CHADEMA yavifunika vyama vyote vya siasa nchini

CHADEMA yavifunika vyama vyote vya siasa nchini

Masusu
WanaJF,

Msingi wa hoja yangu upo kwenye hali halisi ya mambo ya siasa yanavyoendelea hapa nchini; CHADEMA imevifunika vyama vyote kwa umarufu na kuteka mioyo ya watu

1. Si jambo la kupinga , kiongozi wa CHADEMA hususani Mwenyekiti na Katibu ni karibu watanzania wote wanafuatilia ratiba zao za kikazi wanapenda kujua wako wapi na wanafanya nini kwa wakati huo, tofauti pengine ilivyo hata kwa Rais na waziri Mkuu, uthibitisho ni vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo na mitandao ya kijamii

2. Ni chama pekee ambacho kwa kipindi kama cha miaka miwili mfululizo kinaandikwa sana kwenye vyombo vya habari,bungeni na kwenye mitandao ya kijamii

3. Ni chama ambacho nguvu ya kukihujumu imetumika nyingi sana lakini bila mafanikio tofauti na vyama vingi vya upinzani vilivyowahi kutokea hapa Tanzania

4. Ni chama pekee cha siasa kinachoweza kuthubutu kufanya maamuzi magumu, rejea kufukuza madiwani wasaliti Arusha na kutetea viti vyote kwenye uchaguzi wa madiwani

5. Ni chama kilichobebeba Uzalendo wa kweli na hakina unafiki

6. Mwisho ni chama kinachoenda kuandika historia ya kukiondoa chama tawala kikongwe madarakani 2015, kwa maana kuna kila dalili kuwa sasa CCM haina uwezo wa kupambana na chama kilichojaa watu wanaojitambua
 
Mkuu! Mbona sifa sots unazosema ni mtaji wa ccm? Tumekuwa tukiona jinsi Jk anavyopanga safu yake kwa mwelekeo wa kidini lakini pia propaganda za kidini zilivyoota ndani ya ccm na serikali yake walivyoshindwa kushighulikia tatizo la uchinjaji wa kitoweo,suala la shehe ponda na mengine mentioned,jumlisha kashfa za kingono za mwigulu,kapuya,nape na wengine wengi ndani ya ccm.
Kinana kaa mbali na tembo,ccm ni janga kwa mustakabali wa Taiga.

Sasa bandugu kwahiyo kama mwenzio kajinyea we ndo uharishe au!??. Ccm ndo role model wenu!??. Najua wewe ni mwanaChagadema, Aah samahani i mean mwanaChadema.Lakini kama mnataka kuwa-replace CCM madarakani inawalazimu kutokuwa na madhaifu yao!, SWALI NAKUULIZA Kwanini niipigie kura Chadema iongoze nchi hii, ikiwa ina mafisadi kama ccm, uzinzi kama ccm, udini kama ccm, uchu wa madaraka kama ccm. bora ccm ikae madarakani hadi chama m'badala kitakapopatikana mana nchi haiwezi kuwa bila uongozi. Chadema imepoteza uhalali wa kui-replace ccm madarakani.
 
Duh! kweli cdm yafunika vyama vyote? Ina maana: 1 rais anatoka cdm! 2 asilimia ya wabunge wengi wanatoka cdm! 3 cdm inawanachama wengi kuliko vyama vingine! Dah! bila shaka wanakufirimba.

Santeeeeee!
 
Ni kweli kabisa cdm iko katika moyo wa kila mtanzania anayetaka mabadiliko ya kweli ya kuondakana na mafisadi sisiem,nikiwa kwenye maombi jana ,nimeoteshwa kuwa cdm ipo kwenye pepeto kuu,Mungu anapepeta magugu na ngano,lazima ngano safi ibaki

Ila mi nimeoteshwa kwamba katika pepeto kuu, wavu utatoboka na magugu, ngano safi vyote vitamwagika kwenye mchanga.
 
Kujitambua kwa kuwa na wafuasi wahuni ambao wapo kwasababu ya mtu fulan....kwa hali hii ya kufukuzana itabaki kma ndoto ya Ali nacha ya kutaka kuwa raic wkt 4m4 ana zero
 
Watu wanasahau kuwa Chadema ina miaka karibu ishirini sasa ...na ilishuhudia hujuma zote zilizofanywa kwa vyama vingine, ambavyo vilikuwa na nguvu kutokana na umaarufu wa Viongozi wake. Ukiwa na kiongozi maarufu kuliko nia ya chama kuwasaidia wananchi, ni rahisi sana kukihujumu chama hicho. Maana wananchi wanakuwa hawaelewi nia ya chama kwao bali wanaelewa umaarufu wa kiongozi. Umaarufu wa kiongozi ukipotea na chama kinapotea kwa wananchi. Nia ya chama siyo rahisi kuipoteza ikishakuwa maarufu na kujulikana sawia kwa wananchi.

Hili Chadema waliliona mapema wakaweka msingi imara wa kufuata miiko ya uongozi wa chama kwa kutumia katiba ya chama na taratibu nyingine za chama. Vyote hivi vinaheshimiwa ndani ya chama, na vinasaidia sana kuipa NIA ya Chadema ya kuwaletea wananchi maendeleo kwa kufuata misingi ya kidemokrasia umaarufu hivyo kutambulika kwa wananchi kirahisi.

Kosa la kiongozi kuwa maarufu kuliko nia ya chama liliwapata NCCR-Mageuzi,kwa Mrema kuwa maarufu na kutumia umaarufu huo kukiua chama, hata alipoenda TLP... kinachojulikana sasa ni Mrema zaidi ya nia ya Chama cha TLP kwa wananchi. Kutokana na hilo pale TLP wala hakuna hata dhamira thabiti ya kuchukua dola. Nia ya TLP siyo maarufu kwa wananchi kwa namna kinavyoendeshwa hivyo si rahisi kupewa dola.

CUF...ilikumbwa na hilo pia Maalim Seif na Prof. Lipumba wamekuwa maarufu kuliko chama na hili limefanya umaaruf wao uipoteze CUF kwenye siasa za ushinda kuchukua dola. Mnajua kilichotokea Zanzibar 2010....Lipumba aliyasema yote kwenye ile video aliyorekodiwa Msikini Dar es Salaam. Nia ya CUF siyo maarufu kwa wananchi, Pale maarufu, ni Maalim Seif na Lipumba, na Hamadi Rashid alitaka kuleta mabadiliko ya kuondoa umaarufu wa viongozi pale CUF (sina hakika kama alitaka kujenga umaarufu wa nia ya CUF kwa wananchi ama la) kilichompata sote tunakijua.

Chadema waliamua kujifunza kutokana na makosa ya wenzao vizuri sana, ndiyo maana...hakuna mtu kuwa maarufu kuliko nia ya chama ya kuwaletea wananchi maendeleo kwa njia ya kidemokrasia. Nia hii ya chama ndiyo iliyo maarufu pale Chadema. Na ni kwa umaarufu wa nia Chadema kwa wananchi...watanzania wengi wanakiunga mkono chama hicho japo wengine wanakiunga mkono kwa kujificha.
Mkuu uchambuzi mzuri sana
 
Siyo siri, CHADEMA inawaacha wengi hoi. wengi wanaipenda na kuna wengine wengi inaowanyima usingizi. zote hizo ni athari za CHADEMA. Pia kuna wengi ambao wanaitakia mema, wanaishauri isibweteke na sifa, ikumbuke kwamba kuna fisi anayefuatilia mkono unaokwenda mbele na kurudi, akitumaini kwamba utaanguka. tatizo ni kwamba fisi anaweza kuamua kuurukia mkono ule na kuung'ata. na kwa kuwa fisi ana mataya yenye nguvu sana, kwake kuukata mkono sio tatizo. kwa hiyo iko haja ya kuchukua tahadhari. mimi nawafurahia sana wale ambao wanapenda kutoa CONSTRUCTIVE CRITICISM. na ningeomba uongozi uwe unafuatilia kwa karibu sana ushauri wa aina hiyo. hata maadui wake, CHADEMA iwasikilize sana, isiwapuuze. kutokana na shutuma mbalimbali na hata matusi, CHADEMA wanaweza kupata pointi za kuwafanya wasonge mbele zaidi.
CDM nawaona wakifuata huu ushauri kwa vitendo kwani huko Kigoma the REAL DR. P.W. SLAA ALIWASIHI POLISI WASIWAZUIE WALA KUCHANA MABANGO YA WALIOKUWA WAMETUMWA KUCHAFUA MKUTANO ILI WAFIKE MBELE YAKE WASEME YA MOYONI.
 
MSALANI wacha unafiki, mnauwa watu eti CHADEMA tumejirushia mabomu??
Huna hata aibu muuwaji mkubwa wewe!!
Hufai shetani mkubwa, Mungu at
atulipia!!
 
Last edited by a moderator:
ccm ni chama chakafu kimeshakufa chadema ni chama makini sana tuombe uzma 2015 ccm ndo maziko ya ccm chama cha mafisadi; wauaji wakubwa ;wakabakaji vp kapuya yuko wapi
 
MSALANI wacha unafiki, mnauwa watu eti CHADEMA tumejirushia mabomu??
Huna hata aibu muuwaji mkubwa wewe!!
Hufai shetani mkubwa, Mungu at
atulipia!!
Mkuu unatokwa na povu bure! viongozi wenu wamesema wana ushahidi wa DVD inayomuonyesha muuaji, kwanini hawaipeleki panapohusika ili ajulikane? na sheria ichukue mkondo?
 
MSALANI wacha unafiki, mnauwa watu eti CHADEMA tumejirushia mabomu??
Huna hata aibu muuwaji mkubwa wewe!!
Hufai shetani mkubwa, Mungu at
atulipia!!

Mkuu! Achana na hawa misukule wa mafisadi.......vijana wadogo kabisa lakini mawazo yao ni mafupi utafikiri wanapigiliwa mchana kweupe!
Wasikupe homa hata kidogo Mtumishi Wetu.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu unatokwa na povu bure! viongozi wenu wamesema wana ushahidi wa DVD inayomuonyesha muuaji, kwanini hawaipeleki panapohusika ili ajulikane? na sheria ichukue mkondo?
Wamesema hawawezi kuutoa ushahidi mpaka rais aunde tume wanajua kabisa rais hawawezi kupangiwa kazi na kina Lema.
 
WanaJF,

Msingi wa hoja yangu upo kwenye hali halisi ya mambo ya siasa yanavyoendelea hapa nchini; CHADEMA imevifunika vyama vyote kwa umarufu na kuteka mioyo ya watu

1. Si jambo la kupinga , kiongozi wa CHADEMA hususani Mwenyekiti na Katibu ni karibu watanzania wote wanafuatilia ratiba zao za kikazi wanapenda kujua wako wapi na wanafanya nini kwa wakati huo, tofauti pengine ilivyo hata kwa Rais na waziri Mkuu, uthibitisho ni vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo na mitandao ya kijamii

2. Ni chama pekee ambacho kwa kipindi kama cha miaka miwili mfululizo kinaandikwa sana kwenye vyombo vya habari,bungeni na kwenye mitandao ya kijamii

3. Ni chama ambacho nguvu ya kukihujumu imetumika nyingi sana lakini bila mafanikio tofauti na vyama vingi vya upinzani vilivyowahi kutokea hapa Tanzania

4. Ni chama pekee cha siasa kinachoweza kuthubutu kufanya maamuzi magumu, rejea kufukuza madiwani wasaliti Arusha na kutetea viti vyote kwenye uchaguzi wa madiwani

5. Ni chama kilichobebeba Uzalendo wa kweli na hakina unafiki

6. Mwisho ni chama kinachoenda kuandika historia ya kukiondoa chama tawala kikongwe madarakani 2015, kwa maana kuna kila dalili kuwa sasa CCM haina uwezo wa kupambana na chama kilichojaa watu wanaojitambua
Chadema ikulu 2015.....chadema idumu
..
 
Ata Ze comedy inafunika vipindi vyote ,na chadema ni wasanii kiana yake ! Kutolewa mzobemzobe bungeni, makonde yaani unaweza kuhesabu tu !
 
Huu uzi umetulia. ccm-chama cha magaidi kazi yao ni kununua watu na kuwavisha mabomu ili waje kulipua vyama vingine ila kwa rehema za Mungu chadema ina spiritual sensitivity.
 
Nakupongeza sana mleta mada, kitu imetulia Nchemba na Nape wakikatiaha miguu yao hapa usiku hawatalala aiseeeeeeee
 
Na hili nalo watabisha sana sababu wanaasili ya ubishi kwa kila chembe yao ya mwili
 
Uko sawa kabisa!!! Sio kuvuma tu tunataka kuchukua dola
 
Back
Top Bottom