kuandaa muhtasari wa matumizi na kuambatanisha nakala ya bajeti inayowasilishwa na mtu wa fedha ambaye yuko chini ya katibu

Hivyo kimsingi ukatibu ndiyo unashida na si uenyekiti
Hili la kusema wanachama wanamlalamikia ni makosa. Ni baadhi ya wanachama na waliokuwa wanachama ndio wanaolalamika. Ingekuwa wanachama wengi hawana imani nae wasingemchagua tena kuwa Mwenyekiti wao kwa kipindi kingine. Hamna Katibu Mkuu wa chama chochote anaepambana na Mwenyekiti wake hadharani. Ikitokea hivyo ujue kuwa hiyo nafasi haitaki. Ndivyo ilivyo.

Amandla...
 
Biashara ishafanyika na kutakiwa waseme walichosema nadhan Chadema kama taasisi walipaswa kukaa kimya na kupuuza
 

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimewataka wabunge wenye ushahidi juu ya tuhuma za matumizi mabaya ya fedha, kuuweka hadharani.

Kauli hiyo ya Chadema imetolewa jana Jumamosi tarehe 23 Mei 2020, na Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara, kufuatia wimbi la wabunge waliotangaza kukihama chama hicho, kudai kwamba Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema anatumia vibaya fedha za chama hicho.

“Waambie walete huo ushahidi kwa sababu anayetoa tuhuma anatakiwa alete ushahidi, kama zimekopwa walete ushahidi. Kuna yeyote ameshatoa ushahidi kama zimekopwa?” amehoji Kigaila.

Juzi Ijumaa tarehe 22 Mei 2020, Susan Maselle na Joyce Sokombi , Wabunge Viti Maalumu wa Chadema, walipotangaza adhima ya kukihama chama hicho na kujiunga na NCCR- Mageuzi mara baada ya Bunge la 11 kuvunjwa walitoa shutuma kadhaa ikiwamo unyanyasaji wa kingono.

Pia, walidai hakuna mtu anayeruhusiwa kuhoji juu ya matumizi ya fedha za Chadema.

Tuhuma hizo pia ziliwahi kutolewa bungeni na Spika Job Ndugai, hivi karibuni, ambaye alimtuhumu Mbowe kuwa anawalazimisha wabunge kuchangia fedha hizo.

Ndugai alidai kwamba, kuna wabunge kadhaa wa Chadema walifikisha malalamiko yao katika ofisi yake, ya kwamba wanalazimishwa kutoa sehemu za posho yao, kwa ajili ya kuchangia shughuli za chama hicho.

Kuhusu matumizi ya fedha za Chadema kutowekwa hadharani, Kigaila amesema tuhuma hizo sio za kweli, kwa kuwa bajeti ya matumizi ya chama hicho inapangwa na vikao husika, kisha kupitishwa na baraza lake kuu.

Kigaila amesema baada ya fedha za Chadema kutumika, Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), hukagua taarifa za matumizi hayo.

“Pesa wanazochanga wabunge, madiwani na wanachama wakishachanga zinakuwa za chama haziwi za wabunge, chama kinapanga matumizi ya fedha zozote iwe ruzuku, michango ya wanachama, watu binafsi na wadau wengine, ” ameeleza Kigaila

“Chama kinapanga matumizi kwa kutumia vikao vya chama, bajeti ya chama inapitishwa na baraza kuu kisha matumizi yanaidhinishwa kwa wakati. Na taarifa zinatolewa na kamati kuu, si wabunge wanakaa na kupanga matumizi.”

Wakati huo huo, Kigaila amesema katiba ya Chadema inaelekeza wabunge kuchangia fedha, kwa ajili ya kuendesha shughuli zake.

“Hakuna makubaliano kati ya chama na wabunge isipokuwa kwa kanuni ya chama, wao walichangia kwa mujibu wa kanuni ya chama kama wengine walivyochangia toka mwaka 2006. Hatukai na wabunge tukakubaliana hizi hela zinatumikaje, ni chama kinapanga zinatumikaje, zikishatumika CAG anakuja kukagua, ” amesema Kigaila.

Kigaila ameongeza kuwa “Katiba ya chama hicho imeeleza namna wabunge wanavyotakiwa kuchangia chama, kwamba wabunge wa majimbo watachangia asilimia 10 ya posho, na viti malaumu watachangia asilimia 30 ya posho zao.”

Amesema wanaolalamika kuchangishwa fedha kinyume na sheria, ni uzembe wao wa kutosoma katiba ya chama kilichowadhamini kupata ubunge.

“Mbunge yeyote wa Chadema anakuwa na katiba kabla hajagombea, anateuliwa hadi anashinda, anajua akiwa mbunge atachangia hivyo, hakuna makubaliano chama kinakaa na wabunge wanasema watachangia,” amesema Kigaila

“Hao wanalalamika huenda katiba inaandikwa wakati hawakuwa Chadema, lakini ukiingia Chadema inatakiwa usome kanuni, kama hujasoma hilo ni tatizo lako binafsi.”
Hivi kwa akili ya kawaida tu, Mbowe afuje pesa za CDM Serikali imuache tu mtaani... You guys are not serious

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wajinga hujifariji kwa ujinga wao na kuutetea hadi unapokuwa upumbavu na hapo tena haiwezekani kuwarekebisha.

Kama CHADEMA wanakula fedha kwa kiwango hicho wanachosema CCM ni kwa nini CCM huwa haichukui hatua wakati wao ndiyo wanaoongoza serikali?

Kama wanaotoka CHADEMA ndiyo wanaoujua huo wizi ndani ya CHADEMA je walipokuwa CHADEMA waliwahi kutumia vikao vya chama kuonesha wizi huo na jinsi unavyofanyika?

Wapumbavu wawili wakutanapo huwa chukizo mbele za Mungu. Wapo wanaowapongeza wanaotoka CHADEMA kwa ujasiri wakati wapongezaji hawana muda wa kutaka kujua kama wanachoambiwa kina ukweli wowote ule!!
Hakuwai kuuubali ukweli toka nimekufahamu,Nani asiejua kua uko pale ufipa unaongoza kundi la vijana linalomsifia DJ mbowe pamoja na kumtukana muheshimiwa rais,wakati mwingine Jambo linapozungumzwa jaribu kutumia akiri kulitafakari sio unapinga pinga mbwa wewe wa ufipa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wakati kulikuwa na shida sana ya usafiri. Basi likija mijitu ya miraba minne huwasukuma wanyonge nao wakaingia kwenye basi bila shida. Polisi wakaja utaratibu wa kuingia kwa foleni ikasaidia kidogo lakini haikuwa wakati wote.
Siasa za Tz kwa ni za kibabe mwenye nguvu tu ndiye atakayeingia. Ama uungane na mwenye nguvu au wewe mwenyewe upige tizi.
Tunategema chombo fulani kiseme tuingie kwa foleni (tume). Demokrasia itamalaki la sivo paka wataendelea kuhamia jikoni inakoungwa mboga!

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Akiri ndio nn?kwa msaada wa kuandika mtafute yule bb kizee chenu kilichopo hapo Lumumba
Hakuwai kuuubali ukweli toka nimekufahamu,Nani asiejua kua uko pale ufipa unaongoza kundi la vijana linalomsifia DJ mbowe pamoja na kumtukana muheshimiwa rais,wakati mwingine Jambo linapozungumzwa jaribu kutumia akiri kulitafakari sio unapinga pinga mbwa wewe wa ufipa

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom