CHADEMA yaumbuka Geita mjini

CHADEMA yaumbuka Geita mjini

ray jay

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2011
Posts
1,084
Reaction score
485
katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndg Abdulrahman Kinana amewaumbua wanachama na viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya kusema kuwa Viongozi wa Chama hicho wanatoa ahadi feki na matumaini hewa kwa wananchi wakati hawana uwezo wa kufanya maamuzi yeyote kwani Serikali iliyopo ipo Chini ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ndicho chenye uwezo wa kufanya maamuzi ya kusaidia wananchi.

Kinana ameyasema hayo leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Nyangumbu - Geita mjini, ambapo amesema kuwa Viongozi wa CHADEMA wamewalaghai wananchi wa Kijiji cha Mgusu kwa kuwakataza kupokea fedha ya ruzuku kutoka Serikalini kiasi cha Bilioni 3.4 kwa wachimaji wadogo, wakiwadanganya kuwa wakipokea eneo lao litachukuliwa.

Katibu Mkuu huyo wa CCM amesema kuwa CHADEMA wamekuwa na tabia ya kudanganya wananchi, ambapo M/kiti wao Mhe Mbowe alidanganya kuwa anarudisha gari ya KUB lakini ukweli ni kuwa gari hiyo anaitumia mpaka hivi sasa na anaitumia kufanyia magendo ambapo iliwahi kukamatwa nchini Kenya, pia ametaja kuwa Halmashauri ya Karatu inayoongozwa na CHADEMA inaongoza kwa rushwa na ufisadi wa zaidi ya Bilioni 2.

7.jpg

Katibu Mkuu akihutubia maelfu ya wananchi wa Geita mjini katika uwanja wa Nyangumbu

3.jpg

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Kalangalala, Nyankumbu Geita ambapo aliwata wananchi hao kutokubali kuyumbishwa na vyama vilivyopoteza muelekeo.

2.jpg

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Geita Mhe.Vicky Kamata akihutubia wananchi wa Geita.
 
Mfa Maji na Chama Chake Cha Mafisadi (CCM), Haachi Kutapatapa. Hivi Wizi na Ufisadi unaofanywa na CCM Kweli una Mfano wake kwa Vyama Vya Upinzani.
 
Hizi tuhuma nzito sana, bil tatu! Zilitolewa lini na kwa budget ipi? Cdm msipojibu hili basi tutajua zilishapigwa juu kwa juu sawa na za viwanja kule mwanza.
 
Ni uongo mtupu hakuna cha chadema kuumbuka pamoja na kuleta baiskeli lakini wananchi wa geita wamemdhihirushia kwamba chadema ni chama pendwa
 
Wameumbuka wapi sasa??? Ni kwrli serikali inaongozwa na Ccm lakini Ccm ndio wametufikisha hapa yulipo hata mlo wa siku ni issue!! Dollar sasa ni 2300/ bado mnajigamba kwa upuuzi?? Mawaziri wote wamekimbia bungeni bado ni uongozi huo?? Kuwa rais unatakiwauwe na 1st degree mnamuyzia mkulima darasa la saba form?! Wezi nyie??? Sasa hii ni Tanzania sio bla blaaa. Mmekwisha Ccm. Hamna sera wala pa kutokea I ache zen na fisi.
 
Sasa hapo wameumbuka vipi ewe think tank wa CCM?
 
Kinana hana jipya watia nia wake wote mafisadi lowassa kawashinda utawaweza chadema? Mkuu hangaika Na mafisadi wako waliowadhurumu watanzania Mali zao
 
Jifunze kwanza kuandika kwa nukta kwanza,ndio ulete uongo wako wa lumumba hapa.
 
Eddy hata wewe mafisadi wenu wanataka uraisi wakiongozwa Na papa lao EL mwambie Kinana kajaribu kukata jina EL msikie mziki wake achana Na chama dume cdm
 
Wameumbuka wapi sasa??? Ni kwrli serikali inaongozwa na Ccm lakini Ccm ndio wametufikisha hapa yulipo hata mlo wa siku ni issue!! Dollar sasa ni 2300/ bado mnajigamba kwa upuuzi?? Mawaziri wote wamekimbia bungeni bado ni uongozi huo?? Kuwa rais unatakiwauwe na 1st degree mnamuyzia mkulima darasa la saba form?! Wezi nyie??? Sasa hii ni Tanzania sio bla blaaa. Mmekwisha Ccm. Hamna sera wala pa kutokea I ache zen na fisi.

1USD= Tzs2323.38
 
wameumbuka wapi,kwa kauli ya majukwaa ya siasa?
this is so pathetic Kama unaweza kudanganyika na kauli cheap Kama hizi then you are too shallow in thinking.
 
Hakuna mtu anaye walaghai wananchi kama Kinana. lla sema kwa sababu wananchi wengi hawajitambui wanadiriki kupoteza muda kuwasikiliza manabii wa uongo wa CCM....!!
 
Back
Top Bottom