Elections 2010 CHADEMA yatoa tamko: Hatumtambui Kikwete kama rais

Ninachokiona hapa, watu wataanza kushindwa kumtofautisha Slaa na Lyatonga Mrema. Kama kweli hamtambui Rais awaambie wabunge wake wasiingie bungeni kama walivyofanya wenzao wanaume CUF 1995-2000.
 
On the Chadema's stand over President Kikwete's win, Judge Werema said Chadema's decision was ‘nonsense'. (Ni mawazo na msimamo wa kijinga na kipumbavu kutomkubali Rais)


Huyu ni AG kweli ?

Hata mimi nilikuwa nalishangaa hili, huyu AG hajui kwamba kuna recent precedent events za namna hii? We saw it in Zanzibar, Kenya and Zimbabwe. Well mwisho wa siku ndiyo wameibuka na hizi the so called GNU's. Ukisoma hii na ile ya kuiandikia NEC wakati wa uchaguzi malalamiko kuhusu CHADEMA unapata picha huyu jamaa ni mtu wa namna gani!
 
All in all, JK sasa atatambua nini maana ya kufake demokrasia wakati huohuo unategemea misaada kuendesha nchi!
 
Huyo anayeona Dr. Slaa hafai amepotoka akili na ni maskini wa akili na asiyetaka mabadiliko. Tuwe na umoja tz tupinge kwa nguvu zetu zote udhalimu wa Ccm. 2015 for CHADEMA.
 
Wewe, katika nchi ambayo ina watu kama wewe, kutofautina matokeo ni kitu cha kawaida kabisa. Huwezi ukapata exact figures za Kigoma,mwanza, mbeya, Tanga na mikoa yote nchini na zile zitakazokuwa tume. Isitoshe tume inaweza kufanya masahihisho kurekebisha yale makosa yaliyotokea vituoni. Hicho kitu kiko all over the world, si TZ tu.
So this is a justification of whateva messy the election results are?

Ni ngumu sana kufanya majadiliano ya hoja kwa mtu anayeamini namna hii!!!!!!!!!! Huu unazi haisadii chochote Tanzania na hautaipeleka popote.
 
KUMTAMBUA KIKWETE NA SERKALI YAKE NI KUISALITI NGUVU YA UMMA,SERKALI YAKE ITAKUWA YA HILA KAMA YEYE ALIVYOINGIA MADARAKANI KWA HILA,AKIJUA SASA ANAO WAKATI MFUPI KABISA YEYE MWENYEWE NA CCM YAKE KUFANYA DHULUMA KWA WATANZANIA.:israel:
 
Kikwete ni rais wangu na wenu ninyi wote ndani ya jf, mpende msipende.
Nguvu ya umma ndio iliyomuweka madarakani
nguvu ya umma ndiyo iliyowapa ubunge wabunge 22 wa chadema
 
Kama CHADEMA hawamtambui Rais:
1. Watashiriki kupiga kura za kumpitisha/kutompitisha waziri mkuu? Waziri mkuu hupendekezwa na Rais, kushiriki katika kumpigia kura ni kutambua huyo aliyemleta ni Rais halali.

2. Baada ya waziri mkuu kupitishwa, wataweza kumuuliza mwaswali yeye pamoja na mawaziri wengine, ambao wote wameteuliwa na Rais wasiyemtambua?

Ndugu zangu wana JF, tamko hili la CHADEMA ni la kisiasa tu na halitekelezeki. Sababu kubwa ni kwamba wabunge wa CHADEMA hawawezi kugive-up ubunge wao - kwa katiba ya Tanzania kama humtambui Rais huwezi kuwa mbunge.
 
Kama CHADEMA hawamtambui Rais:
1. Watashiriki kupiga kura za kumpitisha/kutompitisha waziri mkuu? Waziri mkuu hupendekezwa na Rais, kushiriki katika kumpigia kura ni kutambua huyo aliyemleta ni Rais halali.

2. Baada ya waziri mkuu kupitishwa, wataweza kumuuliza mwaswali yeye pamoja na mawaziri wengine, ambao wote wameteuliwa na Rais wasiyemtambua?

Ndugu zangu wana JF, tamko hili la CHADEMA ni la kisiasa tu na halitekelezeki. Sababu kubwa ni kwamba wabunge wa CHADEMA hawawezi kugive-up ubunge wao - kwa katiba ya Tanzania kama humtambui Rais huwezi kuwa mbunge.

Nakubaliana na wewe hili linaweza kuwa tamko la kisiasa lakini lina impact.

Mkuu tukumbushane kidogo, CUF walipomkataa Karume walishiriki vp kwenye serikali yake, Tsvangirai Vs Mugabe wameenda enda vipi mpaka sasa? na pia what transpired between Odinga na Kibaki. Kiukweli none of the mentioned models ni attractive kwa Tanzania yetu lakini probably kukataliwa is the only language watawala wa kiafrika dhalimu na walioinghia madarakani kiuchakachuaji inawafanya wasikie . The other option ni vurumai which is not a good one.

Otherwise it's just business as usual.
 
kaongea Point moja tu hapo, kubadilisha katiba. Mengine yote yote upupu mtupu na amechelewa sana. Kubadilisha katiba naunga mkono
 
Ebu nielimishe zaidi. Kifungu hicho hapo juu hakisemi ni uchaguzi upi, wa raisi au wa wabunge. Inaoenekana unaweza kwenda mahakamani ku challenge uchaguzi wa wabunge ingawa sijui ni wapi katiba inasema specifically kuhusu wabunge. Swali langu kuhusu uchaguzi wa raisi ni hili:

Is there a constitutional provision that explicitly states that the results of a presidential election - as opposed to parliamentary elections - are final, and can not be challenged in court, after they are announced by the electoral commission?

Nachofahamu hakuna kifungu kilicho moja kwa moja kinachokataza kesi dhidi ya matokeo ya urais. Ila kifungu 74(12) hutumika kuvunja nguvu ya mahakama kuu (actually mahakama yoyote) kujadili maamuzi ya NEC. Suala la matokeo ya wabunge linapelekwa mahakamani kwa kuwa matokeo ya ubunge yako chini ya Wakurugenzi wa Halmashauri, NEC hapa huwa overseer tu. Ila popote ambapo NEC ndo inatoa matamko aidha katika mgawanyo wa majimbo ((75(6)) na matokeo (inatoa ya urais) basi mahakama zimenyimwa uwezo wa kujadili.
 
Nakubaliana na wewe hili linaweza kuwa tamko la kisiasa lakini lina impact.

Mkuu tukumbushane kidogo, CUF walipomkataa Karume walishiriki vp kwenye serikali yake, Tsvangirai Vs Mugabe wameenda enda vipi mpaka sasa? na pia what transpired between Odinga na Kibaki. Kiukweli none of the mentioned models ni attractive kwa Tanzania yetu lakini probably kukataliwa is the only language watawala wa kiafrika dhalimu na walioinghia madarakani kiuchakachuaji inawafanya wasikie . The other option ni vurumai which is not a good one.

Otherwise it's just business as usual.

Unachosema ni sahihi kabisa, lakini usahihi wake utakuwepo pale tu ambapo kutakuwa na mikakati mingine zaidi ya kutokumtambua Rais. Na mikakati hiyo ni lazima iwe communicated kwa wanaounga mkono chama. Kwa jinsi mambo yanavyoenda sasa naona viongozi wa CHADEMA wanasherehekea "ushindi" tu na kama kuna mikakati basi wameamua iwe ya siri. Katika hiyo mifano mizuri uliyoitoa, hakuna hata sehemu moja ambapo wananchi waliachwa pembeni; actually dunia nzima ilijulishwa kinachoendelea, unlike our case.
 
So this is a justification of whateva messy the election results are?

Ni ngumu sana kufanya majadiliano ya hoja kwa mtu anayeamini namna hii!!!!!!!!!! Huu unazi haisadii chochote Tanzania na hautaipeleka popote.

Nyambala nakuheshimu sana hoja zako. Si kwa unazi wala ukereketwa mkuu, ila nakukumbusha na nitaendelea kukukumbusha daima, kuwa huwezi kujadili baada namna ya kuchota maji yaliyomwagika mchangani. haiwezekani na ni kichaa hicho. Kilichotakiwa ni kuzuia maji yasimwagike. Muda. Haupo tena, sasa hivi ni kelele tu na zitapigwa sana hakuna results za maana. Nakuhakikishia. Tujadili mambo ya akili. mambo ya katiba mpya. Kuanzia sasa. Hamna njia nyingine yoyote.
 
Kwa Kauli ya Dr Slaa Nanukuu hapa (kisheria na kikatiba, hautoi nafasi kupinga matokeo ya uchaguzi katika mahakama au chombo kingine kinachoundwa kikatiba.

Alisema NEC inalindwa kisheria na hata kama inachakachua matokeo ya uchaguzi kwa makusudi kwa lengo la kumnufaisha Rais Kikwete na chama chake)

Basi kuna haja ya Kuunda sheria na Katiba ya Nchi Upya au ifanyiwe hiyo sheria ya kikatiba Marekebisho sio tu kumlinda mtu mmoja aliye Madarakani itabidi hili suala lizungumziwe kwenye kikao kijacho cha Bunge. Mnasemaje Wakuu wenzangu?
 
Atamtambuaje mwizi, ukimshika mtu ugoni halafu mjumbe anakuja na kusema huyo sio mgoni utakubali vipi? JK kashikwa pabaya na Chama Chake Cha Majambazi.
 
kaongea Point moja tu hapo, kubadilisha katiba. Mengine yote yote upupu mtupu na amechelewa sana. Kubadilisha katiba naunga mkono

Ukikubali kwamba kubadilisha katiba ni muhimu ili kuwe na mchakato wa uchaguzi ulio wa huru na haki, huna budi kukubali kwamba hili linatokana na ukweli kwamba sheria za uchaguzi, ambazo msingi wake ni katiba, nazo ni mbovu. Kwa maana nyingine, huwezi kukubali kwamba katiba ni mbovu, halafu akaja mtu kupinga kuanzia sheria za uchaguzi mpaka katiba, halafu wewe ukasema kupinga sheria dhalili za uchaguzi zinazotokana na katiba dhalili ni upupu. Utakuwa unajikanganya mwenyewe.

Nakubali kwamba msingi wa matatizo yote ni katiba, katiba inayompa rais mkono wa chuma sawa na Draco au Hammurabi na uhuru wa kisultani. Lakini hili halina maana kwamba mtu hawezi kuanza kuonyesha ubovu wa katiba kwa kuangalia sheria zinazotokana na katiba hiyo na kupanda juu mpaka kufikia kwenye katiba.

Kama mfalme yuko uchi, ashakum si matusi, mtu hashindwi kuanza kwa kusema kwanza hajavaa viatu, kisha hana hata soksi, tena suruali hana, he hata kaptula hana, na kutoka hapo kusema kumbe hata shati wala nguo za ndani hana.

Si lazima mtu aende moja kwa moja kwenye ubovu wa katiba, mwingine anaweza kutaka kufundisha ubovu wa katiba unaathiri vipi maisha ya kila siku, na hivyo kuona bora aanze kwa kuonyesha ubovu wa athari za katiba kwatika sheria zinazotumika kila siku.

Napenda wananchi wanapoeleweshwa kwa nini ni muhimu kubadilisha katiba kwa kupitia mambo yanayoathiri maisha kila siku kama hivi. La sivyo wengine wanaweza kuona mabadiliko ya katiba ni kama zoezi fulani la constitutional lawyers na madokta fulani hivi tu.

Kwa hiyo, tunapoongelea katiba dhalili, ni muhimu tuelewe kwamba katiba dhalili ni mzizi unaozaa matunda ya sheria dhalili, na mara nyingi kuwaonyesha watu mzizi si kitu rahisi kama kuwaonyesha watu matunda. Kwa hiyo yeyote anayeweza kuwaonyesha watu uhusiano wa matunda dhalili na mzizi dhalili anakuwa amefanya kazi nzuri na kamwe hatakiwi kuitwa amesema "upupu".

Labda kwa wale wenye pupa tu.
 
Wewe, katika nchi ambayo ina watu kama wewe, kutofautina matokeo ni kitu cha kawaida kabisa. Huwezi ukapata exact figures za Kigoma,mwanza, mbeya, Tanga na mikoa yote nchini na zile zitakazokuwa tume. Isitoshe tume inaweza kufanya masahihisho kurekebisha yale makosa yaliyotokea vituoni. Hicho kitu kiko all over the world, si TZ tu. Hii ni tatizo la miundo mbinu. Kama kuna wizi vituoni, hilo ni suala lingine litatokana na uzembe wa vyama vya siasa kubweteka na ni funzo kwa 2015.
Ninapokuambia maelezo yako ni upupu nina maana kuanza kuchachamaa sasa hivi ati matokeo yamechakachuliwa na ili hali ulijua uwezekano huo hata kabla ya uchaguzi ni upuuzi mkubwa sana.
Sijajua wewe uchungu wako ni upi? Kwamba ulikuwa ni lazima upate unachokitegemea na hukubali kilichopo au ni mkereketwa kama mashabiki wa mpira wa simba na yanga ambao siku zote wanajua team zao zinatakiwa zishinde na zikishindwa anafukuzwa mwenyekiti?! Na ushindwe ulegee mpaka ufe.

Kanyafu hapo kwenye red una suggest kuwa CCM si waaminifu?
 
Achana na kumtambua mimi simtaki

Hata Masai wa Loliondo ndio kabisa utasikia Heroo hiii Jakaye nafanya sisi laiyoni, yaani wanatema mate chini kuonyesha dharau na hasira waliyonayo kuhusu waarabu walivyo wachomea maboma, wee acha tu, JK = NEC President
Dr Slaa = PEOPLES' PRESIDENT,
 
Back
Top Bottom