William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,588
- 10,375
Kama CHADEMA hawamtambui Rais:
1. Watashiriki kupiga kura za kumpitisha/kutompitisha waziri mkuu? Waziri mkuu hupendekezwa na Rais, kushiriki katika kumpigia kura ni kutambua huyo aliyemleta ni Rais halali.
2. Baada ya waziri mkuu kupitishwa, wataweza kumuuliza mwaswali yeye pamoja na mawaziri wengine, ambao wote wameteuliwa na Rais wasiyemtambua?
Ndugu zangu wana JF, tamko hili la CHADEMA ni la kisiasa tu na halitekelezeki. Sababu kubwa ni kwamba wabunge wa CHADEMA hawawezi kugive-up ubunge wao - kwa katiba ya Tanzania kama humtambui Rais huwezi kuwa mbunge.
- Great post bro!, Chadema wamefanya kazi nzuri sana kwenye huu uchaguzi kwa sababu wame-expose weaknesess za uongozi wa CCM kila kona kitu ambacho kitawapa nafasi CCM kujirekebisha au huenda ukawa ndio mwisho wa empire,
- Binafsi siamini kwamba Chadema watasimamia msimamo wa kutomtambua Rais aliyeapishwa tayari, kwa sababu itaishia kuvuruga kazi kubwa na nzuri waliyoifanya tayari, kwa maoni yangu ni kwamba kwa msimamo kama huu watakuwa wanajitafutia un-necessary national political attention ambayo itawapa mwanya maadui wao kisiasa kuwaingia kati kati, kuwagawa na wataishia kufarakana kama enzi za TLP na NCCR na CUF kule visiwani
- Chadema chonde chonde wananchi tunwahitaji sana sasa kuliko wakati wowote uliopita, kumkosesha tembo usingizi huu mwendo wa kutotambuana haujakaa sawa!
William.