Chadema yataka jiji la Dar es Saaam liwekwe katika Karantini

Chadema yataka jiji la Dar es Saaam liwekwe katika Karantini

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
104,319
Reaction score
183,636
Chama kikuu cha upinzani Chadema kimeitaka serikali kuliweka katika karantini jiji la Dar es salaam ili kukabiliana na maambukizi ya Covid 19.

Chadema wameshauri kwa kuwa Dar es Salaam ndiyo yenye wagonjwa wengi basi wakazi wake wasitoke nje ya Jiji wala wageni kutoka mikoani na duniani wasiruhusiwe kuingia jijini.

Source Tanzania Daima.
 
Ni wazo zuri kwa kweli, Serikali ifanye hivyo japo itakuwa ngumu sana maana biashara nyingi zinafanyika Dar na mikoa mingine, labda iandae njia nyingine ya kutoathiri biashara ila watu ndo wasihame kirahisi.
 
Wazo zuri, zuia muingiliano wa DAR yenye wagonjwa wengi.... na mikoani ambako hakuna maambukizi.

Ugonjwa huu hauhitaji Maombi bali Maarifa.

Hosea 4:6
watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa.
 
Hii itasaidia kupunguza maambukizi, hasa maeneo ya mikoani. Wa Dar wabaki Dar na waliopo nje ya Dar waendelee na maisha huko. Hii itapunguza maambukizi nchi nzima

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chama kikuu cha upinzani Chadema kimeitaka serikali kuliweka katika karantini jiji la Dar es salaam ili kukabiliana na maambukizi ya Covid 19.

Chadema wameshauri kwa kuwa Dar ndiyo yenye wagonjwa wengi basi wakazi wake wasitoke nje ya Jiji wala wageni kutoka mikoani na duniani wasiruhusiwe kuingia jijini.

Source Tanzania Daima
Ni wazo zuri ila kama hakuna mpango wa kuwapima raia wote wa Dar ili wale wenye maambukizi watengwe kwenye vituo vya tiba Karantini itakuwa haina maana yoyote. Karantini iendane na kupima raia wote walioko kwenye karantini
 
Nashauri watu wasiokuwa na ajira rasmi warudishwe mikoani, ili kupunguza msongamano wa watu

Ila itabidi wapimwe kuthibitisha hawajaathirika na Korona kabla ya kurudishwa.

Vinginevyo itakuwa tatizo linahamishiwa sehemu nyingine.
 
Serikali ipige marufuku mikusanyiko ya ibada, hata mle kariakoo wauza mitumba kila corner no social distance hyo ni hatari Sana Bora kuwe hata na partial lockdown, yafunguliwe maduka ya vyakula na madawa bila hivo Hali itakuwa mbaya tusiwe vichwa ngumu kusingizia umaskini si ajabu Kenya Uganda, na majirani wakidhibiti sisi ndo tuwe tunapata shida ya Corona, though kusali muhimu bila ku practice kanuni za kiafya ni hatari mno

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom