CHADEMA Yatangaza makubwa kwenye Hukumu ya viongozi wake wakuu Machi 10, Jumanne

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Chadema Kanda ya Pwani imeitangaza siku ya Jumanne kuwa siku maalum ya mashujaa wa kutetea haki na demokrasia katika Taifa.

Akizungumza na vyombo vya Habari vya ndani na nje ya nchi Katibu wa Kanda hiyo Hemed Ally amewataka Watanzania wapenda demokrasia kote nchini kuungana na kusafiri kokote waliko kuja kushuhudia na kuwatia moyo viongozi wakuu wa Chadema ambao hukumu ya kesi yao itasomwa siku hiyo.

Katibu huyo pia amewataka wafuasi wa chama hicho na watanzania wapenda demokrasia wafunge vitambaa vyeupe kwenye mikono yao popote pale walipo kama sehemu ya kuonyesha mshikamano.

Hemed amezungumza kwa kirefu kuhusu makandokando yaliyogubika kesi hiyo tangu mwanzo hadi sasa yenye kila kiashiria cha kutikiswa kwa uhuru wa mahakama.

Mtendaji huyo mkuu wa Kanda ya Pwani amewataka wanachama wa Chadema na wasio wanachama kufurika na kujazana mahakama ya Kisitu mapema siku hiyo na kusubiri uamuzi wa mahakama.

Hukumu ya kesi ya kisiasa ya viongozi wakuu wa Chadema akiwemo Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu John Mnyika itasomwa siku ya Jumanne March 10 saa tatu asubuhi.
IMG-20200307-WA0076.jpg
 
Hivi vitambaa ni uganga au vina kazi gani kwenye hukumu?!

Watu wakifurika hukumu inabadirika au msomaji wa hukumu ataogopa kuisoma?!

Mikusanyiko hairuhusiwi, ukishawishi watu wajazane mahakamani bila sababu, unawapa chanjo ya CORONA VIRUS?!

Tunapenda haki lakini kuna vitu havina maana kushawishiana, sioni logic kwenye hoja inayopendekezwa.

Vitambaa vyeupe vya nini?!

Mkajazane mahakamani kwasababu gani au nini mta accomplish?!
 
Hukumu inaandaliwa ikulu kisha itasomwa kwenye ile Kangaroo Court sasa nini itakuwa hatima ya Mashinji aliyeenda kuunga mkono juhudi.

Huyo atawapa hao wanao-dictate hiyo hukumu wakati mgumu sana maanake defection yake wameichagiza at a very wrong time. Let us wait and see.
 
Ninaamini siku hiyo hata Jeshi linaweza kutawanywa katika viunga vya mahakama na katika maeneo mengine ya jirani, na mkiona hali hii, basi mjue viongozi wa CHADEMA wanaenda jela ingawa huo hautakuwa mwisho wa upinzani na CHADEMA kwa ujumla bali ndio itakuwa chachu ya kudai mabadiliko katika Taifa hili.
 
Zipo dalili za visasi ama kuihujumu cdm maudhui ya kesi, mwaliko ikulu wa viongozi ikulu,matamshi mbalix2 viongozi ccm. Dawa ya hukumu ya kidhalimu kijani kisivalike mtaani.Ukondoo ukizidi heshima inapotea.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hayo ndio maneno ya kishujaa kabisa. Wakati wa kushare maumivu umefika.
Nyumba hii iwe na mgonjwa basi nyingine iwe na msiba!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Molemo,
Kwa hiyo baada ya hukumu ya kuwafunga viongozi wa juu wa chama. Msajiri wa vyama atatangaza uhakiki wa vyama vitakavyoshiriki uchaguzi mkuu,

Vyama ambavyo viongozi wake wako jela havitaruhusiwa kushiriki uchaguzi mkuu.

Ukiwa na dola unashindwaje kuituimia kubaki madarakani hata kama wananchi hawakutaki- bashru ally
 
Tanzania flag-XXL-anim.gif

tz}chad-1.gif

Tanzania Tanzania Peolpes Power!! Chadema Chadema Peoples Power!!

Risasi Mapolisi Ubambikiwaji wa kesi Kuandamwa na mashushushu pandikizi kukejeliwa na Dakta katibu yote yetu lakini tutatoboa tuko na Mungu
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom