Malafyale
JF-Expert Member
- Aug 11, 2008
- 13,813
- 11,126
CHADEMA ina wabunge wa kuchaguliwa na kuteuliwa na wote waliapa mbele ya Spika kuwa "watatii sheria za Jamhuri ya Muungnao wa TZ";kwa kiapo hicho si ni wazi basi wametambua na wametii mamlaka tatu za dola ambazo ni Rais,Bunge na Mahakama au mimi ndiyo sipo sahihi?Je ina maana sasa Wabunge wa CHADEMA hawatachukua posho na mishahara itolewayo na serikali inayoongozwa na Rais wasiyemtambua?Au hawamtambui tu Rais lkn wanazitambua posho na mishahara inayotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu-mamlaka ya Bunge?
Kama tunakumbuka vyema kule ZNZ baada ya uchaguzi wa mwaka 1995 chama cha CUF kilisusia matokeo na hakikumtambua Rais Salmin kama Rais halali wa ZNZ kulikopeleka uongozi wa juu wa CUF kuwapiga marufuku Wawakilishi na Wabunge wa CUF kuingia barazani;tamko la CUF lilikuwa na nguvu miongoni mwa watu kwani hakuna Mbunge wake aliyeapa kuiheshimu serikali wala hakuna aliyepokea hata senti toka Barazani kama posho ya kuhudhuria vikao na baadae wakavuliwa nyadhifa zao za kuchaguliwa!
Tuanze maandalizi sasa ya kuiondoa CCM mwaka 2015 na huku tukikazania kwenye mabadiliko ya kikatiba hasa hiki kipengele kisemacho NEC ikitangaza matokeo hayapingwi popote pale.Siku za kuwepo madarakani CCM zinahesabika na hili sakata la Spika ni ongezeko lingine la kura wa wapinzani mwaka 2015.
Mimi nimeanza tayari maandalizi ya kuichukua Kyela yetu inayozidi kudorora,mwanzoni tu mwakani nitawaita waandishi wa habari na wana JF waje kijijini kwangu Talatala-Kyela waione 'manifesto'yangu kuhusu 'take back our Kyela'!