CHADEMA yatoa dira ya Uchaguzi Mkuu 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yatoa dira ya Uchaguzi Mkuu 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jun 18, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG] [​IMG] [​IMG]

  CHADEMA watoa dira ya Uchaguzi Mkuu 2015
  Katika jitihada za kujiandaa na uchaguzi mkuu wa 2015 Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimewataka wanachama wake wenye nia ya kugombea ubunge na udiwani kuwasilisha barua za maombi, picha, vyeti, wasifu na jimbo wanalotaka kugombea kwenye Ofisi ya Katibu Mkuu, tayari kwa maandalizi.Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alisema jana na kuwaagiza wanafunzi ambao ni wanachama wa Chadema wanaohitimu mwaka huu katika vyuo vikuu vya Mkoa wa Dodoma kufanya hivyo mara moja.

  Akihutubia katika mahafali ya kuwaaga wanachama hao wanaosoma vyuo vikuu vya Dodoma, St. John’s na Chuo cha Biashara (CBE), Mbowe, alisema kila anayetaka kugombea awasilishe maombi na kwamba mwaka 2015 wagombea watakuwa wengi kwa kila jimbo ili kuleta ushindani.Alisema taarifa za wagombea hao zitafanywa kuwa siri na watakaojitokeza kugombea 2015 watapata mafunzo maalumu ya uongozi, kampeni na pia watapewa ajenda za kuzungumzia majukwaani wakati wa kampeni.

  “Kama CCM ilidhani kuwa mwaka 2015 kutakuwa na jimbo au kata ambalo mgombea atapita bila mgombea, safari hii wameula wa chuya. Tumefanya operesheni Mtwara na Lindi, tutaendelea na operesheni Dar na Pwani kisha tutaendelea Dodoma, Morogoro na Singida.“Tunataka kujenga mtandao wa chama ngazi za chini, vijijini na mtaani kama CCM inadhani tunacheza makidamakida watashangaa,” alisisitiza Mbowe na kuongeza kuwa lengo ni kuwatambua na kuwajenga viongozi mapema.

  Katika mkutano huo, Mbowe aliwaambia wanachama wa Chadema vyuoni (Chaso) Mkoa wa Dodoma kuwa CCM inawanyanyasa wanafunzi wanaoiunga mkono Chadema na pia inanyanyasa wafanyakazi na wafanyabiashara wanaoonekana kushabikia chama hicho.

  MIKAKATI YA CHADEMA
  Mbowe ametangaza kuwa katika uchaguzi mkuu wa 2015 Chadema haitapokea 'maskrepa' yaliyokosa nafasi katika vyama vingine, biashara ya kupokea watu waliokosa nafasi katika vyama vingine ilikuwa 2010.
  Alisema tabia ya kukimbilia meli dakika za mwisho ilikuwa zamani na kwamba uchaguzi ujao hawatakubali waliokosa fursa kwa vyama vyao kukimbilia Chadema.


  Mipango yao ni kupata wabunge na viongozi bora watakaopimwa kwa dhamira, uwezo na uwajibikaji kwa chama.“Wafanyakazi wanatishiwa kufukuzwa kazi na wafanyabiashara wanafilisiwa na kubambikiwa kodi kisa wameonekana kushabikia Chadema,” alisema.

  Baada ya kuhutubia, wanachama wa Chadema vyuoni mkoani Dodoma wameutaka uongozi wa chuo kuondoa bango la CCM lililoko UDOM kwa maelezo kuwa ni kinyume cha Ibara ya 7 ya Sheria ya Vyuo Vikuu ya 2005.

  Akisoma risala ya wanafunzi Pasquina Ferdinand mwanafunzi wa Shahada ya Ualimu mwaka wa pili, Chuo Kikuu cha St John’s, alisema CCM ina bango ndani ya UDOM kinyume cha sheria ya vyuo vikuu ya 2005, alionyesha kuwa ni sheria inayoihusu Chadema pekee lakini kwa CCM haina tatizo.“Tunaomba umweleze Waziri Mkuu kama siasa haziruhusiwi vyuoni kwanini basi CCM ina bango UDOM kinyume cha sheria wapewe amri ya kuliondoa kwani UDOM siyo mali ya CCM inajengwa kwa fedha za Watanzania,” alisema.

  Akijibu, Mbowe aliwataka wanafunzi wanachama wa Chadema wanaosoma UDOM kumletea taarifa za kunyanyaswa kwa itikadi yao ili azipeleke kwa Waziri Mkuu na awe na ushahidi wa kutosha ili amuulize swali bungeni.  [​IMG]
  Lisu Anena
  Wakati huo huo, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Tundu Lissu, ametangaza kuwa watatumia nguvu ya umma kupinga kufukuzwa wanafunzi vyuo vikuu. “Sisi wazazi tunawajibika kuhakikisha kuwa watoto wetu wanasoma kwa kuizuia serikali isiwanyanyase kwa kuwafukuza wakidai haki yao, hili litafanywa kwa njia ya nguvu ya umma ... tukiona wanafunzi wamefukuzwa UDOM umma uingie mitaani kuandamana kama ni Dar es Salaam watu waingie mitaani tuhakikishe kuwa hapatoshi,” alisema Lissu.
   
 2. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  CHADEMA haina mpinzani 2015!
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mipango ya muda mfupi na ya muda mrefu. Wagombea wanatakiwa kuandaliwa, kujiandaa na kuenga hoja na sera za kipindi cha Uchaguzi ujao.

  Mimi binafsi nina mchango wangu kwa Chama ninachofikiria kitafaa kushika dola next election, nataka kuwasilisha mapendekezo yangu ili yawe chachu kwa wapenda maendeleo watakapoelekea ku -
  cast ballot next election wawe makini nani anafaa na nani ni mchumia tumbo. Pia nini sera nzuri za kwuajali watanzania katika makundi mbalimbali, rika mbalimbali, mipango miji, uwekezaji na mengine.
   
 4. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Chadema inajipanga kiasi ambacho inatisha mwaka 2015 ccm itaona manyoya tuu
   
 5. B

  Bob G JF Bronze Member

  #5
  Jun 18, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Uamuzi huo niwa msingi kuandaa viongozi. Vijana hii ndo nafasi adhimu huwezi ipata kokote vyama vingine ni vya kizee na nafasi kama hizo huzikuti coz kijana huna pesa ya kuhonga kupata ubunge CDM. ccm ushindi unaangalia unene wa mfuko wa fedha/
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  We usiwatishe mno, umeona akina Mwiguru Mchemba alivyotoka povu jingi bungeni leo hadi kasahau kujipangusa akitoka nje ya ukumbi watu wamebaki wameduwaa nini kimempata!
   
 7. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Viva Chama cha Demokrasia


  na Maendeleo!
   
 8. A

  Aristides Pastory JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 348
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Najivunia kukipenda chama cha demokrasia na maendeleo....

  Kwa rehema za mwenyezi mungu awalinde viongozi wote mpaka siku ile ya kupewa nchi yetu ya ahadi(...tanzania tuitakayo..)
   
 9. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #9
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160

  Tulianza na MUNGU na tutamaliza tukiwa na MUNGU wetu aliye hai sasa na hata milele!

  Ngoja tuone kama kodi ya wanainchi waliojilimbikizia kama itawavusha safari hii 2015.

  Zaliwa 1977
  Zika 2015.
   
 10. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #10
  Jun 19, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Ukisoma sura ya sarafu hii ina maana kubwa sana katika uchaguzi ujao. Usiri wa wanaotaka kugombea majimbo ya uchaguzi Tanzania kupitia Chama cha Chadema ni sababu ya walio katika vyama vingine ambao wanashikilia majimbo hayo wenye nia ya kujiunga na Chadema wapenyeze barua za maombi kwa siri chama ili chama kiwatengee majimbo hayo kama wanakubalika. Mbinu nzuri, kwani si rahisi watu kuachia ubunge katikati kwani hawawezi kujua kama watarudi bunge au la, bora bunge litakapohitimishwa na kupata masurufu yao hapo wataelekeza nguvu zao kwenye upinzani ambako walishapeleka maombi, vinginevyo wengine wataandaliwa kugombea maeneo hayo.
   
 11. S

  Sheshejr JF-Expert Member

  #11
  Jun 19, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 435
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Utaratibu mzuri, hongeren makamanda!
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  Jun 19, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Biashara mapema, Chadema si chama cha msimu kama alivyosema Kikwete, labda kutokana na wimbi hili anasita kubadilisha kauli lakini ukweli unabadki hadi kieleweke.
   
 13. z

  zamlock JF-Expert Member

  #13
  Jun 19, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  wanataka kupata na idada ya wanaccm watakao kuja chadema, nimewakubali mtego mzuri pia kwa wana ccm wanaotaka kujiunga chadema 2015
   
 14. M

  Molemo JF-Expert Member

  #14
  Jun 19, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Hongereni sana mashujaa wetu
   
 15. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #15
  Jun 19, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Chadema ni Kati ya Chama ambacho tokea kuanzishwa kwake hakikupaparika kuweka mgombea urais mwanzoni kilitumia muda mrefu kujijenga na kurusha karata yake ya kwanza 2005 na mafanikio makubwa yakaonekana mwaka 2010 kikaporwa ushindi sasa kutokana na historia nzuri na umahiri viongozi wake hainipi shida kutambua ushindi 2015 ni dhahiri tena kwa zaidi ya wabunge 200
   
 16. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #16
  Jun 19, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  mimi naamini mwaka 2015 tanzania itaongozwa na chadema kwani nimebahatika kuzunguka nchi hii hakika iko tayari kuongozwa na chadema..cha msingi mashambulizi yaendelezwe na tuongeze umakini maana hawa mafisadi wanatafuta pakujishika...
   
 17. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #17
  Jun 19, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Wengi hawajaweka wazi dhamira zao kujiengua CCM, bora kutunza majina yao wayajue ili kuhakiki majimbo ambayo hatuhitaji nguvu ya ziada kuyakomboa.
   
 18. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #18
  Jun 19, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Walinitoa jasho kikao chao kilipoamua kwa pamoja kumwangukia Slaa agombee, jambo ambalo ni nadra kwani vyama vingine huwa na ushindani wa kugombania nafasi hiyo nyeti.
   
 19. K

  Katalyeba Member

  #19
  Jun 19, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Bravo Dr. Slaa, mwanzo mzuri, tuendelee kujipanga, maana bila maandalizi, kumbuka kuna majangili waweza kutupora tena. Tuhimize vijana kujiandikish mapema, na hiyo tume ya uchaguzi iwe huru, hapo sawa, ushindi ni wetu
   
 20. kuku dume

  kuku dume JF-Expert Member

  #20
  Jun 19, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 415
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuku dume like this massage.
   
Loading...