CHADEMA yataka TAKUKURU ichunguze Wabunge wake kutimkia CCM

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,976
Uamuzi wa aliyekuwa Mbunge Serengeti, Ryoba Chacha kutangaza kujiuzulu ubunge na kuhamia CCM, umekifanya chama chake cha zamani cha Chadema kuitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza kuona kama kuna aina mpya ya rushwa ya madaraka ambayo inawavuta wabunge wengi wa chama hicho kukimbilia chama tawala.

Ombi hilo lilitolewa leo na Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema alipozungumza na Mwananchi baada ya Ryoba kutangaza kuhamia CCM kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais John Magufuli.

“Wabunge wamekuwa wakiahidiwa kupewa ubunge wao baada ya kuhamia CCM, hiyo ni aina nyingine ya rushwa, Takukuru waingilie kati suala hilo na kuchukua hatua,” alisema.

Mrema alidai suala la wabunge na madiwani wa Chadema kutimukia CCM haliwapi shida kwa sababu wanajua mazingira yalivyo sasa.

Alidai Mbunge huyo (Ryoba) amefanya kile alichokisema wakati wa mkutano wa Rais Magufuli huko Serengeti na kwamba hawashangazwi na uamuzi wake kwa sababu yeye siyo wa kwanza kuhama.

Chanzo: Mwananchi
 
Kazi mnayo, lle michango ya DJ ya kuchangia chama kila mwezi inabidi iongezeke ili kufidia pengo la wale aanao amia CCM. Hesabu ya tajiri iko palepale mtajijua nyie wabunge mlio baki mna itimiza vipi.

Hahahaaa,,, dhiki ikizidi na mbinu za kuishi huongezeka

Watu wamebaini hadi rushwa mpya dadeki
 
Ni jambo jema kutii Agizo/ amri ya mfalme. Tumlaumu mtoa amri na si mtekelezaji.
 
Kazi mnayo, lle michango ya DJ ya kuchangia chama kila mwezi inabidi iongezeke ili kufidia pengo la wale aanao amia CCM. Hesabu ya tajiri iko palepale mtajijua nyie wabunge mlio baki mna itimiza vipi.

Mkuu;

Hueleweki!
 
CHADEMA mnaonyesha jinsi gani mlivoweak,kabisa Mkurugenzi wa Itikadi anasema TAKUKURU wachunguze wabunge wao kama waMepokea Rushwa au vipi kweliii waliwapa vipi kugombea Ubunge wakati na wala Rushwa!??

Kwa sababu Magufuli ni mkoa rushwa hapendwi hana uwezo wa siasa anatumia hazina alike muweka mpwaye kuchezea demokrasia utawala wake wakishetani amekuwa kutumbukiza hii nchi kwenye lindi la damu
 
Kama wanataka wasafishwe kabisa basi wajaribu kuwatuma hao watumishi wa Ikulu.
Hawajajifunza kwa Mnyeti bado?
Kinachotakiwa kufanywa ni kuwaacha CCM wafanye wanavyotaka kwani muda si mrefu watatoa siri wenyewe bila hata kuwaita Takukuru.
 
CHADEMA mnaonyesha jinsi gani mlivoweak,kabisa Mkurugenzi wa Itikadi anasema TAKUKURU wachunguze wabunge wao kama waMepokea Rushwa au vipi kweliii waliwapa vipi kugombea Ubunge wakati na wala Rushwa!??
Yap, ili anayetoa rushwa ajulikane!
 
Uamuzi wa aliyekuwa Mbunge Serengeti, Ryoba Chacha kutangaza kujiuzulu ubunge na kuhamia CCM, umekifanya chama chake cha zamani cha Chadema kuitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza kuona kama kuna aina mpya ya rushwa ya madaraka ambayo inawavuta wabunge wengi wa chama hicho kukimbilia chama tawala.

Ombi hilo lilitolewa leo na Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema alipozungumza na Mwananchi baada ya Ryoba kutangaza kuhamia CCM kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais John Magufuli.

“Wabunge wamekuwa wakiahidiwa kupewa ubunge wao baada ya kuhamia CCM, hiyo ni aina nyingine ya rushwa, Takukuru waingilie kati suala hilo na kuchukua hatua,” alisema.

Mrema alidai suala la wabunge na madiwani wa Chadema kutimukia CCM haliwapi shida kwa sababu wanajua mazingira yalivyo sasa.

Alidai Mbunge huyo (Ryoba) amefanya kile alichokisema wakati wa mkutano wa Rais Magufuli huko Serengeti na kwamba hawashangazwi na uamuzi wake kwa sababu yeye siyo wa kwanza kuhama.

Chanzo: Mwananchi

Wao walivyompokea ' Fisadi ' Mkuu nchini Tanzania katika Chama chao cha CHADEMA waliomba TAKUKURU wamchunguze?
 
Back
Top Bottom