Chadema Kanda ya Pwani imeitangaza siku ya Jumanne kuwa siku maalum ya mashujaa wa kutetea haki na demokrasia katika Taifa.
Akizungumza na vyombo vya Habari vya ndani na nje ya nchi Katibu wa Kanda hiyo Hemed Ally amewataka Watanzania wapenda demokrasia kote nchini kuungana na kusafiri kokote waliko kuja kushuhudia na kuwatia moyo viongozi wakuu wa Chadema ambao hukumu ya kesi yao itasomwa siku hiyo.
Katibu huyo pia amewataka wafuasi wa chama hicho na watanzania wapenda demokrasia wafunge vitambaa vyeupe kwenye mikono yao popote pale walipo kama sehemu ya kuonyesha mshikamano.
Hemed amezungumza kwa kirefu kuhusu makandokando yaliyogubika kesi hiyo tangu mwanzo hadi sasa yenye kila kiashiria cha kutikiswa kwa uhuru wa mahakama.
Mtendaji huyo mkuu wa Kanda ya Pwani amewataka wanachama wa Chadema na wasio wanachama kufurika na kujazana mahakama ya Kisitu mapema siku hiyo na kusubiri uamuzi wa mahakama.
Hukumu ya kesi ya kisiasa ya viongozi wakuu wa Chadema akiwemo Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu John Mnyika itasomwa siku ya Jumanne March 10 saa tatu asubuhi.