Elitwege
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 5,294
- 10,977
Amani iwe nanyi.
Mara baada ya kamati kuu ya Chadema kukaa na kuja na maazimio ya kukataa kushiriki uchaguzi wa marudio kwenye majimbo ya Singida kaskazini, na Longido vijana wengi bendera fuata upepo waliunga mkono na kumshangilia sana Mbowe.
Ni mbunge wa moshi vijijini pekee Anthony Komu ndio aliyejitokeza hadharani na kupinga uamuzi wa kamati kuu.!!
Mh Anthony Komu alipinga uamuzi wa kamati kuu wa kutoshiriki uchaguzi kwa kutoa hoja kuwa chadema imefanya makosa kususia uchaguzi huo kwa sababu itatoa nafasi kwa ccm kuelezea sera zake kwa wananchi huku chadema ikikosa nafasi hiyo.!
Baada ya Anthony Komu kutoa mawazo yake hayo bavicha wote walimtukana na kumuonya aache mara moja kumkosoa Mbowe la sivyo atafukuzwa kwenye chama aende huko ccm!!
Yani Mh Komu alitukanwa kwa kutoa mawazo yake huru na kusingiziwa amenunuliwa na ccm!!.
Kama wahenga walivyosema lakuvunda halina ubani , baada ya matokeo yale kamati kuu ya chadema iliamua kukaa tena na kuamua kushiriki uchaguzi wa marudio wa kinondoni na Siha.!!
Rai yangu ni kuwaomba bavicha na chadema kwa ujumla kumuomba radhi Mh Komu kwa sababu sasa hivi chadema inatekeleza matakwa yake na kumbe alikuwa sahihi tangu mwanzo licha ya kutukanwa sana na kuitwa msaliti.
Kumuomba radhi mtu ni jambo la kiuungwana sana hapa duniani.
Nawasilisha.