CHADEMA yaumbuka Geita mjini

CHADEMA yaumbuka Geita mjini

Kinana ni sawa na nzi mbona yy hajtaj ktk sakata la kuuza pembe za ndovu? Na hajawah kukanusha!
 
Sasa chadema imeumbuka wapi? Mfamaji haachi kutapatapa et krt inaongoza kwa rushwa. Nenda kajipange kwanza mkuu.
 
Ukisoma kwa makini utagundua kuwa CCM ,viongozi na wanachama wake ndio walioumbuka
 

  • Katibu Mkuu huyo wa CCM amesema kuwa CHADEMA wamekuwa na tabia ya kudanganya wananchi, ambapo M/kiti wao Mhe Mbowe alidanganya kuwa anarudisha gari ya KUB lakini ukweli ni kuwa gari hiyo anaitumia mpaka hivi sasa na anaitumia kufanyia magendo ambapo iliwahi kukamatwa nchini Kenya, pia ametaja kuwa Halmashauri ya Karatu inayoongozwa na CHADEMA inaongoza kwa rushwa na ufisadi wa zaidi ya Bilioni 2.

    Ikiwa kweli katamka haya basi hakika siasa na wanasiasa ni wa kushangaza! Mtanzania tena kiongozi anatumia chombo cha umma kufanya magendo nje ya mipaka yetu na bado anatembea huru! Na nayeyasema hayo ni kiongozi ambaye mara kadhaa anadai anaweza kuwaagiza serikali kushughulikia masuala yanayowakera wananchi - alisema haya hata katika mkutano huu kwa kuahidi kuwapa wachimbaji wadogo wadogo wa madini maeneo sanayoyadai!​








 
Msingi wa CHADEMA ni ulaghai, Hawana budi kuumbuka sasa, Wananchi wa leo wanafahamu ukweli wote.

wamekulaghai na nini?wanaowalaghai ndio mnawakumbatia we ni nonsens fo sure embu subiri oktoba japo mnafny kila liwezekano mijin watu wasijiandikishe
 
Miaka ya kuishi kijanja janja imeisha, watanzania wanajua ukweli.
Hawana muda wa kudanganywa tena, wamechoka kudanganywa. Michezo ya kisiasa ya kutangaza kuacha kutumia garoi la KUB wakati watu wanakuona nalo mtaani, si tu yanaondoa hadhi na heshima bali yanawaonyesha watanzania kuwa hawawezi kukuamini tena kwa namna yeyote.
 
AHADI - ALIITOA AKIWA WAPI...

Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
Kulinda haki za walemavu - Makete
Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha
Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara
Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha
 
katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndg Abdulrahman Kinana amewaumbua wanachama na viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya kusema kuwa Viongozi wa Chama hicho wanatoa ahadi feki na matumaini hewa kwa wananchi wakati hawana uwezo wa kufanya maamuzi yeyote kwani Serikali iliyopo ipo Chini ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ndicho chenye uwezo wa kufanya maamuzi ya kusaidia wananchi.


Kinana ameyasema hayo leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Nyangumbu - Geita mjini, ambapo amesema kuwa Viongozi wa CHADEMA wamewalaghai wananchi wa Kijiji cha Mgusu kwa kuwakataza kupokea fedha ya ruzuku kutoka Serikalini kiasi cha Bilioni 3.4 kwa wachimaji wadogo, wakiwadanganya kuwa wakipokea eneo lao litachukuliwa.


Katibu Mkuu huyo wa CCM amesema kuwa CHADEMA wamekuwa na tabia ya kudanganya wananchi, ambapo M/kiti wao Mhe Mbowe alidanganya kuwa anarudisha gari ya KUB lakini ukweli ni kuwa gari hiyo anaitumia mpaka hivi sasa na anaitumia kufanyia magendo ambapo iliwahi kukamatwa nchini Kenya, pia ametaja kuwa Halmashauri ya Karatu inayoongozwa na CHADEMA inaongoza kwa rushwa na ufisadi wa zaidi ya Bilioni 2.

Dah! chama kikiongozwa na mwenyekiti Criminal ni shida! Haya huyo msaidizi wale Lema naye yuko ndani! unategemea nini hapo!
 

Attachments

  • 1434827368141.jpg
    1434827368141.jpg
    20.4 KB · Views: 121
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom