Chama cha Chadema leo kupitia mtandao wake maarufu Dar es Salaam ujulikanao kama CHADEMA FAMILY kimefanya tukio kubwa la kihistoria.
Chadema Family huku wakiwa na mavazi yao maalum wamefanya usafi katika hospitali ya mwananyamala na kutembelea wagonjwa.Pia watatoa zawadi mbalimbali kwa wagonjwa.
Mmoja wa Makamanda wa Chadema Family Ally Bananga amesema lengo kubwa la tukio la leo ni kuonyesha moyo wa upendo kwa wagonjwa na wahitaji.Kamanda Bananga ameendelea kusema kwamba alama ya rangi nyekundu kwenye bendera ya Chadema ina maana nyingi ukiwemo upendo kwa masikini,wagonjwa na wahitaji.
Chadema Family wameacha gumzo hapa Mwananyamala na wagonjwa mbalimbali wameonekana wakiwakimbilia Makamanda wa Chadema Family kuwauliza namna ya kujiunga na Chadema.
Mama mmoja mwenye tatizo la miguu ameonekana akiangua kilio alipowaona Chadema Family na kupaza sauti akisema '' Mungu wangu naona kama Nyerere amefufuka''.
Chini ni mavazi ya Chadema Family: